George Simbachawene, hakupitia JKT?

Walimu wanafundisha kwa bidii ili wanafunzi washinde.
Wanafunzi wanasoma kwa bidii ili washinde.
Serikali inawekeza pesa ili wanafunzi washinde.

Hii ya kutaka ambao hawakufaulu vizuri imekaaje?

Kama ndivyo, shule za elimu ya juu tunafungua za nini?

Sent from my Infinix X624 using JamiiForums mobile app
 
Huyu mimi mara zote huwa namuona ni kiongozi mzuri sana na anayo nidhamu hasa ile ya 'kiuongozi', na anaheshimu sana watu anaowaongoza. Huyu tunatakiwa tuendelee naye mpaka 2025 halafu tutaona hapa katikati atakwendaje, kama kweli ana tatizo litadhihirika tu. Hata hivyo, mimi naona mambo mengine yanaweza kuwa ni mitego ya kisiasa tu, watu wengine hawajui kuseleleka maneno mdomoni lakini kazi wanafanya vizuri. Wengine wapo wana maneno mengi matamu utashangilia lakini kazi hamna
Watu wa kazi huwa siyo wazuri sana kwenye majukwaa ya mahojiano, na mara chache sana huwa wanapenda mahojiano. Huyu mtu mimi huwa namuona ni mtu wa kazi, siyo wa maneno na picha za kwenye TV.
Mama amesema tutakwenda kwa mtindo wa matendo makali, na si maneno makali. Simbachawene hana maneno makali. Kama hana maneo makali, je kuna anayeweza kuthibitisha pia kuwa hana matendo makali?
Tuwaombeeni viongozi wetu wamsaidie Mama vizuri, tusiwe kila wakati tunam-prompt Mama ili awabadilishe viongozi. Tuwaacheni wastabilize ili wafanye kazi vizuri, Mama aende nao wote kama walivyo muda huu mpaka hiyo 2025! Baada ya hapo sasa yeye mwenyewe atakuwa amejifunza mengi atafanya kama anavyoona inafaa.
Tusitake sana Mama awe anabadilisha badilisha viongozi, siyo afya sana kwetu sisi tunaoongozwa
 
Aliemteua kapita JKT?
 
Interviw yake Dk45 imemuumbua kiuwezo na kifikra.
Sidhani kama yuko mentally equipped kuongoza wizara nyeti kama aliyonayo.
 
Interviw yake Dk45 imemuumbua kiuwezo na kifikra.
Sidhani kama yuko mentally equipped kuongoza wizara nyeti kama aliyonayo.
Lakini Wizara amekuwa nayo kwa kipindi sasa na hatujawahi kusikia chochote cha ajabu. Kwa hiyo wewe unataka maneno makali badala ya matendo makali, si ndiyo?

Kuna mtu mmoja alikuwa na akili nyingi sana, akaulizwa swali na wanafunzi wake kwamba "mwalimu tufanye nini ili tuweze kuelewa na kuwa wazuri kiakili na kifikra kama ulivyo wewe"? Mwalimu alijibu swali akasema "attention, attention", which was the perfect answer ever ila ukiangalia kwa jicho jingine, the obcvious ni kwamba huyu mwalimu hakujibu swali kwa ufasaha na hivyo kwa akili ya juu juu tu, mtu anaweza kumuona mwalimu kuwa alifeli kujibu swali wakati siyo kweli

Twendeni kwa matendo makali, na si kwa maneno makali; Mama amesema hivyo!
 
Sisiemu hoyeeeee...teh teh
 
pole sana kauri ya ovyo sana kwa hiyo div 1 awawezi beba silaha au kupokea mafunzo,k
 
Mkuu kati ya mambo yanayoiumbua wizara ni hii kesi ya ugaidi ya Mbowe.
Kwamba Jeshi la Polisi hadi maofisa hawajui kutumia PGO its a revelation!
Anayesimamia UBORA wa jeshi la Polisi kwa kiasi kikubwa ni wizara.
Sasa kama waxiri msono yake ni kama yale ya katika Dk45 basi we have very low standards.
Wenzetu kama FBI ya Marekani, mlinda benki anaweza kuwa agent aliyewekwa pale kuchunguza issues serious na long term, na ana Div1.

Na kwa mashirika bora kiulinzi duniani polisi siyo tread of the mill tu, ni proffessionals.
Tukikubali ku equate polisi na virungu tu, basi we have very low expectations of our law enforcers.
 
Najaribu Kuwaza.Ila Mama Yetu Samia Naimani hili limemfikia atalifanyia kazi,Mama anatoa mikopo,Mama anaboresha Elimu kujenga Madarasa,kuajili Walimu wapya.Naimani kubwa Wasaidizi wa Mhe.Rais watakuwa wamemshauri kitu Hon.Waziri.Angalau atoke aitolee ufafanuzi kauli yake
 
Hivi mkuu kosa la waziri ni kusema ukweli ama?Mbona Watanzania hatupendi ukweli lakini?
 
Naendelea kumwelewa waziri kwani baada ya depo angejikuta hajasolve tatizo bali kaongeza.
Hao div 1 wangeenda karibu wote kuwa maofisa na askari waliohitajika kwa kazi za kawaida ingeendelea kuwa ni tatizo.

Kuliweka sawa swala hili yatubidi turudi kwenye sera zetu na mifumo yetu iliyotengenezwa tangu zamani. Na tusisahau kuihusisha budget (hela) kwani hauwi bora burebure tu.


Inawezekana kuwa hivi: Askari baada ya kuajiliwa, kwa wale ambao hawakufika vyuo wanapelekwa vyuoni mara baada ya depo halafu ndipo anakuja kulitumikia jeshi.
Div 4 wanatengenezewa utaratibu utakao wapeleka chuo, kisha nao watarudi kulitumikia jeshi.
Hili linawezekana(tatizo hela)

Kama askari wote watakuwa na elimu zinazokaribiana utaratibu wa kuwa maofisa itabidi ubadirishwe ili kuepukana na hii hali ya maaskari wasomi karibia wote wanakuwa maofisa na hivyo kukosa askari wa kazi za kawaida.
 
Siyo GPO ni PGO.
 
Kile kipindi kilirushwa na ITV jana usiku saa tatu,cha ajabu ni kwamba Mh.Waziri mpaka sasa hivi hajaomba msamaha kwa matamshi yake.
Polisi moja ya jukumu lao ni kulinda wananchi na mali zao na tukianza kuwa nyanyapaa....
 
Kama sikosei, wote waliomaliza form kuanzia mwaka 1991 todate hawakupita JKT, Simbachawene anaangukia kundi hilo, check mwaka aliomaliza Technical school, maanake before miaka hiyo ulikua ukimaliza form 6 au technical collage kama alivyo fanya huyu jamaa then jeshini hawakwenda, this include myself, serikali ya Mwinyi ilikua imeelewemewa, hakukua na pesa kabisa so baadhi ya mambo ambayo hayakua ya muhimu sana yaliachwa. Utakumbuka pia ni miaka hiyo hiyo hata nauli zile tulikua tunapewaga wanafunzi wa boarding ziliacha kutolewa hasa kwa wanafunzi waliokua wanatoka nje ya mikoa 2 hadi ilipo shule, baadae ndio wakafuta kabisa. I think waziri wa fedha alikua bwana Steven Kibona
 
yote hii ni kutokana na kukosa kazi, mnaanza kutamani mpaka na kazi za form four failure.
Mkuu unaandika kwa vile una haki hiyo, lakini wewe kama hao failures unaowasema, ambao mko sawa kifikra mnashindwa kuelewa kuwa ulinzi wa nchi hii huwezi kuwaachia
low performers.
 
Kuna watu ni wa hovyo sana kwenye hii nchi.
 
Inawezekana alilala late maana kwa Alvin hakuna jema πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚. Kuchelewa kulala na kazi nzito nzito kunachangia sana kupunguza uwezo wa kufikiri.
Ndio maana wanashauri pombe ilewe kwa walio na miaka 18 na kuendelea na wanataarifu usilewe na kuendesha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…