JWTZ
Najua mnafahamu kuwa endapo lolote likitokea Uganda hata leo, Rais anayefuata wa Uganda ni Generali kichaa Muhoozi Kainerugaba.
Najua mnafaham kuwa Muhoozi na Mjomba wake Kagame wanaamini sana kwenye theory ya Expansionism! Kwa Kagame na Muhoozi maeneo ya Afrika Mashariki yanapaswa kuwa nchi moja (imaya moja) na wao kuwa Viongozi wa hiyo nchi.
Sote tunafaham, miaka ya hivi karibuni Kagame na Muhoozi wamekuwa wakiyaimarisha sana majeshi yao. Uimarishaji huu unaenda sambamba na kununua vifaa vya kisasa vya teknolojia ya Juu sana.
Taarifa zinasema kwenye ziara ambazo Kagame amekuwa akizifanya UAE, Uturuki na nchi zingine, amekuwa akinunua vifaa vya kisasa kwa ajili ya majeshi yake ikiwemo Drones, Makombora ya kutungulia ndege na Silaha nyingine za teknolojia mpya na za kisasa.
Wito wangu kwenu!
1. Kuanza sasa wekezeni heavily kwenye mafunzo ya kutumia silaha za kisasa za teknolojia mpya. Mf. Drones makombora ya kisasa na nyinginezo.
2. Kuanzia sasa wekezeni sana kwenye kununua silaha za kisasa za teknolojia mpya. Kuanzia Vifaru, Makombora, Ndegevita na hata Ndege zisizotumia rubani (UAV/Drones)
3. Imarisheni sana Kamandi yenu ya Wanamaji. Nadhani mmejifunza namna Rwanda na M23 walivyoingia Goma na Lubavu kupitia Ziwa Kivu. Kuna haja kubwa sasa kuwa na Kambi Kubwa za Kijeshi za Wanamaji kwenye Maziwa ya Victoria na Tanganyika. Kambi hizi ziwekewe vifaa vya kisasa na bora kabisa vya kivita na Wanajeshi wetu wapewe mafunzo bora kabisa kuhudumu kwenye silaha hizo.
4. Imarisheni sana Uhusiano na Mataifa yenye uwezo mkubwa wa kijeshi hasa Marekani na China. Ingawa mnafanya vizuri kwenye hili, ila ongezeni sana ushirikiano kwenye eneo hili. Pelekeni maofisa wengi kwenye mafunzo vyuo vya nje vya kijeshi wachukue utaalam na waje kuwafundisha wenzao.
5. Mwisho ingawa sio kwa umuhimu, wekezeni basi hata kwenye mavazi mazuri na nadhifu kwa wanajeshi wetu pamoja na other protective gears (Mabuti mazuri na viatu vizuri vya kiaskari). Hivi karibuni naona Askari wetu wanavaa nguo kuu kuu zilizochoka sana. Wafanyeni askari wetu wawe proud kuvaa nguo zao. Watengenezeeni nguo na mavazi mazuri ya kijeshi yanayowafanya sio tu wawe vizuri ila wapendeze na kuonekana askari nadhifu wanaojaliwa vizuri. Kwenye hili mjifunze kwa wenzenu wa Rwanda.
View attachment 3243938View attachment 3243939
View attachment 3243925View attachment 3243927
View attachment 3243921View attachment 3243922View attachment 3243928View attachment 3243924
Mkuu Lord Dennig,
Huyo Muhoozi Kaneirugaba asikutishie simba wa kuchorwa. Hana lolote....,na kimsingi hayo matamshi ya mkwara unayoyasikia toka kwake mara kwa mara yana mtazamo kisiasa.
Ambition yake ni kuwa mkuu wa nchi,..sasa anatumia kauli kama hizo katika kujenga taswira yake kwamba aonekane ni tough guy aliyekomaa japo wengi wanamuona ana utoto mwingi sana.
Kauli zake hizo za vitisho zinafanana na Joyce Banda,aliyekuwa rais wa Malawi ambaye wakati wa kampeni akatoa vitisho dhidi ya Tanzania kuhusu uhalali wa mpaka....na lengo lake likiwa ni kujijenga illi aonekane ni mama wa shoka kwa vile urais wake kabla ya hapo aliupata kwa namna Samia Suluhu Hassan kaupata urais.
Kichekesho ni kwamba rais Jakaya hakumjibu ambayo ilikuwa ni nzuri kidiplomasia, lakini waliomjibu kwa ukali Joyce Banda walikuwa wagombea urais watarajiwa wa Tanzania....bwana Bernard Membe na Edward Lowassa. Na lengo lao nao lilikuwa moja tu ....kujijenga kisiasa ili watu wawaone wanafaa kuwa amiri jeshi mkuu.
Hata hivyo tahadhari uliyoitoa kwamba jeshi lisibweteke....kwamba linatakiwa kuwa ALERT muda wote ni sahihi ikizingatiwa ukweli kwamba katika vita ya Kagera,pamoja na Idd Amin kuanza uchukozi mapema sana mara baada ya kuingia madarakani mwaka 1971, lakini bado Tanzania ilikamatwa OFF-GUARD pale jeshi la Uganda lilipovamia na kuteka eneo la Kagera.
Kulikuwa hakuna jeshi wala kambi ya maana eneo la Kagera au jirani Mwanza ambayo ni maeneo ya karibu na Uganda wakati uchokozi wa Amin ulikuwepo kwa miaka 6 mfululizo ikiwa pamoja na kitendo cha wanajeshi wa Amin kumteka bwana HANS POPE aliyekuwa Mkuu wa polisi mkoa,ukijulikana kama Nyanza wakati huo,pamoja na dereva wake. Dereva aliuawa na kuachwa lakini wakaondoka na Hans Pope ambaye ni baba mzazi wa Zacharia Hans Pope. Mwili wa Hans Pope ulirudishwa Tanzania baada ya vita mwaka 1979,baada ya afisa mmoja wa hospitali ya Mulago, Kampala kuuhifadhi mwili wake katika jokofu na kuwaambia watu fulani wa Tanzania.
Na kutekwa kwake kuliwafanya Zacharia na nduguye wajiunge na jeshi.
Vifaa vingi vilivyitegemewa kwa vita vilikiwa kambi ya Tabora,lakini kikosi ambacho kilikuwa kimeiva na kuwa tayari kivita ni kikosi kilichokuwa kambi ya Mlale, Songea.....,na ambacho kiliweka umakini kujiandaa kusaidia nchi za Msumbji,Zimbabwe kimafunzo .....huku jeshi zima la Tanzania lilikuwa halizidi watu 5000.
Kwa vita ya Kagera Tanzania ilijifunza kwa njia ngumu sana ni namna gani kutokuwa makini na kubweteka kijeshi kunavyoweza kukugharimu.
Na kutokana na hilo funzo gumu..JWTZ limekuwa likifanya yote uliyoyasema. Kwanza kufanya Intelligence ya kutosha kujua uwezo wa silaha na mbinu mpya wanazotumia wanaoweza kuwa mahasimu, kisha kuzifanyia kazi namna ya kuzikabili.
Ikumbukwe,moja ya sababu kubwa ya JWTZ kuishinda Uuganda mwaka 1979 ilikuwa ni kuwa na maafisa wa kijeshi waliosoma katika nchi tofauti tofauti....,Cuba,Israel,America na UK na hivyo kuwa na mbinu na mifumo ya namna nyingi.
Kuwa na ubunifu wa mbinu nyingi katika medani ya kivita na kumsoma kwa usahihi adui yako ni njia bora kabisa ya kushinda vita hasa katika nchi zetu hizi ambazo tunategemea silaha za kununua.....,maana kila mtu anaweza kununua silaha hizo hizo kama mwenzake....tofauti yenu itakuwa ni mbinu na nidhamu ya jeshi.
Umegusia suala la Tanzania kuwa karibu na kama Russia na China kijeshi. Hiyo wala haina haja,kwa vile ikitokea vita usitegemee hizo nchi yoyote kukupa support ya moja kwa moja kama Tanzania ilivyosaidiwa kisilaha na Algeria,huku Uganda ikisaidiwa na Libya.
Kitu cha msingi kabisa kwa Tanzania kukifanya kiusalama miaka ya usoni ni kuzidi kukuza uchumi kwanza, huku ikiwekeza kwa nguvu katika maeneo ya teknolojia maeneo yote ikiwa pamoja na utengenezaji wa silaha tutakazobuni wenyewe. Ukiwa na silaha ulizobuni mwenyewe, ndiyo maana halisi ya SIRI za jeshi....,maana ukinunua silaha kwa mtu huwa hakuna siri.....na ndo maana tunajua nchi fulani imenunua ndege ngapi za kivita na za aina gani,au vifaru aina gani n.k.