Genius Hayati Magufuli Hakuongeza Mshahara ila Maisha yaliendana na Kipato

Genius Hayati Magufuli Hakuongeza Mshahara ila Maisha yaliendana na Kipato

Wekeni na Bei za utawala wa kikwete . Hakuna bidhaa ambayo enzi za JPM ilishuka Bei ukilinganisha na utawala wa kikwete
Hata km zilipanda sio kwa kiwango Cha Sasa,swali mbona wao wanaongezeana posho?!!!
Why us huku chini?
Mchele tumennua mpk 1100 Bei y jumla enzi za Magu(Mimi nilikua nauza mchele )nimeacha baada ya huyu ni tozo na vitu kupanda
 
Tatizo mama anampiga vijembe mtanguliza wake kila kukicha, wakati JPM ndiye aliyemtoa huko uswekeni. Kama vile Nape na Makamba wanavyo mnanga JPM.
Kama JPM alivyompiga vijembe JK wakati enzi za JPM ulitokea mfumuko wa Bei wa kufa mtu Hadi Sasa unaendelea tu kupanda
 
Wekeni bei za bidhaa ambazo wakati wa KIKWETE zilikuwa juu na alipoingia MAGUFULI zikapungua bei yake. Wekeni bidhaa hata 5 tu.

Mkizipata niiteni MBWA.

Mimi naanza na moja viwanja.

Mbili kodi za nyumba za kuishi Dar

Tatu vyakula hasa nafaka

Nne pay tv kama dstv subscription fee

Tano kodi za fremu za biashara
 
Kuna ambaye bado anabisha tu kua Hayati JPM alikua ni Genius? Kwamba Hayati JPM alikua ni Mteule wa Mungu aloletwa Kuwainua Watanzania !!.?

Watumishi wa Umma hao , walimu kama nawaona , Mapolisi kama nawaona ( Hawa watu wawili Wana Maisha ya tabu sana ) Lakini ndio wa kwanza kuimba nyimbo za mapambio Kila kukicha !!

Nirudi kwenye Mada, Niliposikia Vifujo na mayowe kisa Rais Samia kasema 23% nilicheka sanaaaa, nikawaonea huruma, pasipo kujali ni kiasi gan Cha Pesa kingeongezwa,

Swali pekee nilojiuliza lilikua ni hii[emoji116]

[emoji117]Je hiyo 23% itapambana na HII INFLATION TUNAYOISHUDIA ?

Petrol Juu, Diesel Juu, Mafuta ya Taa Juu , Mafuta ya Kupikia Juu, Gas Juu sana, Nauli juu, Vyakula ndo usiguse juuu sana na Kuna Njaaa inakuja Iko njiani haijawah shuhudiwa ( endeleen kuruhusu wakulima wauze nje ) , Sabuni Juu, Sukari juuu sana Umeme Juu,

Nchi hiii Kila kitu kipo juuu Kwa Sasa na vinaendelea kua Juu !!

Haya Sasa Nyongeza hiyo hapo, mnasemaje ??. Mmeacha kubweka ?
bado mna la kusema juu ya Chuma JPM??..

HIi Nchi kama lilivyo Bara la Afrika Kwa ujumla, tunakoswa viongozi wenye Maono, watu ni viongozi sababu wanataka waonekane kwenye Rununga, wapigiwe Saluti, Magari ya bure ,Majumba ya bure, Walindwe ,na watumie Pesa za Umma Kwa faida za familia zao na matumbo Yao wenyewe .

katika Nyakati za Sasa, Kwa hakika, Kiongozi aina ya Hayati MAGUFULI ni mwibaa mchungu Kwa watu wachache lakini Mwenye Maana kubwa Kwa Watanzania walio Wengi !!

Hii Nchi inahitaji Viongozi wenye Maono, Akili zilizokomaa na Pevu, watu wazalendo wenye Kupenda na wapo tayari kuifia nchi Kwa faida ya Wananchi wenyewe kama alivyokua JPM.

Sahizi Nchi Haina hata Bei Elekezi, wafanyabiashara wanajiamulia tu wanavyotaka, MAKODI MENGI YA KIJINGA bahati mbaya MAKODI yenyewe yanadeal na watu wakawaida, Wafanyabiashara wanaambiwa ni wawekezaji wazuri wapewe misamaha ya Kodi !!

Kuanzia Leo mkome kabisa Kumfananisha Hayati JPM , Chuma, Genius , Akili kubwa na Hawa mbumbumbu wenu wa Sasa wasotulia nchini Kila kukicha ni Nje ya Nchi utadhan Nchi inajengwa na Mabeberu !!.

Hata Ukope kiasi gani, kama Hauna Upeo, Maono , Usimamizi na Uadilifu utawaumiza Watanzania tu!!.

Hivi bila JPM Leo hii kweli hata haya machache makubwa ambayo tunayaona kama Alana za uongozi wake, Yangekuwepo?

Watumishi wa Umma nanyie acheni Ujinga, kutegemea Mshahara , achen kua na Akili mgando , wekezeni ,muongezee mzunguko wa Pesa kwenye mifuko yenu !!....bila Ivo mtalia sana ,mtalia sanaaa na ndo kwanza Vita ya ' Ukraine na COVID-19 ' kama ilivyo kisingizo Cha mbumbumbu wetu ,ndo kwanza vinaanza !!.

JPM aliwezaje ?
Wengi hawatalielewa bandiko lako.
 
Kwan toka maza kaingia kafanya kipi cha maana??
Royo tuwa,
Tozo
Tunaaminika na tunakopa kwa kwenda mbele,
kafungua nchi, Kaaodoa kero ya machinga mijini,
Kuachiwa wauza ngada walioonewa na mwenda zake
Kuwaondoa Masai loliondo kwa maslah mapana yawanyama wetu, Bandari ya Bagamoyo,
Wazazi kuendelea na shule.
Bwawa la umeme la Stiglaz Goji mchakato unaendelea
No umeme wa Rea.
Bunge live.
Chanjo ya covid,
Wakulima soko huru, Pembejeo soko huru
, kapandisha Watumishi madaraja na mishahara juu. Nk nk... Ni mengi sana siwezi kumaliza.
Mama anaupiga mwingi!
 
Kwa ufahamu wangu, JPM hakufanikiwa kabisa kumanage inflation, zaidi sana vitu kama sukari, mafuta ya kula n.k vilipanda bei mapema sana ktk uongozi wake na havikuwahi kushuka bei. Kwa maoni yangu, JPM alikuwa tu na uthubutu lkn kusimamia uchumi vizuri hata kwake ilikuwa shida. JK ndio ambaye aliweza sana kisimamia uchumi
The best leader ever was Mkapa..

Sent from my itel W5001P using JamiiForums mobile app
 
Angalau sasa mtu unaweza kusema maisha ni magumu na ukawa huru, enzi za Mzee alishawahi kuagiza wakamatwe wanasema vyuma vimekaza na ikawa hivyo. Wote tukakaa kimya na walijidai jeuri wakakiona cha mtema kuni.
 
JPM hakuruhusu wezi na mafisadi kujichotea pesa , lakini yeye ndo akaamua kukomba zile trillion 1.5 ufisadi wa kufuru kabisa
Hilo hamna ambaye amewahi kulidhibitisha humu, inabaki kuwa maneno ya kwenye kanga tu. Tumia Logic ya kawaida tu.

Watu 1O wakidokoa million 5OO kwa ujumla na watu 5OO wakidokoa million 1O kila mmoja hasara inakuwa ni wapi zaidi? Do the Math!!!

Unabariki ufisadi which means kila mtu aibe katika eneo lake. Kuna wafanyakazi wangapi katika hii nchi? Kuna maendeleo yapi yaliwahi kupatikana kwa style hii. Haya after effects ndio hizo sasa kila mtu ana ndevu sasa kama kambale bidhaa hazishikiki sokoni. Mkurugenzi mpaka level ya Waziri wote wakiwa wadokozi kuna nini tena.
 
Mimi naanza na moja viwanja.

Mbili kodi za nyumba za kuishi Dar

Tatu vyakula hasa nafaka

Nne pay tv kama dstv subscription fee

Tano kodi za fremu za biashara
Hahahahahahah bila kusahau bidhaa muhimu inayoitwa utu na heshima baina ya raia. Hii bidhaa ilikuwa ya bei sana ila ilishuka kipindi cha mwamba
 
Mkikamatwa na kwenda kuliwa ndogo mnakuja kulalamika kuwa serikali inaonea raia wake mara sijui watu wasiojulikana. ..ona mashudu, matusi na dhihaka ulizoandika juu ya Rais wa nchi!

Hata kama hukubaliani nae basi kuwa na staha kwenye uandishi wako...shubaamiti
 
Magufuli alisuka mipango ya mauaji ya wakosoajin wake.. alikata moto gafla baada ya kugundua amekwama kwenye uchumi
 
Back
Top Bottom