Geor Davie ni nani?

Geor Davie ni nani?

Huwezi kunishawishi niamini kama hz ni sadaka tu ndo zinafanya yote haya.

Pale magogoni kuna orodha ya wachungaji wauza sembe.
 
Unapeleka pesa kidogo ulizonazo halafu unabaki klumsifia anakula maisha ya starehe kwa mgongo wa maskini
 
Waumini wake na watangazaji wa redio yake wanamuabudu kuliko wanavyomwabudu Mungu mwenyewe
 
Acha ubishani wa kitoto!
Mleta Uzi kaeleza wazi kuwa ni Askofu tajiri bongo, hayo ya Amerika yanahusiana na nini hapa???
Watu wengine ni wabishi tangu mnazaliwa!
Huyu jamaa ni tajili na vyanzo vya utajiri wake vinatia shaka na hilo ndilo la kujadili sio issue za huko marekani na matajiri wa huko!

Acha kushupaaa na story za mtaani wewe...kwa jinsi ulivyo na mawazo mgando napata wasi wasi na umri wako , pia na uwezo wako wa kupambanua mambo ?uwezo wa kufikili. USA nimetolea mfano tu.
 
Biblia inasema utafuteni kwanza ufalme wa mbinguni na hayo mengine mtazidishiwa, lakini leo hii waumini wengi tunahangaika na mambo ya dunia na mali, tumeacha agizo la kuutafuta kwanza ufalme wa mbinguni, wakati neno liko wazi kwamba itamfaidia nini mtu akiupata ulimwengu wake na akaipoteza nafsi yake?
 
Hivi bongo kila mtu mwenye mbwembwe tu ni bilionea, je huyu mtu akienda mfano USA akataka kuwekeza hapo mradi mkubwa akaambiwa atoe "AUDITED FINANCIAL STATEMENT " ya miaka mitano nyuma iliyokaguliwa na wakaguzi wa kimataifa kama Earns & Young Juu ya mwendendo wake wa ulipaji kodi, makusanyo yake na kila kitu kama TRA wanavyosema, je anaweza kuwa na uthibitisho dhahiri usio na doa/ warakini? coz nchi za wenzetu huwezi kuwa unajiita Bilionea wakati ni mkwepa kodi mkubwa katika nchi na wanaoumia ni watu wa chini wanaofukuzwa kama digi digi kila waendapo kutafuta rizki. Tuacheni sifa za kijinga za kukweza watu mabilionea wakati akienda marekani anajifanya yeye ni mtu hali ya mtu tu. ni mtizamo wangu.... kwani mtizamo wa kumuita mtu bilionea kwa vipicha hivyo vya kuruka ruka ni sawa na yule mkuu wa nchi aliyesema kuwa a na foleni ndefu /jam bara barani hapa dar (msongamano wa magari) ni ishara ya maendeleo... ahaaa wapi.

Mkuu usiihusudu hivyo Marekani na kuifanya ndio kipimo cha kila kitu. Huyu mtajwa kwa hakika ana mabilioni ya shilingi - hiyo ndiyo sifa inayomstahilisha kutajwa kama bilionea.
 
Sasa jamani mnashangaa utajiri wake, na wakati mtu anaponya kwa miujiza, manake yake hata utajiri ameupata kwa miujiza, ila mitume wengine wanashindwa kujifanyia miujiza wenyewe. Huo ulinzi ni swaga na mbwembwe hamna tatizo hapo.
 
Sawa kabisa mkuu, balozi wa mbinguni analindwa na malaika.

Board guards sio wanaolinda uhai wake , ni malaika ukitaka kujua dhamiria kumuua uone nini kitakachokupiga. Hao wapo ili kumpunguzia karaha sasa atatembeaje kila mtu anataka kumshika ,kumgusa,kumvuta mguu ndo kazi yao ili ratiba iende sawa
 
Ufalme wa Mungu watafutwaje?

Biblia inasema utafuteni kwanza ufalme wa mbinguni na hayo mengine mtazidishiwa, lakini leo hii waumini wengi tunahangaika na mambo ya dunia na mali, tumeacha agizo la kuutafuta kwanza ufalme wa mbinguni, wakati neno liko wazi kwamba itamfaidia nini mtu akiupata ulimwengu wake na akaipoteza nafsi yake?
 
Huu ndio mwanzo wa nchi kusambaratishwa. Kuna hela nyingi kutoka nje na si kwa ajili ya mungu ila watu kuchukua madaraka au kugawa wananchi ili kuiba au kumiliki uchumi. Ona Nigeria kuna watu wa aina hiyo wengi na mnaona nchi haitawaliki vurugu tupu. Mtumishi wa mungu anaogopa nini hadi ulinzi kiasi hicho! Hata kama ni mbwembwe haiwashtui watu kuona nini maana yake? Yesu aliishi kimaskini hata kuuliwa kifo cha aibu kufuatana na imani ya wakristo. Je ni kweli hawa maaskofu ni watumishi wa mungu au ni watumishi wa mali?
 
Back
Top Bottom