Mtanzanika
JF-Expert Member
- Feb 27, 2012
- 2,389
- 1,131
...Hivi kuna shehe bilionea!Mungu wa kweli(sio alla)ni mwema angetunuku huo utajiri kwa mashehe wangekuwa wafadhili wa ugaidi.UMASKINI kwa wengine sio wa kupiga vita kama unavyodhania
Kwani hela huwa zatoka wapi mkuu?
Mkuu ndahani​ mimi nimeshuhudia Mama mmoja aliyekuwa na uwezo mkubwa wa kifedha akifilisika kabisa.Kwanza alianza kwenda kwa huyu msanii wakati huo huduma yake ya Ngurumo upako inapamba moto sana nadhani wale wasaidizi wa Dr Mheshimiwa wakajua Mama anazo fedha za kutosha wakamwingiza kwa mtumishi akapewa cheo baada ya muda biashara yake ya kusambaza mikaa Arusha na Kilimanjaro ikayumba sana kwasababu alisomba pesa zote akazipeleka kwa huyu msanii mwisho wa siku akaishia kupelekwa Marekani kuosha macho.Watoto wake hawana mbele wala nyuma baada ya Mama yao kujiingiza kichwa kichwa kwa Msani na tapeli la kimataifa.
Alikuwa nao tena 12
Hajavunja sheria za nchi na anatenda kama Mungu wake anavyomtuma atende. Anaponya wagonjwa kwa jina la Yesu Kristo. Anaihubiri injili kwa ajili ya kuleta amani nchini na duniani kwa ujumla. Yesu Kristo mwenyewe alifanya mengi ya ajabu lakini alikataliwa na mwisho kuuwawa kwa kuwambwa msalabani sebuse mwanadamu wa leo. Hapa duniani hata aje Mungu mwenyewe bado watu watamkataa na kumtukana. Bora kukaa kimya kuepuka laana inayowapa watu umaskini kuliko kuropoka kwa midomo michafu na kuendelea kuwa masikini wa kiroho na kimwili.
Na kwa sababu hiyo si unajua kilichompata?angekuwa na bodyguard unafikiri wale wahuni wangethubutu kumtundika?wacha wajilinde kwani wanajua nabii hapendwi kwao!ila najiuliza hao "clients" zao huchangia kiasi gani mpaka "hawa enterprenuer wa mungu" wanakuwa matajiri hivi? au kuna biashara nyingine kificho inaendelea?
kumwita "nabii wa uongo" ni kosa pia huyo si nabii kabisa yaan hana nasibu yeyote ya kinabii ,ni sawa na mwanamume shoga kumwita "mwanamke wa uongo" hilo ni shoga tu si janajike wala janadume dubwana tu! Ndio hiyo mitapeli ya imani tuliyonayo hapo au mijambazi inayojificha katika kichaka cha huduma za kiroho au 'akili' maana nahisi wadau wao kama wameshikiwa akili zao!
zinaokotwa jalalani!
Ghorofa la Mheshimiwa Dr Nabii na Mtumee Askofu Mkuu Geordavie
Matayo 19:23-24
Hatari Za Utajiri
23 Kisha Yesu akawaambia wanafunzi, Nawaambieni kweli, itakuwa vigumu kwa mtu tajiri kuingia katika Ufalme wa mbinguni. 24 Tena nawaambieni, ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko mtu tajiri kuingia katika Ufalme wa mbinguni.
kwani POPE anaogopa nini na ulinzi wote ule??!
Hivi nabii maana yake nini?
Mbona sijawahi kusikia hawa manabii wa nchi hii wakitoa unabii wowote?
Wewe pimbi jalibu kufikili ata kwa kutumia kitovu,kama huna ubongo.Gazeti lenyewe ni la udaku,mbona mimi naishi karatu sijawahi kuona hata msafara wa M ENDE,hujiulizi,mbona KARATU ipo ARUSHA na Siyo MANYARA?.hali ya kubumba hiyo,tafuta MAZUZU wenzio.
Jamani eee, anakula kwa nafasi yake. Tutapiga keleleee lakini hatusaidii jamii hii ya Tz. Huyu anakula anakojua, je hawa wanaokula kodi zetu kwa Katiba viza mbona hatuwakemei?? Ale tu, alindwe na chopa, azungukwe na magari, lakini zangu hali simpelekei miye. Wanaopeleka wapeleke. Huwez niambia nimpelekee wakati miye nimeenda kwa miguu naye akaja kifahari hivyo.
Jiulize, hiyo gharama ya ulinzi mkuu hivyo ingesaidia makanisa yake mangapi tunayo yaona huku kwetu, yapo kwenye turubali zilizochoka kuliko, si awanunulie mabati?? Nakuambia waumini wake wamelogwa, wameshikwa fahamu zao na akili zao zote. Hao polisi sawa, wanachotaka posho tuuu lakini siwezi enda hapo nikadanganywe mchana peupe.
Ikiwa ana mtumikia Mungu tu na hana mambo mengine yanayoweza kusababishia maadui wengi wa mwilini....ulinzi wote huu mpaka kukodi askari wa nini?
umesahau hawara zake, ambao wengi ni wake za watu.
Anatumia vibaya kodi zetu, hawa maafande hawana shughuli nyingine au ndio wanatafuta allowance zao hapo.
ni muiraq, alikuwa mtangazaji wa redio moja ngaramtoni arusha.. baada ya kupata upako nigeria ndio kawa nabii
Walikuwepo watu ambao ni nje ya hao wanafunzi, pia inaaminika kuwa Yesu alikuwa ni mwanaume wa miraba sita the likes of Samson...
Wanathiolojia wanaamini hivyo kwa kutumia evidence kama ile ya kupindua meza za wanyang'anyi kwenye hekalu, namna Wayahudi walivyopata tabu kumkamata n.k
Hivyo usidhani kuwa Kristo alikuwa mnyonge mnyonge tu...