General Muhoozi akishika madaraka tutafata Tanzania baada ya kuwa DRC wameisha, tujipange

Hao hawaelew uganda rwanda zimbabwe wanakuja Tz kuja kuchukua mafunzo ya kijeshi na mambo ya diplomasia..
Kwahiyo China inavyokuja kuchukua mafunzo na mbinu mbalimbali ina maana tumewazidi? Hujui kama mataifa makubwa wababe wa vita wanajifunza kwa nchi ndogondogo nyingi tu?
 
Dunia imerudi enzi za kutishana sana,
 
JWTZ

Najua mnafahamu kuwa endapo lolote likitokea Uganda hata leo, Rais anayefuata wa Uganda ni Generali kichaa Muhoozi Kainerugaba.

Najua mnafaham kuwa Muhoozi na Mjomba wake Kagame wanaamini sana kwenye theory ya Expansionism! Kwa Kagame na Muhoozi maeneo ya Afrika Mashariki yanapaswa kuwa nchi moja (imaya moja) na wao kuwa Viongozi wa hiyo nchi.

Sote tunafaham, miaka ya hivi karibuni Kagame na Muhoozi wamekuwa wakiyaimarisha sana majeshi yao. Uimarishaji huu unaenda sambamba na kununua vifaa vya kisasa vya teknolojia ya Juu sana.

Taarifa zinasema kwenye ziara ambazo Kagame amekuwa akizifanya UAE, Uturuki na nchi zingine, amekuwa akinunua vifaa vya kisasa kwa ajili ya majeshi yake ikiwemo Drones, Makombora ya kutungulia ndege na Silaha nyingine za teknolojia mpya na za kisasa.

Wito wangu kwenu!

1. Kuanza sasa wekezeni heavily kwenye mafunzo ya kutumia silaha za kisasa za teknolojia mpya. Mf. Drones makombora ya kisasa na nyinginezo.

2. Kuanzia sasa wekezeni sana kwenye kununua silaha za kisasa za teknolojia mpya. Kuanzia Vifaru, Makombora, Ndegevita na hata Ndege zisizotumia rubani (UAV/Drones)

3. Imarisheni sana Kamandi yenu ya Wanamaji. Nadhani mmejifunza namna Rwanda na M23 walivyoingia Goma na Lubavu kupitia Ziwa Kivu. Kuna haja kubwa sasa kuwa na Kambi Kubwa za Kijeshi za Wanamaji kwenye Maziwa ya Victoria na Tanganyika. Kambi hizi ziwekewe vifaa vya kisasa na bora kabisa vya kivita na Wanajeshi wetu wapewe mafunzo bora kabisa kuhudumu kwenye silaha hizo.

4. Imarisheni sana Uhusiano na Mataifa yenye uwezo mkubwa wa kijeshi hasa Marekani na China. Ingawa mnafanya vizuri kwenye hili, ila ongezeni sana ushirikiano kwenye eneo hili. Pelekeni maofisa wengi kwenye mafunzo vyuo vya nje vya kijeshi wachukue utaalam na waje kuwafundisha wenzao.

5. Mwisho ingawa sio kwa umuhimu, wekezeni basi hata kwenye mavazi mazuri na nadhifu kwa wanajeshi wetu pamoja na other protective gears (Mabuti mazuri na viatu vizuri vya kiaskari). Hivi karibuni naona Askari wetu wanavaa nguo kuu kuu zilizochoka sana. Wafanyeni askari wetu wawe proud kuvaa nguo zao. Watengenezeeni nguo na mavazi mazuri ya kijeshi yanayowafanya sio tu wawe vizuri ila wapendeze na kuonekana askari nadhifu wanaojaliwa vizuri. Kwenye hili mjifunze kwa wenzenu wa Rwanda.
View attachment 3243938View attachment 3243939
View attachment 3243925View attachment 3243927

View attachment 3243921View attachment 3243922View attachment 3243928View attachment 3243924
Huna Akili hasa kwa kusema kuwa CDF Muhoozi ni Kichaa na katika Maelezo yako nimegundua kuwa Wewe ndiyo Kichaa hasa halafu huna unachokijua zaidi tu ya Kuhemka. Uganda ya Museveni na Mwanae Muhoozi na Rais Kagame haina na kamwe haitokuja kuwa na Uadui na Tanzania ambayo si kuwa Wanaiheshimu bali pia Wanaipenda kwakuwa ndiyo iliyowajenga na kuwasaidia vingi. Mtafute Mtu makini akuelimishe kuhusu Urafiki wa Kindugu na wa Kudumu wa Uganda na Rwanda dhidi ya Tanzania kwa Heshima kubwa ya Baba wa Taifa Hayari Mwalimu Nyerere na Waandamizi Wastaafu Wawili ambao bado wako Hai mmoja akiishi Masaki na mwingine Mabwepande.

Nimemaliza.
 
Naizima hoja yako kwa swali 1 tu!

Kama Kagame anaipenda Tanzania kwa nini vikosi vyake viliua askari 2 wa Tanzania na kujeruhi 4 huko North Kivu wakati wanaiteka Goma?
 
M23 msiwachukulie poa, jeshi la congo, afrika kusini, burundi wakisikia m23 wako karibu wanakuja wanaacha silaha wanakimbia, hicho kishindo cha m23 na milio ya mizinga, drones sio mchezo kabisa, jamaa wamejipanga
Wale jamaa hata wakipigwa leo. Wakiondoka wataenda kujipanga tena, wakirudi ni wa moto zaidi.
 
Kama huyu kichaa naye watampa urais basi ntaamini weusi wa Africa mashariki tuna shida na genetically tulifanyiwa manipulation wakabaki wakenya pekee! Huenda wajerumani sio wajinga kubeba mafuvu ya watawala wote wa jadi waliowasumbua miaka zaidi ya 100+ iliyopita
 
Jiandae tu. Huyo ndo next President of Uganda na kwa sasa tu yeye ni De facto President!
 
Urais sio kama kufuga moustache, hata akipewa na baba yake kama urithi atafeli big time, na ataleta chaos kiasi ambacho hata hao uncle zake hawatamvumilia ukiazi wake! So premature...
 
Kama Una "CounterIntelligence" ya 'Maana' hutakiwi kuwa na wasiwasi!!

Nawaza, naweza kuwa sipo sahihi kwa kuwaza hivi; kwa hiyo, ruksa kunikosoa hata kwa kurusha povu poa tu!!!
Huna sababu ya kuogopa kusema unachowaza pedeshee.

Hata mm nawaza kama unavyowaza.

Una Intelligence unaweka Jamiiforums?

Yani unasema hamna njia inayoeleweka kufikisha ujumbe?🤨🤔 mpaka iwe Jamiiforums😂🤔

Inatuambia nn hiyo batanzanie?
 
JWZT Watu sijui mnawachukuliaje.. TISS sijui mnaichukulia aje....

Hapa Africa ukitoa nchi kama 4 hakuna wa kuweza kushinda vita na Tz hayupo..
Sijafika mwisho kusoma nyuzi hii, ila na uhakika wamekudhihaki kwa kuposti Ukweli usiopingika.

🤜🤛
 
JWTZ kama wanaiona hii habari wasiipuuze.... na nyie machawa hizi ndio habari za kumpelekea Samia na mawaziri wake na sio kumpelekea habari zinazohusiana na Lisu anapanga mikakati gani...
Kwanini aliyeleta hii habari yy mwenyewe asipeleke? Au hana visa ya kuingia nchini? Nawaza tyu.
 
Niliwahi kuwa na shemeji yako mmoja mjeda, aliniambia kwamba kwa Tanzania yetu hii tuna military active personel ya 24,000 na reserve ni 80,000 ambapo jumla yake ni kama 104,000 ya jeshi lote tulionao... halafu wakati huo population yetu ni 61m

Huu ni utani wa hali ya juu..... kazi kununua mav8 kila mwaka badala ya kuimalisha ulinzi wa taifa.

Wakati huo Rwanda yenye population ya watu 12m tu wana active personnel 33,000
Mambo mengine kukaa kimya tu, utakuja kuonekana mtutsi sijui mhutu, tuendelee kuiombea nchi yetu ikae ktk amani.
 
Silaha za kisasa na teknolojia vyote vinahitaji fedha kuvipata. Labda kama taifa tuangalie vipaumbele vyetu.

Kama tumeamua kuwekeza kwenye kuwalipa wenza wa viongozi, na kuwajengea mahekalu viongozi wakuu wastaafu, hayo mengine lazima yatakosekana.

You can't have your cake and eat it too.
Ndio maana ya uwepo wa picha hii mkuu?👇
fb_img_1740125218545-jpg.3243927

😂😂😂😂
 
JWTZ

Najua mnafahamu kuwa endapo lolote likitokea Uganda hata leo, Rais anayefuata wa Uganda ni Generali kichaa Muhoozi Kainerugaba.

Najua mnafaham kuwa Muhoozi na Mjomba wake Kagame wanaamini sana kwenye theory ya Expansionism! Kwa Kagame na Muhoozi maeneo ya Afrika Mashariki yanapaswa kuwa nchi moja (imaya moja) na wao kuwa Viongozi wa hiyo nchi.

Sote tunafaham, miaka ya hivi karibuni Kagame na Muhoozi wamekuwa wakiyaimarisha sana majeshi yao. Uimarishaji huu unaenda sambamba na kununua vifaa vya kisasa vya teknolojia ya Juu sana.

Taarifa zinasema kwenye ziara ambazo Kagame amekuwa akizifanya UAE, Uturuki na nchi zingine, amekuwa akinunua vifaa vya kisasa kwa ajili ya majeshi yake ikiwemo Drones, Makombora ya kutungulia ndege na Silaha nyingine za teknolojia mpya na za kisasa.

Wito wangu kwenu!

1. Kuanza sasa wekezeni heavily kwenye mafunzo ya kutumia silaha za kisasa za teknolojia mpya. Mf. Drones makombora ya kisasa na nyinginezo.

2. Kuanzia sasa wekezeni sana kwenye kununua silaha za kisasa za teknolojia mpya. Kuanzia Vifaru, Makombora, Ndegevita na hata Ndege zisizotumia rubani (UAV/Drones)

3. Imarisheni sana Kamandi yenu ya Wanamaji. Nadhani mmejifunza namna Rwanda na M23 walivyoingia Goma na Lubavu kupitia Ziwa Kivu. Kuna haja kubwa sasa kuwa na Kambi Kubwa za Kijeshi za Wanamaji kwenye Maziwa ya Victoria na Tanganyika. Kambi hizi ziwekewe vifaa vya kisasa na bora kabisa vya kivita na Wanajeshi wetu wapewe mafunzo bora kabisa kuhudumu kwenye silaha hizo.

4. Imarisheni sana Uhusiano na Mataifa yenye uwezo mkubwa wa kijeshi hasa Marekani na China. Ingawa mnafanya vizuri kwenye hili, ila ongezeni sana ushirikiano kwenye eneo hili. Pelekeni maofisa wengi kwenye mafunzo vyuo vya nje vya kijeshi wachukue utaalam na waje kuwafundisha wenzao.

5. Mwisho ingawa sio kwa umuhimu, wekezeni basi hata kwenye mavazi mazuri na nadhifu kwa wanajeshi wetu pamoja na other protective gears (Mabuti mazuri na viatu vizuri vya kiaskari). Hivi karibuni naona Askari wetu wanavaa nguo kuu kuu zilizochoka sana. Wafanyeni askari wetu wawe proud kuvaa nguo zao. Watengenezeeni nguo na mavazi mazuri ya kijeshi yanayowafanya sio tu wawe vizuri ila wapendeze na kuonekana askari nadhifu wanaojaliwa vizuri. Kwenye hili mjifunze kwa wenzenu wa Rwanda.
View attachment 3243938View attachment 3243939
View attachment 3243925View attachment 3243927

View attachment 3243921View attachment 3243922View attachment 3243928View attachment 3243924
Kwa hiyo una wasiwasi na hili jeshi ambalo wanajeshi wake hupata hiyo nafasi kwakuwa tu wana kadi za yuvisisiemu?
 
Back
Top Bottom