Genge la Mafisadi na Viongozi Wastaafu waliotumika kuchafua Utawala wa Magufuli

Madawa ya kulevya yalithibiwa kwa kiasi kikubwa wakati wa JPM. JPM alideal na wale madon wakubwa wengi kimyakimya waliokuwa wanatamba mjini wakati wa Kikwete. Kabla ya awamu ya tano Tanzania ilikuwa kati ya major transit point ya madawa ya kulevya duniani. USA waliomba Tanzania iwa- extradite Kingpin kadhaa Marekani.

Baada ya awamu ya tano madawa yameshamiri tena.
 
Marehemu alikuwa kiongozi shupavu sana. Alifanya mengi ndani ya muda mfupi. Ikiwa ni pamoja na kushughulika na sisi wa vyeti fake.
 
Majizi na mafisadi yaliyojificha serikalini lazima yang'olewe.

Siku mkinipa urais ndio mtajua vile nchi inapaswa kuwa.

Nitakuwa katili kuliko shetani, mpaka majizi yote yanyooke kama RULA.

Magufuli aliwabembeleza sana tena alikuwa na roho ya huruma wakatumia huo mwanya kummaliza.

You must be a ruthless dictator to deal with parasites, unagonga marungu mazito mazito tu.
 
Hayo unayo sema ni kweli.

Ndo maana tunasema the guy was not smart enough for the Job.

You need shap & fine knife to cut a piece of cake, sasa that lilikua panga lile au shoka kabisa ndo mlitaka likate keki? Mwishowe anaishia kuitawanya tuu.

Nauhakika alikua anasshauriwa kila step anayotaka kufanya na watu wa usalama, lkn anashupaza shingo kwa kuona wanampangia cha kufanya.

Jamani, Vijana hata ukipewa taasisi uiongoze kama kuna mabadiriko unafala kufanya na unajua yatagusa ugari wa watu be smart otherwise it will end in tears, na histolia itakuandika kama looser na wao wamewin
 
Sound advice
 
Inaonekana hakuna unachojua.
Kabendera hakufanyiwa ule unyama kwa sababu ya mambo ya Kibiti. Yawezekana ulikuwa unamaanisha Azory Gwanda.

Kabendera, articles zake zilikuwa zinaonesha jinsi awamu ya 5 ilivyokuwa inaharibu uchumi.
 
Lakini nashangaa Magufuli alifariki mwaka 2021 haya ya sasa yanawasaidia nini hawa ndugu?

Kunyoosha mambo October 2025 na kuhakikisha hakuna mtu caliber ya Magufuli anakuja tena kukata mirija yao na kuharibu biashara zao. Mtu kama huyo ataitwa katili, hafuati haki za kibinadamu ni dikteta, mshamba, dikteta uchwara.

Ile kuwasimamia Barrick, na ku-negotiate mikataba ya hovyo watu wa magharibi hawakupenda. Angeweza ku-inspire vizazi vya Waafrika wengi wapiganie rasimali zao. Lissu ndio alikuwa kinara akaingia mzigoni kutetea ili mikataba ya hovyo iliyokuwa kinyume na maslahi ya Tanzania kwa dhihaka kubwa akienda kwenye media kila siku kumtukana Rais wa wakati ule na maneno mengi ya kejeli.

Magharibi na vyombo vyao vya kijasusi wakishirikiana na mafisadi wa Tanzania wanamtaka mtu kama huyu wa sasa aendelee, dalali wa rasilimali za Tanzania, ameuza heka kibao za mbuga, misitu, wanyama wanasafirishwa tena Uarabuni, Bandari imeenda, madawa yamerudi, mikataba mibovu, ufisadi umetamalaki, mikopo ya hovyo na matumizi ya hovyo ya pesa na rasilimali za nchi. Muhimu aside mtu mwenye uchungu na atakaye jitoa kulinda rasilimali za Taifa hili zitumike kwa manufaa ya wananchi wengi.
 
huyu alikuwa mwamba kwelikweli.. sijajua kama kuna sheria Inamruhusu marehemu kushaki iwapo tu atachafuliwa kama haipo inabidi hiki kipengele kiwekwe..Mwamba alileta heshima kila kona huko kwenye local Goverment ilikuwa full kuheshimiana na kuokopana uwekibarua, wamkataba mfupi au mwajiriwa rasmi ilikuwa heshima sahv watu wanatengenezewa zengwe wanafukuzwa kama mbwa aliyeiba mayai hakuna cha malipo yoyote wanatengenezewa makesi hatimaye kuludi kwenye ufukara wa hali ya juu sisema mama hafanyi kazi hapana ila wanamzunguuka na kujuana kwingi sambamba na kulindana katika kazi...R.I.P Magufuli daima tutakukumbuka.
 
Wanaomkataa Magu the Great ni Wapumbavu.
 
Looser hapo ulitaka maanisha nini in english or swahili?
 
Majina ya hao wastaafu na vigogo yako wapi? Au hadi Kabendera ayataje?
 
Marehemu alikuwa kiongozi shupavu sana. Alifanya mengi ndani ya muda mfupi. Ikiwa ni pamoja na kushughulika na sisi wa vyeti fake.


Kuifanya article yako ipate nguvu, inatakiwa ufanye utafiti wa kutosha na uwe na taarifa sahihi.

Program ya kuwadhibiti wenye vyeti fake ilianza tangu wakati wa Kikwete ambapo wenye vyeti fake 9,000 walifukuzwa kazini, lakini ile kampaign haikupewa sana coverage wakati wa Kikwete. Ilikuja kupata nguvu kubwa na kutangazwa na kupambwa sana wakati wa awamu ya 5. Kama unavyofahamu, wakati wa awamu ya 5 ndipo ilipozaliwa hii tabia ya hovyo ya unafiki na uchawa inayoendelea hata sasa, ya mafanikio madogo kisha kupambwa na kukuzwa kwa namna ya ajabu sana.

Uwepo wa wafanyakazi fake halikuwa tatizo lililosababishwa na utawala mmoja bali kama yalivyo matatizo mengi ya nchi hii, lilisababishwa na mifumo, sheria na katiba mbaya ya nchi hii. Ndiyo maana hawa watu, wengine waliajiriwa tangu awamu ya kwanza, wengine ya pili, ya tatu, ya 4 na ya 5 yenyewe. Na wengine kwa kutumia vyeti fake hivyo hivyo wakaenda vyuo vya juu mpaka nje ya nchi, na baadaye wakawa wataalam wabobezi. Kwa hiyo lilikuwa ni tatizo la kimfumo. Na kwa sababu mifumo haijabadilishwa, yawezekana hao wenye vyeti fake wakaendelea kuajiriwa maana wote wawili, Kikwete na marehemu walidili na matokeo ya tatizo bila ya ku-uproot chanzo.

Pamoja na baadhi ya mazuri aliyoyafanya marehemu, lakini kwa kiasi kikubwa makosa aliyoyafanya siamini kama kweli yalisababishwa na watu wengine.

Hivi kweli kushambuliwa Lisu kwa risasi, tuamini ni wastafu ndiyo walisababisha?

Kuuawa Ben Sanane aliyehoji uhalali wa degree ya marehemu, tuseme walisababisha wastaafu?

Kuuawa Azory, kubambikiwa kesi, watu kuporwa pesa yao halali, na kuwafunga watu kwa uonevu, unataka tuamini kuwa ni wastaafu walisababisha ili kumchafua? Haileti mantiki kwa mtu yeyote mwenye akili timamu, hata ile ya kawaida kabisa.
 
Mzee alikuwa na roho mbaya sana nikikumbuka alivyowatesa na kuwachomoa uhai vijana wa TISS Tena Kwa mambo ya Majungu Kwa kutumia vijana wake wa kisukuma namchukoa sana
 
Mzee alikuwa na roho mbaya sana nikikumbuka alivyowatesa na kuwachomoa uhai vijana wa TISS Tena Kwa mambo ya Majungu Kwa kutumia vijana wake wa kisukuma namchukoa sana
Ukiwa msaliti watakuua tu.

Tena kama wewe unaonekana ni bingwa wa uchawi na usaliti, kaa mguu pande watakunyofoa makalio wakayapike nyama.
 
Mwenzako nililipa 10000 tu na mpaka Sasa nadunda.
 
Kabendera kalipuwa mlango .....mtatajana moja baada ya mwingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…