Geor Davie ni nani?

Geor Davie ni nani?

Hivi kuna shehe bilionea!Mungu wa kweli(sio alla)ni mwema angetunuku huo utajiri kwa mashehe wangekuwa wafadhili wa ugaidi.UMASKINI kwa wengine sio wa kupiga vita kama unavyodhania
...
Nabii, Mtume, Askofu anaishi maisha ya kifahari kwa kuwaminya na kuwadanganya waumini wake kama wewe....haihitaji kwenda shule kutambua utapeli wa hawa mnaowaita manabii....mnakaa mnamuabudu mtu eti nabii...nabii analindwa na watu na jeshi la polisi!?!!
Nabii wa kweli Yesu alikua analindwa na nani!? Hawa manabii wenu feki mbona wanaishi maisha kinyume na Yesu...wamekua kama wanamuziki tu..
Ama kweli wajinga ndo waliwao.
 
Mkuu ndahani​ mimi nimeshuhudia Mama mmoja aliyekuwa na uwezo mkubwa wa kifedha akifilisika kabisa.Kwanza alianza kwenda kwa huyu msanii wakati huo huduma yake ya Ngurumo upako inapamba moto sana nadhani wale wasaidizi wa Dr Mheshimiwa wakajua Mama anazo fedha za kutosha wakamwingiza kwa mtumishi akapewa cheo baada ya muda biashara yake ya kusambaza mikaa Arusha na Kilimanjaro ikayumba sana kwasababu alisomba pesa zote akazipeleka kwa huyu msanii mwisho wa siku akaishia kupelekwa Marekani kuosha macho.Watoto wake hawana mbele wala nyuma baada ya Mama yao kujiingiza kichwa kichwa kwa Msani na tapeli la kimataifa.

mkuu, umetumia maneno makali sana. ni kweli tunapaswa kuwa makini hawa 'manabii' wanaoibuka kila kukicha kwa 7bu ya matendo yake.
 
Alikuwa nao tena 12

wale walikuwa mitume wake, sio walinzi. kama hujui jambo bora ukae kimya kuliko unavyojidhalilisha hapa. hao 12 unaowasema walikuwa wanabeba bunduki wakimlinda?
 
Hajavunja sheria za nchi na anatenda kama Mungu wake anavyomtuma atende. Anaponya wagonjwa kwa jina la Yesu Kristo. Anaihubiri injili kwa ajili ya kuleta amani nchini na duniani kwa ujumla. Yesu Kristo mwenyewe alifanya mengi ya ajabu lakini alikataliwa na mwisho kuuwawa kwa kuwambwa msalabani sebuse mwanadamu wa leo. Hapa duniani hata aje Mungu mwenyewe bado watu watamkataa na kumtukana. Bora kukaa kimya kuepuka laana inayowapa watu umaskini kuliko kuropoka kwa midomo michafu na kuendelea kuwa masikini wa kiroho na kimwili.

mkuu, bila shaka wewe utakuwa mfuasi wa askofu huyu.
 
Na kwa sababu hiyo si unajua kilichompata?angekuwa na bodyguard unafikiri wale wahuni wangethubutu kumtundika?wacha wajilinde kwani wanajua nabii hapendwi kwao!ila najiuliza hao "clients" zao huchangia kiasi gani mpaka "hawa enterprenuer wa mungu" wanakuwa matajiri hivi? au kuna biashara nyingine kificho inaendelea?

huyu yawezekana akawa miongoni mwa 'wajasiriamali' waliomo kwenye orodha ya JK.
 
kumwita "nabii wa uongo" ni kosa pia huyo si nabii kabisa yaan hana nasibu yeyote ya kinabii ,ni sawa na mwanamume shoga kumwita "mwanamke wa uongo" hilo ni shoga tu si janajike wala janadume dubwana tu! Ndio hiyo mitapeli ya imani tuliyonayo hapo au mijambazi inayojificha katika kichaka cha huduma za kiroho au 'akili' maana nahisi wadau wao kama wameshikiwa akili zao!

mkuu, kwa comment hii sidhani kama rungu la admin litakukosa.
 
attachment.php


Ghorofa la
Mheshimiwa Dr Nabii na Mtumee Askofu Mkuu Geordavie

Matayo 19:23-24

Hatari Za Utajiri

23 Kisha Yesu akawaambia wanafunzi, “Nawaambieni kweli, itakuwa vigumu kwa mtu tajiri kuingia katika Ufalme wa mbinguni. 24 Tena nawaambieni, ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko mtu tajiri kuingia katika Ufalme wa mbinguni.”

Asante kwa neno la uzima, mkuu DryRoot. You hit the right point.
 
Wewe pimbi jalibu kufikili ata kwa kutumia kitovu,kama huna ubongo.Gazeti lenyewe ni la udaku,mbona mimi naishi karatu sijawahi kuona hata msafara wa M ENDE,hujiulizi,mbona KARATU ipo ARUSHA na Siyo MANYARA?.hali ya kubumba hiyo,tafuta MAZUZU wenzio.

mkuu mdudu (maggot) hizi hasira zako zimemlenga nani? ungem-quote ili tumjue.
 
Jamani eee, anakula kwa nafasi yake. Tutapiga keleleee lakini hatusaidii jamii hii ya Tz. Huyu anakula anakojua, je hawa wanaokula kodi zetu kwa Katiba viza mbona hatuwakemei?? Ale tu, alindwe na chopa, azungukwe na magari, lakini zangu hali simpelekei miye. Wanaopeleka wapeleke. Huwez niambia nimpelekee wakati miye nimeenda kwa miguu naye akaja kifahari hivyo.
Jiulize, hiyo gharama ya ulinzi mkuu hivyo ingesaidia makanisa yake mangapi tunayo yaona huku kwetu, yapo kwenye turubali zilizochoka kuliko, si awanunulie mabati?? Nakuambia waumini wake wamelogwa, wameshikwa fahamu zao na akili zao zote. Hao polisi sawa, wanachotaka posho tuuu lakini siwezi enda hapo nikadanganywe mchana peupe.

hahahaha! mkuu naona umegalagaza kabisa.....
 
Ikiwa ana mtumikia Mungu tu na hana mambo mengine yanayoweza kusababishia maadui wengi wa mwilini....ulinzi wote huu mpaka kukodi askari wa nini?

inaonekana ni jinsi gani huyu 'nabii' alivyo MPAGANI. kama kweli anamuamini Mungu ni kwanini asimuombe ulinzi mpaka aombe ulinzi wa mwanadamu? angekuwa nabii wa kweli angetegemea ulinzi wa kiroho kuliko ulinzi wa nyama na damu (mwanadamu).
 
Jesus said to him, “If you would be
perfect, go, sell what you possess and
give to the poor, and you will have
treasure in heaven; and come, follow
me.”
 
Anatumia vibaya kodi zetu, hawa maafande hawana shughuli nyingine au ndio wanatafuta allowance zao hapo.

hawa maafande wanatumia kodi za umma kumlinda mtu binafsi kwa maelekezo ya wezi (maCCM).
 
Walikuwepo watu ambao ni nje ya hao wanafunzi, pia inaaminika kuwa Yesu alikuwa ni mwanaume wa miraba sita the likes of Samson...

Wanathiolojia wanaamini hivyo kwa kutumia evidence kama ile ya kupindua meza za wanyang'anyi kwenye hekalu, namna Wayahudi walivyopata tabu kumkamata n.k

Hivyo usidhani kuwa Kristo alikuwa mnyonge mnyonge tu...

taja andiko au kifungu cha biblia kinachothibitisha kuwa Yesu alikuwa na body guards. kama hujui jambo ni bora ukae kimya kuliko unavyojidhalilisha hivi.
 
Back
Top Bottom