George Simbachawene, hakupitia JKT?

George Simbachawene, hakupitia JKT?

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
16,419
Reaction score
26,594
Nikiwa kada wa siku nyingi niliyepitia JKT kwa mwaka mzima, nimesitushwa na majibu ya Mh Simbachawene katika ajira za wasomi Polisi.
Nimelazimika kupitia CV yake iliyo ukurasa wa Bunge, hakuna mahali anaonekana kapitia JKT.


HII NI HATARI!

Majibu aliyotoa leo kipindi cha Dk 45 yanaonyesha kabisa mtu asiye na ufahamu wa basics za ajira za wasomi, hasa Polisi.
Ati msomi wa Div 1 hawezi kulinda benki!!!!
Hivi Simbachawene anajua anaongea nini?
Sisi tuliosoma zamani, tena tulifaulu vizuri, kulinda sehemu nyeti ilikuwa sehemu ya kazi.
Leo kuna majenerali waliofaulu vizuri tu na kulinda sehemu nyeti, ni sehemu ya majukumu ya ulinzi.

Nitashangaa kama Simbachawene ataendelea kuwepo sehemu asiyostahili.

Profile​


0.41642400 1485861053.png



Hon. George Boniface Simbachawene​



Member Type : Constituent Member

Constituent : Kibakwe

Political Party : CCM

Phone : +255755375623

P.O Box : P. O. Box 75112, Dar es Salaam

Email Address : g.simbachawene@bunge.go.tz

Date of Birth : 1968-07-05

Education History :​


School Name/LocationCourse/Degree/AwardFromToLevel
Arusha Technical CollegeFull Technician Certificate19891992FTC
University of DodomaMasters in Public Administration20102013Masters Degree
Open University of TanzaniaLL.B20002005Bachelor Degree
Mazengo Secondary SchoolCSEE19851988Secondary School
Pwaga Primary School-19781982Primary School
Mahomanyika Primary SchoolCPEE19831984Primary School

Employment History :​

Company/InstitutionPositionFromTo
Ministry of Energy and MineralsDeputy Minister20122013
Muzdalifah Charitable DispensaryManaging Director20002001
Urafiki Bus Service-DodomaTransport Officer19952000
Future World Vocational Training CentreTeacher/Instructor19971999
Ministry of LandDeputy Minister20132014
Ministry of Energy and MineralsMinister20142015

Political Experience :​


Political PartyPositionFromTo
President's Office Regional Administration and Local GovernmentMinister20152017
Chama cha MapinduziMember of District Political Committee2002Todate
Local Authorities Accounts Committee of the ParliamentMember of the Committee20052010
Administration and Local Governments CommitteeMember20152018
Subsidiary Legislation CommitteeChairman20102012
Constituent AssemblyMember20142014
Parliament of TanzaniaMember of the Parliament20052010
Parliament of TanzaniaMember of the Parliament20102015
Chama cha MapinduziMember of the National General Meeting2005Todate
Parliament of TanzaniaMember of the Parliament20152020
Chama cha MapinduziMember of the Regional Executive Council-Dodoma2005Todate
Chama cha MapinduziMember of the District Executive Council-Mpwapwa2000Todate
Ministry of Home AffairsMinister20202025
Vice President's Office responsible for Union Affairs and EnvironmentMinister20192020
Budget CommitteeChairman20172019
Parliament of TanzaniaMember of the Parliament20202025
 
Nikiwa kada wa siku nyingi niliyepitia JKT kwa mwaka mzima, nimesitushwa na majibu ya Mh Simbachawene katika ajira za wasomi Polisi.
Nimelazimika kupitia CV yake iliyo ukurasa wa Bunge, hakuna mahali anaonekana kapitia JKT.


Nitashangaa kama Simbachawene ataendelea kuwepo sehemu asiyostahili.
Waziri: Tunataka hawa waliopata ufaulu duni fomu foo ili wasipate njia za kuondoka jeshi kwa kigezo cha kwenda kujiendeleza kielimu, watabaki tu wakiendelea kushika bunduki.

Nilivyoelewa Mimi: Ni kweli tumetaka watu wenye ufaulu mdogo fomu foo ili wasiweze kusoma na kutafsiri vizuri sheria zinazowaongoza kufanya kazi / majukumu yao. Sheria ya Jeshi la Polisi na Askari wasaidizi, PGO nk, hii itarahisisha utekelezwaji wa mambo tuyatakayo sisi wenye serikali.
 
Na kwa manufaa ya wengi, wacha niambatanishe post yangu ya awali hapa...

Simbachawene akili hana, au ni kama haijui wizara yake!

Ambacho alihitaji kufahamu na kuongelea ni kwamba, Jeshi la Polisi, na hata Jeshi la Wananchi huwa wanaajiri kutokana na mahitaji.

Kuna wakati huwa wanaajiri hao "aliowaita" Walinzi wa Benki"! Hapa qualifications ilikuwa Kidato cha IV up to Div III (ingawaje nasikia siku hizi ONLY Div IV). Hapa ilikuwa inahitajika zaidi physique kuliko brain!

Wakati mwingine mahitaji yanakuwa ni "watalaamu"

Hii ilitokea sana wakati wa Kikwete na kidogo wakati wa Mkapa (huyu Mwamba sitasahau alichomfanyia braza).

Jeshi la Polisi lilipokuwa linahitaji Wataalamu, huwa wanaajiri watu wenye bachelor degrees! Hawa ilikuwa wakishatoka depo pale Moshi, unapiga lindo lako kama miezi 6 hadi mwaka, kisha unapelekwa Chuo cha Polisi Kurasini kubeba mawe yako!

It's easier to retain graduate aliyepata Div I Form IV kuliko kum-retain Form IV Leaver aliyepata Div II.

So, inawezekana kutokana na nature ya jeshi lenyewe, vitengo vinavyohitaji elimu ya juu vimeshajaa na hivi sasa wanahitaji tu watu wa kukimbizana na CHADEMA mitaani!!

But guys, hiyo sio kwa Jeshi la Polisi peke yake, kwa sababu ukichukua mtu wa Div I, it's obvious itafika wakati dogo atakukimbi tu ili akaendelee na elimu! Ukitangaza nafasi za Bank Teller Form IV Div I, lazima utawapata wa kutosha lakini baada ya muda watagundua walichofanya ni uboya na hivyo watakuachia benki yako ili wakasome!!

Miaka ya nyuma NMB walifanya hiyo mistake... wanaajiri Graduate kisha wanawaweka kwenye vyumba vya kutoa pesa (Tellers)! Kukawa na Employee Turnover ya kutisha kila mwaka... NMB wakashtuka kwamba, at least by the time, huwezi kuajiri graduate umfanye Teller!! Sasa hao Form IV Div I leo hii ukiwaajiri benki, hakuna utakapoweka zaidi ya kuwa Tellers wakati wanajiona kabisa ni undisputable Future Graduates... watakukimbia tu!!

In short, Simbachawene sio tu amelidhalilisha Jeshi la Polisi, bali Wizara ya Mambo ya Ndani na serikali kwa ujumla...

Ni mtu ambae ningetarajia asubuhi ya October 12 watu wajadili ama kutumbuliwa kwake au ku-resign kwake!! Katikati ya mjadala wa PGO, Simbachawene anatuambia kumbe serikali inaajiri watu wasio na uwezo kielimu na ndo maana wanashindwa kuifahamu hata PGO!
 
Hajui kwamba sasahivi mifumo ya IT ndio inalinda maeneo mengi Mambo ya kutumia mabunduki kulinda bank Ni Mambo ya kizamani Sana.

Cyber security, CCTV na mifumo ya kisasa kabisa ya ulinzi ndio kusema Waziri wa Mambo ya ndani aelewi hili?

Ndio maana ukipita makao makuu ya wizara ya Mambo ya ndani unakuta Askari wamebeba mabunduki Sasa pale unalinda Nini baaba ya kuajiri wasomi mkafunga vifaa vya ulinzi .

Pumbavu kabisa!!
 
Wengi katika madaraka hawakugusa JKT , yuko mwingine kule Zanzibar , hata hivyo namtetea Simbachawene , huyu alikuwa konda wa mabasi ya mikoani pale stendi , isingekuwa rahisi kwake kupita JKT
Statement aliyotoa si ya mtu aliyepitia mafunzo yoyote ya ulinxi na usalama.
Inashangaza anakuwaje waziri wa Mambo ya Ndani, a very sensitive position.
 
Wengi katika madaraka hawakugusa JKT , yuko mwingine kule Zanzibar , hata hivyo namtetea Simbachawene , huyu alikuwa konda wa mabasi ya mikoani pale stendi , isingekuwa rahisi kwake kupita JKT
Au walikuwa watoro
 
Ukiwa na tatizo la kimtazamo na kiutendaji toka level ya waziri basi hata performance ya vyombo chini yake inakuwa shaghala baghala.
Tunashangaa hadi level ya IGP hawasimamii matumizi ya PGO.
Najua Kinondoni kuna ofisa upelelezi mwenye Phd, na huyu ni lazima kapitia kulinda benki.
 
Wengi katika madaraka hawakugusa JKT , yuko mwingine kule Zanzibar , hata hivyo namtetea Simbachawene , huyu alikuwa konda wa mabasi ya mikoani pale stendi , isingekuwa rahisi kwake kupita JKT
Kwani alishindwa nini kipindi kile cha wabunge walivyo lazimishwa kwenda jkt?
 
Waziri: Tunataka hawa waliopata ufaulu duni fomu foo ili wasipate njia za kuondoka jeshi kwa kigezo cha kwenda kujiendeleza kielimu, watabaki tu wakiendelea kushika bunduki.

Nilivyoelewa Mimi: Ni kweli tumetaka watu wenye ufaulu mdogo fomu foo ili wasiweze kusoma na kutafsiri vizuri sheria zinazowaongoza kufanya kazi / majukumu yao. Sheria ya Jeshi la Polisi na Askari wasaidizi, PGO nk, hii itarahisisha utekelezwaji wa mambo tuyatakayo sisi wenye serikali.
Kama ni kweli basi jeshi hilo halistahili kuzungumzia mambo ya kiweledi
 
Back
Top Bottom