Geor Davie ni nani?

Geor Davie ni nani?

Biblia Inasema Msiwaguse Masihi( Manabii) Wangu, Naheshimu Hilo, Ila Biblia inasema pia Mtawatambua (yaani manabii) kwa matendo yao.

Naomba niulize haya yafuatayo kwa mnao mfuatilia mtu anayeitwa George David Kasambale au kama ajiitavyo yeye Mheshimiwa Nabii Mkuu Baba Dokta (Phd) GeorDavie , ni kwa nini mimi kwa binafsi yangu huwa nikisikia mahubiri yake na jinsi anavyohudumu nakwazika!? nakwazika kwa kuona kuwa yanakinzana na neno la Mungu na mafundisho ya Roho Mtakatifu....Je wewe huonaje huyu jamaa!?

Pili, ukimtazama kwa karibu kwenye Tv au karibu naye utaona kuwa uso wake ni kama mweupe (light in complexion) lakini mikono ni miyeusi (black hands) kabisa inakinzana na uso, yaani pepsi mirinda!, je ina maana huyu anajichubua!?...kwa kuna kuna video yake nimeiona youtube ya mwaka 1990 hivi inamuonesha ni mtu wa rangi nyeusi kabisa kabisa tofauti na hii, je anakunywa maji mengi!?...walio karibu nae mtujuze.

Tatu na Mwisho, nimeona kasri alojenga huko Georlander the city of GeorDavie kama anavyojitapa kwenye Channel 10 ni la gharama na anaonekana kuishi lavishing life kuliko muumini wake, nikajiuliza kwa nini alitumia pesa mingi kujijengea makazi yake kuliko kujenga kanisa lake liwe lakisasa ambalo ni nyumba ya Mungu kuliko sasa anakoabudu kwenye hema miaka kama kumi hivi!?....

Kwa kweli nikifikiria hayo na mengine mengi kama tambo zake mbwembwe n.k nakosa imani kama kweli huyu ni mtumishi wa Mungu au la.

Nawasilisha.

Binafsi zaidi tu ya kuona vile anavyobana pua wakati anaongea, anaonyesha magari yake ya uwongo na kweli, nyumba, suti zake huku akionyesha majigambo na dharau zake huwa sioni kingine kutoka kwake. In short anaboa!
 
Binafsi zaidi tu ya kuona vile anavyobana pua wakati anaongea, anaonyesha magari yake ya uwongo na kweli, nyumba, suti zake huku akionyesha majigambo na dharau zake huwa sioni kingine kutoka kwake. In short anaboa!
Acheni hizo bana tunapaswa kufuata mafundisho yake na sio kumwangalia mhubiri alivyovaa au anavyoongea tuache mambo ya kidunia tuwe kiroho zaidi.
 
Acheni hizo bana tunapaswa kufuata mafundisho yake na sio kumwangalia mhubiri alivyovaa au anavyoongea tuache mambo ya kidunia tuwe kiroho zaidi.
Anafundisha jinsi ya kumpa fedha ili uwe tajiri. Sasa ni mafundisho ya Mungu hayo?
 
Hao wanaojiita manabii wameshtukia kua hakuna mungu hivyo wapo kuwatia ujinga nyinyi musio wahi kutapeliwa.

Amini ninacho kuambia.

Hao ni wajanja wa mjini tu (matapeli kwa jina la mungu)

Wanatumia bible kwakua wacristo ni watu rahisi kutapeliwa linapo kuja swala la mungu.
 
Kuna manabii wa aina mbili;
1;Manabii wa Mungu
-hawa walitumwa na mungu kufikisha ujumbe wa kumcha na kuabudu mungu katika kweli.

Waliihamasisha umoja na upendo miongoni mwa waumini

Hawakupenda kujilimbikizia mali ingawa wangetaka wangeweza na wengi walikufa maskini kwa kuzitoa sadaka mali walizozipata.

Kwa manabii hawa wa mungu waumini wote walikua na hadhi sawa na waliohitaji uombezi waliombewa bila ya kutozwa malipo ya aina yoyote.

KWAO MUNGU KWANZA
PESA BAADAE.

2;Manabii wa pesa.
-Hawa wametumwa pesa,mungu wao ni pesa.

Kwao umoja baina ya waumini si kigezo,wapo tayari kuwaponda manabii wenzao wa makanisa mengine kwamba si manabii wa mungu hivyo waumini wasiende kusali.

Kwao kila baada ya kusoma andiko moja jua wazi andiko litakalofata ni kukuimiza kutoa fungu la kumi na sadaka mbalimbali.

Kwao heshima ya muumini huja kwa wingi wa pesa anazomiki.

Kwao toa kwa ajiri ya bwana ni sentensi isiyoisha midomoni mwao.

Wengi ufa na utajiri wa kutisha.

KWAO PESA KWANZA
 
aisee kuna yule mwngne wa Star tv anaitwa prophet billionaire nchi imejaa manabii na mitume kibao
 
Yule Anatafuta fedha tu! Wala hana mpango na mambo ya Mungu!
Kuhakikisha hilo, hakuna hata siku moja utamsikia akikemea dhambi wala kusisitiza uchaji wa Amri kumi za Mungu!
Yeye ni kuwasifia tu waumini wake, ili watoe fedha za kutosha!
Anawatia ujinga anawaita Kizazi chenye Akili
 
GEORDAVIE1.jpg
 
Back
Top Bottom