hata mimi say zingine napinga na saa zingine kwa mbali nakubali. Ila mzungu ni hatari hasa akipata upinzani flan. Yeye anataka kuwa top kila sehem.
Mfano mdogo tu Angalia hata Obama licha lakulitoa taifa la marekan kwenye uchumi mbaya alioukuta na kuifanya Sasa hivi dola ina nguvu lakini hathubutu kumpa credit. Angalia wanavyomfanyia ghadafi. Je Iran na north korea wasingekuwa strong wangekua wapi Sasa hivi.
Fidel castro alishawahi kusema tunamiliki silaha za nyuklia siyo kuvamia au kuonea bali kujilinda kutoka kwenu
Mkuu,
Marekani na Urusi walikubaliana mwaka 1962, Mrusi atoe silaha zake za nyuklia hapo Cuba, na Marekani atoe Uturuki na Italia. US Navy walikizunguka kisiwa cha Cuba na Rais Kennedy alikuwa tayari kupigana vita na Mrusi. Baada ya mwezi mmoja, walikubaliana , isingekuwa hivyo, ingekuwa vita vya tatu vya dunia.
Hao jamaa uliowataja nyuma itakuwa wamezidiwa tu na maisha au ni wagonjwa. Kuwa na elimu ya juu na kazi nzuri haihusiki na hali ya afya ya binadamu.
Kuna wasomi wa hali ya juu kama Waziri Mkuu wa UK, Mama Thatcher, anaamka asubuhi anajikuta ubongo haukumbuki kitu. Ugonjwa huo wa Alzheimer's pia ukampata mbabe, Rais Ronald Reagan wa Marekani.
Kuhusu Tiger Woods, alipenda mchepuko sana. Ukikamatwa na mchepuko Ulaya au Marekani, mke anapewa pesa nyingi sana. Ndiyo maana wajanja wanakuwa na makubaliano ya ugawaji wa mali kabla ya ndoa (pre-nuptial agreement).
Paul McCartney wa Beatles alilizwa sana alipoachana na mke wake wa pili, ($48 million) ila sijui sababu yao ya kuachana.
Marekani na UK siyo sehemu nzuri ya kuachana na mkeo kama ni tajiri sana. Matajiri wa Urusi wanaoishi London pia wanalizwa sana wakikamatwa na mchepuko au wakiachana kwa sababu yoyote.
Abramovich inasemekana kalipa $300 million.
Tiger Woods, amelipa $100 million.
Siasa ya Marekani ipo wazi sana kuhusu issue ya mafuta. Rais Carter alishasema bungeni kuwa watafanya kitu chochote kuweza kuwa na mafuta ya kutosha kuendesha uchumi wa Marekani. (Matter of national security). Iran alibanwa na vikwazo vya uchumi mpaka serikali yao ikakubali makampuni ya mafuta ya Marekani yaruhusiwe kusaka mafuta kama zamani. BP ilianza kama kampuni kubwa Iran siyo UK. Shah Reza alikuwa kibaka wa Marekani na UK.
Iran pia ina natural gas, 1 trillion cubic feet, ya pili baada Urusi.
Korea ya Kaskazini bila ya kuwa mpakani mwa China na kumiliki mabomu ya nyuklia, CIA wangempindua Kim Il Sung siku nyingi. Mjukuu wake asingekuwa anaendesha nchi leo.