General Tyre Arusha kugeuzwa mabanda ya biashara kama kwa Mromboo

General Tyre Arusha kugeuzwa mabanda ya biashara kama kwa Mromboo

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
17,434
Reaction score
27,177
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Balozi Waziri Salum amesema anakusudia kubadilisha matumizi ya eneo la kiwanda cha tairi cha General Tyre kilichopo Mkoani Arusha kutokana na kiwanda hicho kusimamishwa uzalishaji tangu mwaka 2007 na kutumia kiasi kikubwa cha Fedha kwa ajili ya huduma muhimu kama maji na Umeme kwa sasa ambapo kwa mwezi hutumika takribani Milioni 27.

Ameeleza kuwa kwa Takribani miaka 19 Wawekezaji kutoka maeneo mbalimbali duniani wamekuwa wakija na Kuondoka katika uwekezaji huo na hivyo hadi sasa hakuna muwekezaji yoyote ambaye ameonesha nia ama utayari wa kuwekeza katika kiwanda hicho.

Katika hatua nyingine Balozi Waziri Salum ameeleza kuwa Mashine na miundombinu mingine muhimu ya kiwanda hicho ni ya kizamani na haiendani na wakati na teknolojia ya sasa katika uzalishaji wa tairi na kuagiza Mashine zifunguliwe na kupelekwa kwenye kiwanda cha kuzalisha vipuli.

Kiwanda cha General Tyre kilianzishwa mwaka 1969 na kuanza kazi 1971 na wakati kinaanzishwa machine hizo ilipewa serikali chini ya Hayati Mwalimu Nyerere zikiwa zimeshatumika na hadi sasa bado zimefungwa katika kiwanda hicho.

Imekuwa mila na desturi maeneno ya wazi kufanywa Car wash, masoko /Mnadani au parking za malori huku tukiuza viwanja vya michezo.

Jangwani ishakuwa ICD, Biafra ishakuwa Yard ya kuuza magari , viwanja vy akufanyia mikutano ya mahubiri bado tu.
 
Back
Top Bottom