Genius: Ushauri wa simoni Patrick Ili kukuza soka la Tanzania

Genius: Ushauri wa simoni Patrick Ili kukuza soka la Tanzania

Ila kuna watu watakwambia Karia hafai na ndiye karudisha nyuma mpira wa Tanzania utafikiri Tenga na yule mhujumu uchumi wa Bukoba waliwahi kuchukuwa ubingwa wa AFCON
Awapi ...hata viwanja kipindi hiki Cha karia... kajitahidi kuvilekebisha

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Ila kuna watu watakwambia Karia hafai na ndiye karudisha nyuma mpira wa Tanzania utafikiri Tenga na yule mhujumu uchumi wa Bukoba waliwahi kuchukuwa ubingwa wa AFCON
Alikuwepo mzushi ndolanga
Kasumbua Sana alipokuwa kiongozi
Huyu ofisi ya mpira alihamishia nyumabn kwake kabisa

Ova
 
Simon Patrick (Mwanasheria wa klabu ya Yanga SC)

Hongereni sana @taifastars_ , binafsi siwadai, matokeo haya ndio kipimo chetu cha uwekezaji wetu kwenye soka.

Kwa maslahi mapana ya Taifa, nipende kushauri yafuatayo;

1. Tuziunganishe TFF & ZFF na tuwe na ligi moja bora yenye timu kutoka bara na Zanzibar.

2. Serikali itoe ruzuku kwa timu za vijana kama inavyofanya kwa vyama vya siasa.

3. Serikali ifute kodi na michango isiyo na tija kwa timu za mpira mfano NSSF, WCF, SDL, etc haina tija kwa wachezaji bali huongeza mzigo kwa vilabu, ianzishe kodi maalam ya zuio (WHT) kwa ajili ya wachezaji.

4. Hela zetu za FIFA za maendeleo ya mpira wa miguu zielekezwe kwenye kurekebisha miundombinu ya viwanja hasahasa sehemu ya kuchezea (pitch) ili ligi iwe na ubora zaidi.

5. TFF ianzishe mashindano ya vijana ya kitaifa nje na vilabu na yafanyike kila mwaka sambamba na kurudisha mashindano ya mashuleni.

6. Serikali ianzishe scholarship maalum kwa wanafunzi wote wenye vipaji na kuwataftia akademi nje.

7. Kwakuwa AFCON ya 2027 tunaandaa wenyewe hivo hatutakua na presha ya kufudhu, tuandae timu ya taifa kuanzia leo.

Je ni ushauri Gani unaona ni konk??

#daimambelenyumamwikoView attachment 2883098

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
Wewe uliyeleta hii mada kuwa makini ,kwanini umeandika KUFUDHU badala ya KUFUZU? Uko serious kweli! Unataka watu waseme wakili msomi kakosea?
 
FIFA inapotoa ruzuku huwa inazingatia kuwapo kwa mchezo wa soka wa makundi yote, kama vile wanaume, wanawake, walemavu, vijana na ufukweni. Ndio maana nikasema utawala wa Karia umefanikiwa kuliko tawala zote maana kila kundi hapo limefika hatua nzuri. Hao walemavu ndio wamefuzu hadi fainali za kombe la dunia, jambo ambalo halikuwahi kutokea
Kalia ni mtawala wa kiimla kama Hitler na Mussolini.
 
Back
Top Bottom