GenZ wadhibitiwe vikali vinginevyo Kenya itadumaa na kusinyaa kiuchumi

Mzizi wa haya matatizo ni nini ?

Unaweza kumwambia mtu mwenye Kitu cha Kupoteza (Maisha Mazuri) aingie mtaani na kuhatarisha maisha yake (siongelei wawili au watatu naongelea KIZAZI yaani maelfu kwa maelfu ya watu)?

Utaona kwamba kuna jambo halipo sawa na ili huku tusifike huko ni bora wakaanza kuweka mambo sawa sababu we are a generation behind what Kenya is now facing (na kwa ukubwa wa nchi yetu impact yake itakuwa mbaya zaidi)
 
maisha ya mamilioni ya wakenya yalipotea miaka ya 2007-2008, haya hanayotokea sasa ndio faida ya mauaji yale right?πŸ’

nchi ilishabaribiwa na Tawala zilizotangulia, yanayoendelea sasa ni kujimaliza wenyewe tu na hakuna faida yoyote itapatikana zaid ya watu kupata ulemavu, kupoteza maisha, uharibifu wa miundombinu na kujisababishia wao wenyewe hali ngumu zaid ya maisha, na kujiandalia mazingira ya kupigana tena na tenaπŸ’

ukipoteza maisha kwenye maandamano, maisha ya wengineo yanaendelea kama kawaida, tunakuzika na tunashau πŸ’
 
maisha ya mamilioni ya wakenya yalipotea miaka ya 2007-2008, haya hanayotokea sasa ndio faida ya mauaji yale right?πŸ’
Nope kinachotokea sasa ni kizazi hiki kuona hakina future inayoeleweka yet kuna watu walamba asali mpaka makombo, vijana wametoka Chuo hawana prospects zozote na mfumo umeshakuwa kwamba bila contacts au mzazi wako kuwa na uwezo ni ngumu kutoboa kutoka kwenye poverty cycle....; Ingekuwa ni issue tu ya itikadi au jambo ambalo haliwagusi practically watu wasingekuwa tayari kupoteza maisha yao
Kama status quo haina faida kwao kutokuacha hio status quo ni kuendelea kuumia to infinity..., ni kama kipindi cha utumwa kingeendelea (kama isingekuwa industrial revolution, mpaka leo kungekuwa na mabwana na watwana) ila angalau sometimes hata baadhi ya wakoloni walihakikisha watumishi wao wanashiba kabla ya kuwafanyisha kazi
ukipoteza maisha kwenye maandamano, maisha ya wengineo yanaendelea kama kawaida, tunakuzika na tunashau πŸ’
what if kuishi kwako hakuna tofauti na Jehanamu ? Ndio maana nimekwambie beware of people with nothing to lose...
 
Huu uzi umeletwa na mwana ccm ila una mantiki kenya ni giant ikidumaa nasisi tutadumaa hasa kwakuwa hatuna tiss imara kwenye uchumi hivyo hatuwezi kunufaika na ugomvi wao hivyo ni bora kupakana na kenya imara kuliko kenya iliyodumaa na kuwa a failed state ianze kutengeneza majambazi yasiyodhibitiwa anarchy yaje yatusumbue huku.
 
kweli tuna soma mashahada na maastashahada ambayo hayatusaidii wala kutukomboa kabisa πŸ’

kweli suluhisho la matatizo yetu ni kuandamana, kupora na kuharibu mali na miundombinu tulijenga kwa jasho letu wenyewe, kweli?

sasa ndio a umesoma nini sasa na unapigwa kirungu na polisi kwasabu unalazimisha kupora mali 🀣

kwamba msomi umetafuta mbinu zote za kutatua changamoto zako, ukaona kuandamana ndio solution? dah...
kupoteza uelekeo ni utumwa mazito sana πŸ’
 
una maono ya mbali na ya maana sana gentleman kwa mustakabali mwema wa Kenya na Africa Mashariki kwa ujumla πŸ‘Š πŸ’ͺ

umeona faida za kuwaza na kuchangia mada bila mihemko sasa?
Mawazo yanaflow vizuri, maelezo mafupi yanayoeleweka.....

keep it up πŸ’
 
Yanapo watokea wezi puani,ina kuwa ni muda wa kukimbilia uswiss kula walivyokwiba kipindi chaa amani.
 
waacheni msiwasanue wakijakushtuka nairobi kama bujumbura
wasanuliwe tu kwani kama Africa Mashariki hatuna namna ya kukwepa athari za mahangaiko ya wakenya baadae. tutapata tabu za kiusalama n.kπŸ’
 
kweli tuna soma mashahada na maastashahada ambayo hayatusaidii wala kutukomboa kabisa πŸ’
Ni kosa la waliosomeshwa kwa kutumia kodi na gharama kubwa na bila kutumika kwa kile walichosomeshwa au ni kosa la watunga sera waliopewa dhamana na wameshindwa kutumia hio nguvu kazi ?
kweli suluhisho la matatizo yetu ni kuandamana, kupora na kuharibu mali na miundombinu tulijenga kwa jasho letu wenyewe, kweli?
Kwamba hawa madogo wametoka kwao ili wavunje maduka na kuchoma mali ? Kwamba sababu kuna waliofanya fujo basi hakuna issue yoyote ya maana katika wanachosema madogo ? Au hawa madogo walisomeshwa kwa gharama ili waje kuwa watazamaji wa wachache wakifuja kodi zao?
sasa ndio a umesoma nini sasa na unapigwa kirungu na polisi kwasabu unalazimisha kupora mali 🀣
Kwahio hayo ni maandamano ya waporaji na sio kizazi kilichochoka na majambazi wanaojificha kwenye mwanvuli wa uongozi ?
kwamba msomi umetafuta mbinu zote za kutatua changamoto zako, ukaona kuandamana ndio solution? dah...
kupoteza uelekeo ni utumwa mazito sana πŸ’
All alternatives zimegonga mwamba sababu watawala wanajifanya ni vyura wasiosikia ? Ndio maana nikasema huku wabadilike kabla haijawa too late na kufika point of no return...
 
walikua na hoja za maana mno na zenye mashiko na zilisikilizwa na nyingine kutekelezwa kabisa....

ukatolewa wito na fursa ya majadiliano wamedidinda, wakaibua madai mapya sasa ambayo yatabadilisha kabisa sura ya maandamano ya amani kua ya ghasia....

na ikawa ndiyo mwanzo wa kupoteza uelekeo, zaidi sana kupoteza malengo.
Na sasa hivi wanagawanyika wao kwa walo, pole pole sura za kikabila zimeanza kujitikeza....

na katika ujumla wao wanaonekana ni majambazi, waporaji, wavamia maduka, wezi vibaka na mabandits yasiyo elewa yanataka niini πŸ’

useless kabisa πŸ’
 
Heshima inarudi,na akili zinawakaa sawa wote wanaokwiba na kushindwa kufanya wajibu wao kwa wapiga kura.
ambao ni akina nani sasa na hawakuwahi kupelekwa kwenye vyombo vya sheria? au ndio siasa lawama na chuki tu? πŸ’
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…