George Simbachawene, hakupitia JKT?

George Simbachawene, hakupitia JKT?

Na kwa manufaa ya wengi, wacha niambatanishe post yangu ya awali hapa...

In short, Simbachawene sio tu amelidhalilisha Jeshi la Polisi, bali Wizara ya Mambo ya Ndani na serikali kwa ujumla...

Ni mtu ambae ningetarajia asubuhi ya October 12 watu wajadili ama kutumbuliwa kwake au ku-resign kwake!! Katikati ya mjadala wa GPO, Simbachawene anatuambia kumbe serikali inaajiri watu wasio na uwezo kielimu na ndo maana wanashindwa kuifahamu hata GPO!
Hawa ni aina ya viongozi wa taasisi ambao wanalitafuna taifa la Tanzania.
 
Wengi katika madaraka hawakugusa JKT , yuko mwingine kule Zanzibar , hata hivyo namtetea Simbachawene , huyu alikuwa konda wa mabasi ya mikoani pale stendi , isingekuwa rahisi kwake kupita JKT
Freeman alipotoka JKT aliajiriwa kama mlinzi pale bot!
 
Tatizo ni elimu au maslahi? Wanaenda kwenye uofisa kwa sababu ndio kwenye maslahi zaidi ya kulinda bank Waziri anaelewa Kuna senior na junior katika organization yoyote ile ie junior ni kwaajili ya operation zaidi kwa sababu wanajifunza kuanzia chini na senior ni kwaajili ya administration kwa uzoefu wao kwenye kazi, je watoto wa wakubwa wanaoingia katika jeshi wakiwa na ufaulu mzuri au wana viwango vya juu vya elimu mbona wapo wengi au ndio kumaintain status quo za wazazi wao alafu watoto wa wanyonge waendelee kushika bunduki. Hapo hakuna waziri pia nafikiri tufikie mahali tuangalie upya hivi vyeo vya kisiasa vinaalibu taaluma husika
 
Nikiwa kada wa siku nyingi niliyepitia JKT kwa mwaka mzima, nimesitushwa na majibu ya Mh Simbachawene katika ajira za wasomi Polisi.
Nimelazimika kupitia CV yake iliyo ukurasa wa Bunge, hakuna mahali anaonekana kapitia JKT.

HII NI HATARI!

Majibu aliyotoa leo kipindi cha Dk 45 yanaonyesha kabisa mtu asiye na ufahamu wa basics za ajira za wasomi, hasa Polisi.
Ati msomi wa Div 1 hawezi kulinda benki!!!!
Hivi Simbachawene anajua anaongea nini?
Sisi tuliosoma zamani, tena tulifaulu vizuri, kulinda sehemu nyeti ilikuwa sehemu ya kazi.
Leo kuna majenerali waliofaulu vizuri tu na kulinda sehemu nyeti, ni sehemu ya majukumu ya ulinzi.

Nitashangaa kama Simbachawene ataendelea kuwepo sehemu asiyostahili.
Simbachawene alikuwa Kondakta wa mabasi ya Dodoma- Mpwapwa Kisha akawa akahamia Vingunguti ambako alifungua baa karibu na machinjio ya mbuzi.

Kasoma open university, msamehe bure kwa baadhi ya mapungufu
 
Wengi katika madaraka hawakugusa JKT , yuko mwingine kule Zanzibar , hata hivyo namtetea Simbachawene , huyu alikuwa konda wa mabasi ya mikoani pale stendi , isingekuwa rahisi kwake kupita JKT
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
K
Na kwa manufaa ya wengi, wacha niambatanishe post yangu ya awali hapa...

In short, Simbachawene sio tu amelidhalilisha Jeshi la Polisi, bali Wizara ya Mambo ya Ndani na serikali kwa ujumla...

Ni mtu ambae ningetarajia asubuhi ya October 12 watu wajadili ama kutumbuliwa kwake au ku-resign kwake!! Katikati ya mjadala wa GPO, Simbachawene anatuambia kumbe serikali inaajiri watu wasio na uwezo kielimu na ndo maana wanashindwa kuifahamu hata GPO!
CV ya Mbunge ni kujua kusoma na kuandika.Hukohuko ndiko mawaziri hupatikana.Lakini pamoja na hilo ndiyo maana yuko huko aongoze wanaofanana na yeye.

Mimi sidhani kama kweli madarasa ya mapolisi wengi yapo sawasawa kichwani ukilinganisha na wanachokifanya. Ndiyo maana kasema kazi yao ni gwaride kwa maana kuwa, piga,anapiga.Kamata.anakamata.Piga risasi.Anapiga.Ua.Anaua.Bila kujiuliza na kutumia akili kwanini anapiga,kwa nini anakamata.

Hii ndiyo tafsiri yake.Polisi unawezaje kumbambikizia Mtanzania mwenzako kesi ili kufurahisha watawala wa kisiasa halafu ukasimama mahakamani kutoa ushahidi wa uongo,ukaulizwa maswali ukashindwa kujibu, aliyekutuma akakucheka na kukuona huna akili halafu baada ya hapo atakushusha cheo ukalinde majengo ya magereza.au ukamwekea mtanzania mwenzako madawa ya kulevya na silaha mfukoni kwake halafu ukasema umemkamata na silaha na madawa ya kulevya.

Vitu kama hivi ni lazima vifanywe na polisi ambaye hata darasa la awali hakumaliza.Ndiyo maana huyo kiongozi wao sasa anasema hayo.Bado PGO itaweka mambo mengi wazi.

Tutajua tu.
 
Miaka ya nyuma Wassira alikuwa anampelekea Buhohela maswali ya kumuuliza
Vivo hivyo pascal Mayala alikuwa anapelekewa maswali ya kumuuliza Mtendaji wa Tume ya Uchaguzi na mapema kwenye vipindi vyake
Kondakta George kaingia choo cha kike
 
Wengi katika madaraka hawakugusa JKT , yuko mwingine kule Zanzibar , hata hivyo namtetea Simbachawene , huyu alikuwa konda wa mabasi ya mikoani pale stendi , isingekuwa rahisi kwake kupita JKT

[emoji1787][emoji1787][emoji1787]mbona kama alikua omba omba!!!
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
Ni kweli div 1 wataapply vyuo mara baada ya depo na kuja kuwa maofisa ( maofisa hawaendi lindo kwenye mabenki). Point ya waziri iko hapa.

Nadiriki kusema heading ya huu uzi IMEPOTOSHA.View attachment 1971554

sio kila msomi anakuwa officer.

kanuni za polisi hazimlazimishi mwajiri kumpa cheo mtu isipokuwa kwa utaratibu atakaoona unafaa.

wapo wenye degree ni makoplo,masajent na maoficer pia,cha muhimu ni malipo ya elimu husika.
 
Tatizo ni elimu au maslahi? Wanaenda kwenye uofisa kwa sababu ndio kwenye maslahi zaidi ya kulinda bank Waziri anaelewa Kuna senior na junior katika organization yoyote ile ie junior ni kwaajili ya operation zaidi kwa sababu wanajifunza kuanzia chini na senior ni kwaajili ya administration kwa uzoefu wao kwenye kazi, je watoto wa wakubwa wanaoingia katika jeshi wakiwa na ufaulu mzuri au wana viwango vya juu vya elimu mbona wapo wengi au ndio kumaintain status quo za wazazi wao alafu watoto wa wanyonge waendelee kushika bunduki. Hapo hakuna waziri pia nafikiri tufikie mahali tuangalie upya hivi vyeo vya kisiasa vinaalibu taaluma husika
Inshu kubwa ni kwamba,ukiajili digrii utawalipa mishahara mikubwa na posho kubwa,hivyo Serikali ktk kupunguza mzigo tunaaijili f4.
 
Naona unagaika kufanya Damage Control...

Kwahiyo mnatueleza Jeshi la Polisi linaajiri Rejected Materials, wasio na sifa ya kujiendeleza hata kwa kiwango cha certificate ili waendelee kuwa-exploit?

Yaani mnawaambia mabenki yanayotunza mamilioni ya pesa za watu kwamba tunawaletea watu wasio na future yoyote lakini tutawapa silaha ili wakae kwenye mageti yenu?

Yaani mnawaambia wateja wa mabenki kwamba hao mnaowaona kwenye mageti wakati mnaenda kuweka au kutoa mipesa yenu ni watu ambao walikuwa ndo Vilaza Max na wengine ni Vilaza Pro!!

Yaani mnatuambia hata wale waliovuka mpaka na kuingia Malawi wakiwa na silaha, jambo ambalo kisheria ni halali kabisa kutafsirika kwamba ni uvamizi, kumbe hayo nayo ni matokeo ya kuajiri Academically Futureless Citizens, ambao hawawezi kuwa na future yoyote zaidi ya kubeba silaha na kufanya doria!!

Is that what you're trying to justify?

Kwani angesema tu kwamba kila Mtanzania ana haki na wajibu wa kulitumikia Jeshi la Polisiili hatimae kuweza kulinda usalama wa raia na mali zao , ina maana asingeeleweka?

Kwani angesema tu kwamba, kwa nyakati tofauti Jeshi la Polisi huajiri watu wenye sifa tofauti tofauti kulingana na mahitaji ya wakati husika, ina maana asingeeleweka?!

Btw, hiyo screenshot mmemnukuu Simbachawene au mmeandika wenyewe ili kufanya damage control?!

Na kama ni Simbachawene, ina maana mnaendelea kutudhihirishia kushindwa kwake kuchagua hata maneno ya kuongea ni dalili ya kwamba kichwani ni mtupu ndo maana amefikia hata kusema DIVISION 32, aina ya ufaulu ambao sijawahi hata kuisikia maishani mwangu!!
 
sio kila msomi anakuwa officer.

kanuni za polisi hazimlazimishi mwajiri kumpa cheo mtu isipokuwa kwa utaratibu atakaoona unafaa.

wapo wenye degree ni makoplo,masajent na maoficer pia,cha muhimu ni malipo ya elimu husika.
Mwenye digrii kuwa koplo, hapana bhana... hapo kutakuwa na tatizo

Hata hivyo, nakubaliana na wewe kwamba Mwajiri halazimiki kumpa cheo hata kama ana digrii yake hususani kama aliingia kwa kutumia sifa tofauti!! Na Jeshi la Polisi Tanzania ni wagumu kweli kweli kutoa vyeo, na ndio wanaongozaTZ kwa kuwa wagumu wa kutoa vyeo!

Ajabu ni kwamba, ni rahisi sana kula jiwe pale TPDF kuliko Jeshi!! Form VI aliyeingia TPDF ana nafasi kubwa ya kwenda kuchukua Uluteni Usu within 1 year lakini kwa Polisi, na Form VI yako, hesabu Jiwe utalipatia uzeeni unless ukasomee kozi zao pendwa kama vile za afya au sheria!!

Kuna mambo mawili au matatu yanayoweza kumfanya mwenye digrii asiwe na cheo!!

Mosi, inawezekana kabisa ajira ambazo zilitangazwa ni kwa ajili, mathalani Form IV au Form VI lakini kutokana na kupigika mtaani, mtu na digrii yako unaenda tu, ama kwa kutumia cheti cha Form IV au VI huku ukitarajia ukishaingia kwenye system utatoa cheti chako cha bachelor ili hatimae ufikiriwe kupanda cheo... hapo utasota sana!!

Utasota sana kwa sababu, Jeshi la Polisi linapoamua kutaka wenye digrii basi wanakuwa wamejipanga in advance kwamba, hawa wakishatoka Depo Moshi, "watapiga lindo" kama mwaka mmoja ili wazijue kazi za polisi na baada ya hapo watapelekwa Kurasini kuchukua dongo!!

Of course, kutokana na factors mbalimbali, wengine wanaweza kuwahi zaidi na wengine watachelewa lakini sio sana!!
 
Simbachawene alikuwa Kondakta wa mabasi ya Dodoma- Mpwapwa Kisha akawa akahamia Vingunguti ambako alifungua baa karibu na machinjio ya mbuzi.

Kasoma open university, msamehe bure kwa baadhi ya mapungufu
Kwa mtaji wa CV aliyonayo tunamsamehelakini hafai kuongoza wizara ya mambo ya ndani.
 
Nikiwa kada wa siku nyingi niliyepitia JKT kwa mwaka mzima, nimesitushwa na majibu ya Mh Simbachawene katika ajira za wasomi Polisi.
Nimelazimika kupitia CV yake iliyo ukurasa wa Bunge, hakuna mahali anaonekana kapitia JKT.

HII NI HATARI!

Majibu aliyotoa leo kipindi cha Dk 45 yanaonyesha kabisa mtu asiye na ufahamu wa basics za ajira za wasomi, hasa Polisi.
Ati msomi wa Div 1 hawezi kulinda benki!!!!
Hivi Simbachawene anajua anaongea nini?
Sisi tuliosoma zamani, tena tulifaulu vizuri, kulinda sehemu nyeti ilikuwa sehemu ya kazi.
Leo kuna majenerali waliofaulu vizuri tu na kulinda sehemu nyeti, ni sehemu ya majukumu ya ulinzi.

Nitashangaa kama Simbachawene ataendelea kuwepo sehemu asiyostahili.
Huyo aliishia darasa la saba,kilichofuata ni elimu ya kuunga unga.
 
Huyu konda wa mabasi haelewi kwamba kazi ya ku enforce sheria inahitaji weledi......
 
Back
Top Bottom