bombei_safaya
JF-Expert Member
- Oct 12, 2014
- 311
- 286
Na mbeya city walikataa goli la wazi la mayele wala halizungumziwi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jibu zuri kabisaHuyo Messi hakuiteka Spain kwa kulalamika eti mabeki wanamkamia. Alicheza mpira, akaacha takwimu zake ziongee!
Kwa hiyo unataka mabeki wasimkabe mayele siyo!!?...ndezi kweli wewe!Mpira umekua na vituko vya ajabu sana hususani hapa kwetu Tanzania,eti baada ya kuonyesha uwezo mkubwa wa kuzifumania nyavu mchezaji Fiston Mayele limetokea kundi kubwa sana la watu waliotokea kumchukia na kuomba kila dua kwa mungu Mayele asifunge magoli!...
Hii imepelekea hadi sasa kila timu ikiingia kucheza na Yanga safu ya ulinzi wote wanaagizwa kuwa macho na huyu mchezaji mmoja na kupewa special attention ati asifurukute ...
Imekua kawaida sasa Mayele kukabwa na beki wawili,hadi watatu kila ashikapo mpira!..but the guy is so talented kwani ameshalijua hilo nae hucheza kwa juhudi kubwa ktk mazingira haya magumu kwa kuwapenyezea wenzake mipira washinde mabao na tumeona inaleta matokeo..
Wengine wamefikia mbali hata kufikia kutumia nguvu za giza yaani majini yamdhibiti huyu Mayele asifanikiwe kufunga!..unajiuliza hivi mpira umekua ni vita?..michezo ni furaha...michezo ni burudani..michezo ni amani..
Najiuliza Messi,Ronaldo au Lewandonsky wangekua wanacheza ligi yetu hii na ulimbukeni huu na roho mbaya hizi, si wangekua tayari hata tumeshazika miaka mingi?hivi kuna tatizo gani mchezaji akifanya vizuri?wengine wanaumizwa na nini?tutafika wapi ki soka kama nchi?
Mwisho nimpe hongera George Mpole kwa leo kuongoza ktk ufungaji ligi ya Nbc lakini nina imani hata na yeye anajijua kuwa si tishio kwa mabeki.na ndio maana hakuna mabeki wanayehangaika nae kitu kinachompa speed ya kukimbizana na Fiston..tofauti na ilivyo kwa Fiston ambaye hata baada ya mechi ya mwisho Ya Yanga kumalizika akihojiwa aliweka bayana wakati mgumu a aoupitia kwa kukamiwa
Mayele kwa kipindi kifupi ame trend Tanzania,afrika na hata baadhi ya nchi nyingine za asia na europe kwa ushahidi wa video kuliko mchezaji yeyote wa kigeni aliyewahi kucheza katika historia ya nchi hii
Hongera kwake Fiston na atabaki kuwa mshambuliaji tishio nchini kwa sasa hata kama itatokea azidiwe magoli 4.