Geor Davie ni nani?

Geor Davie ni nani?

Kuna mmoja anaitwa Gwajima kesha umbukua....Alikuwa anakula muke ya mtu..

Gwajima sasa amenunua chopa hataki tena kukanyaga barabara. Kwanini wake za watu wasijigonge? Kumbuka kinachookoka ni roho sio mwili, mwili unabaki na hisia zake kama kawaida
 
Naona unapiga chapuo hapa....Nyie mmelaaniwa na huyo tapeli wenu..

Good nashkuru sana kwa kunilaani pia ujue mti wenye matunda mazuri ndio hulengwa mawe
Unge jiuliza alipokuja Dar alikuja kufanya nini alafu ujijibu mwenyewe!
 
Hosea 4:6

Unaangamia kwa kukosa maarifa....

Hebu nipe historia ya Jehova Shaggggyyyyy......Hii dunia ina vituko vya aina yake..

Nyamaza maana aujui usemalo JEHOVA SHAGI maana yake ni MUNGU APIGAE NGURUMO.
Hapo kale alijifunua kama JEHOVA SHALOM NA JEHOVA NISI lakini sasa amejifunua kwetu kama JEHOVA SHAGI which means MUNGU APIGAE NGURUMO!
 
Nyamaza maana aujui usemalo JEHOVA SHAGI maana yake ni MUNGU APIGAE NGURUMO.
Hapo kale alijifunua kama JEHOVA SHALOM NA JEHOVA NISI lakini sasa amejifunua kwetu kama JEHOVA SHAGI which means MUNGU APIGAE NGURUMO!

Inapatikana kwenye kitabu gani cha Bible..?

Huyu Geordavie karibuni atajiita mungu....
 
attachment.php


ASKOFU na Nabii George David ‘Geordavie' wa Kanisa la Geordavie Ministry ‘Ngurumo ya Upako' lililoko jijini Arusha na Kawe, Dar hivi karibuni alifanya mkutano mkubwa na kutikisa nchi kwa kuwa na magari ya kifahari na ndege aina ya helikopta ‘chopa' iliyokuwa ikirandaranda juu ya anga kulinda usalama wake, Uwazi lina ushuhuda wa kutosha.

attachment.php



Katika mkutano huo uliofanyika Karatu mkoani Manyara, mwandishi wetu alishuhudia msafara wa Geordavie ambaye hutoa huduma ya uponyaji kwa njia za miujiza, ukiwavutia watu wengi kwa kuwa ulikuwa na ulinzi mkali ambao haujawahi kutokea.
GEORDAVIE1.jpg

Mbali ya kuwa na chopa iliyokuwa ikiimarisha ulinzi ambayo ameinunua hivi karibuni, askofu huyo alikuwa na msururu wa magari yenye thamani kubwa yanayomfanya kutajwa kuwa tajiri kuliko maaskofu wengine wanatoa huduma katika makanisa ya kiroho Tanzania.
Akiwa Karatu, mbali na ulinzi binafsi, Geordavie alikuwa akilindwa na askari wa jeshi la polisi, askari kanzu, Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na wale wa usalama barabarani.


attachment.php


Mbali na askari hao wa serikali ambao wamekuwa wakimlinda kila anapofanya mikutano yake, pia Geordavie analindwa na askari wake binafsi hali iliyowafanya baadhi ya watu kuamini kuwa ulinzi wake ni kama ule wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ‘JK'.

"Sijawahi kumuona JK akilindwa na chopa lakini mtumishi wa Mungu Geordavie analindwa na ndege katika msafara wake! Hii ni mara yangu ya kwanza kuona," alisema muumini mmoja ambaye hakupenda kutajwa gazetini.

attachment.php


Hata hivyo, baadhi ya watu walikuwa wakihoji utajiri wa askofu huyo kutokana na fedha nyingi anazozitumia anapofanya mikutano katika sehemu mbalimbali jijini Arusha.
"Tunajua kuwa ni tajiri, lakini anapata wapi fedha za kutumia hivi?" alihoji muumini aliyejitambulisha kwa jina moja la Julius ambaye naye alihudhuria mkutano wa askofu huyo anayetumia kaulimbiu ya Ngurumo ya Upako katika kutoa huduma yake.

GEORDAVIE10.jpg

Pia, waumini wengine walilalamikia ugumu wanaoupata wanapotaka kumuona mtumishi huyo wa Mungu kutokana na ulinzi mkali anaopewa.
"Kila mtu alitamani kumuona mtumishi wa Mungu lakini haikuwezekana kutokana na ulinzi wake kuwa mkali, utajiri wake hakuna mfano, hata kule nyumbani kwake Arusha, anaishi kama Mfalme Daud," alisema Fred Mushi.

attachment.php


Gazeti hili lilimsaka Askofu na Nabii Geordavie kwa lengo la kutaka kujua sababu ya kuwa na ulinzi mkali na kutumia magari ya kifahari ikiwemo chopa katika mikutano anayoifanya lakini simu yake iliita bila kupokelewa.
attachment.php



Bravo Hongera ASKOFU na Nabii George David ‘Geordavie'
 

Attachments

  • GEORDAVIE1.jpg
    GEORDAVIE1.jpg
    42.2 KB · Views: 3,576
  • GEORDAVIE2.jpg
    GEORDAVIE2.jpg
    81.4 KB · Views: 16,524
  • GEORDAVIE3.jpg
    GEORDAVIE3.jpg
    36.9 KB · Views: 16,228
  • GEORDAVIE5.jpg
    GEORDAVIE5.jpg
    44.2 KB · Views: 20,414
  • GEORDAVIE7.jpg
    GEORDAVIE7.jpg
    31.4 KB · Views: 16,176
  • GEORDAVIE9.jpg
    GEORDAVIE9.jpg
    69.8 KB · Views: 16,714
  • GEORDAVIE10.jpg
    GEORDAVIE10.jpg
    33 KB · Views: 3,365
mmmmm hapo sitii neno,
tumuulize mzee wa upako kama haya yanatoka kwa Mungu au virse versa
 
na bado!! dini ina pesa, huyu ndo benn hinn wa bongo!
analindwa na security si Mungu! kazi ipo... afu atakwambia huna haja ya kuweka walinzi nyumbani kwako maana yupo aliye hai mlinzi mkuu anakulinda..
 
Back
Top Bottom