George Ambangile VS Ali kamwe ni nani mchambuzi bora wa mpira wa miguu nchini Tanzania?

George Ambangile VS Ali kamwe ni nani mchambuzi bora wa mpira wa miguu nchini Tanzania?

kukumsela

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2018
Posts
725
Reaction score
917
Wakuu habari,

Ni mchambuzi yupi mahiri katika uga wa mchezoo wa mpira wa miguu hii battle inamuhusisha George Ambangile kutoka Wasafi FM na Ali kamwe kutoka Azam Média
 
Hilo Wala Halina mjadala ni Ambangile tu. Kuna kipindi fulani niliacha kufuatilia uchambuzi wa mpira wa kibongo niliona miyeyusho tangu nimsikie huyu mwamba nimejikuta siwezi kukosa akiwa anachambua.

Kwanza haoneshi mahaba yake tofauti na wachambuzi wengi wakibongo, La pili anachambua mpira in deep kuanzia mfumo wa team na mengine mengi yupo full package.
 
Wote ni Majanga.......! Yaani hamna Kitu. Hao ni mashabiki kama wengine...... Kuwa mchambuzi Mchezo...!
 
Naona kapewa gari kwa kazi nzuri. Sijapata muda wa kumsikiliza kwa sababu sisililizi redio kabisaaaa. Ali namuona sana Azam
 
Ambangale wa kawaida tu, ni mvinyo mpya sokoni wenye ladha ile ile kama za wengine tu

Kwangu Mchambuzi bora ni mwalimu Alex Kashasha tangu nilivyomuonaga kideoni katika uchambuzi wa michuano ya World Cup 2014 Brazil nilitokea kumpa crédits za juu sana,
Mwengine ni Tigani Lukinja wa EA Radio
 
Edo Kumwembe vipi? Au hachambui?
Are you serious!! Tofautisha mchambuzi Wa mpira na mpenzi Wa soka! Kum we me ni mpenzi wa soka! Nanimfuatiliaji wa soka. Hiyo imemwezesha kuwa mwandishi wa makala nzuri za soka! Uchambuzi wa soka ni taaluma!! Ni sayansi ya soka!!
Hawa wa bongo Hamna kitu! Wamejaa mahaba tu ya soka hawa!! Na wengi wao ni wachumia tumbo!
 
Back
Top Bottom