GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Biblia Inasema Msiwaguse Masihi( Manabii) Wangu, Naheshimu Hilo, Ila Biblia inasema pia Mtawatambua (yaani manabii) kwa matendo yao.
Naomba niulize haya yafuatayo kwa mnao mfuatilia mtu anayeitwa George David Kasambale au kama ajiitavyo yeye Mheshimiwa Nabii Mkuu Baba Dokta (Phd) GeorDavie , ni kwa nini mimi kwa binafsi yangu huwa nikisikia mahubiri yake na jinsi anavyohudumu nakwazika!? nakwazika kwa kuona kuwa yanakinzana na neno la Mungu na mafundisho ya Roho Mtakatifu....Je wewe huonaje huyu jamaa!?
Pili, ukimtazama kwa karibu kwenye Tv au karibu naye utaona kuwa uso wake ni kama mweupe (light in complexion) lakini mikono ni miyeusi (black hands) kabisa inakinzana na uso, yaani pepsi mirinda!, je ina maana huyu anajichubua!?...kwa kuna kuna video yake nimeiona youtube ya mwaka 1990 hivi inamuonesha ni mtu wa rangi nyeusi kabisa kabisa tofauti na hii, je anakunywa maji mengi!?...walio karibu nae mtujuze.
Tatu na Mwisho, nimeona kasri alojenga huko Georlander the city of GeorDavie kama anavyojitapa kwenye Channel 10 ni la gharama na anaonekana kuishi lavishing life kuliko muumini wake, nikajiuliza kwa nini alitumia pesa mingi kujijengea makazi yake kuliko kujenga kanisa lake liwe lakisasa ambalo ni nyumba ya Mungu kuliko sasa anakoabudu kwenye hema miaka kama kumi hivi!?....
Kwa kweli nikifikiria hayo na mengine mengi kama tambo zake mbwembwe n.k nakosa imani kama kweli huyu ni mtumishi wa Mungu au la.
Nawasilisha.
Binafsi zaidi tu ya kuona vile anavyobana pua wakati anaongea, anaonyesha magari yake ya uwongo na kweli, nyumba, suti zake huku akionyesha majigambo na dharau zake huwa sioni kingine kutoka kwake. In short anaboa!