Nikiwa kada wa siku nyingi niliyepitia JKT kwa mwaka mzima, nimesitushwa na majibu ya Mh Simbachawene katika ajira za wasomi Polisi.
Nimelazimika kupitia CV yake iliyo ukurasa wa Bunge, hakuna mahali anaonekana kapitia JKT.
HII NI HATARI!
Majibu aliyotoa leo kipindi cha Dk 45 yanaonyesha kabisa mtu asiye na ufahamu wa basics za ajira za wasomi, hasa Polisi.
Ati msomi wa Div 1 hawezi kulinda benki!!!!
Hivi Simbachawene anajua anaongea nini?
Sisi tuliosoma zamani, tena tulifaulu vizuri, kulinda sehemu nyeti ilikuwa sehemu ya kazi.
Leo kuna majenerali waliofaulu vizuri tu na kulinda sehemu nyeti, ni sehemu ya majukumu ya ulinzi.
Nitashangaa kama Simbachawene ataendelea kuwepo sehemu asiyostahili.