Gerald Hando: Ni rahisi kumhoji Katibu Mkuu wa CCM, Emanuel Nchimbi, kuliko Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika

Gerald Hando: Ni rahisi kumhoji Katibu Mkuu wa CCM, Emanuel Nchimbi, kuliko Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika

Nijuavyo kama hauko vizuri upstairs.
Huwezi mhoji Myika yule bwana ana akili sana point 7 form four. point 3 advance

Dr.Nchimbi ameunga unga pale mzumbe . Huyu anaweza hojiwa hata na zembwela
Mnyika aseme nani yupo vizuri upstairs akamfanyie mahajiano.

Sisi wapiga kura wake tunataka kumsikia kiongozi wetu mwenye IQ kubwa kushinda wote TZ
 
Nijuavyo kama hauko vizuri upstairs.
Huwezi mhoji Myika yule bwana ana akili sana point 7 form four. point 3 advance

Dr.Nchimbi ameunga unga pale mzumbe . Huyu anaweza hojiwa hata na zembwela
Mnyiko vizuri na namkubali lakini hapo kwenye advance 1.3 umetupiga kamba.......
 
Tatizo la Chadema wanaaamini wanaakili kushinda watanzania wote.

Wanawadharau mpaka wapiga kura wao.
Hasa hawa chadema wa humu JF wanadharau wananchi wenzao na kujiona wao ndio wenye akili sana, ila cha ajabu wanaenda kujazana kwenye mikutano ya chadema ni hao hao wananchi wanao wadharau na wao hubaki kusifia nyomi.
 
Hivi Gerald Hando bado anaendekeza ule ulevi mbwa wake hadi anazima bar?
 
Bro kwa mwanasiasa kumgomea vyombo vya habari anapata wapi political publicity? Hivi unajua John Mnyika anaweza kupita Kariakoo na watu wasimjue? Je, politically I sahihi?
Wasafi ni chawa wa Ccm ndio maana Chadema hawapendi kwenda huko.
 
Hasa hawa chadema wa humu JF wanadharau wananchi wenzao na kujiona wao ndio wenye akili sana, ila cha ajabu wanaenda kujazana kwenye mikutano ya chadema ni hao hao wananchi wanao wadharau na wao hubaki kusifia nyomi.
Ukiwaambia ukweli wanakuwa wakali na matusi, na hapo ndio hawajachukua madaraka,wakichukua nchi itakuwaje?
 
Sawa. Nitajie chombo Cha habari kisicho chawa kwa CCM.

Kuna jamaa anaitwa John Marwa na online TV yake sio chawa. Waandishi kama Jenerali Ulimwengu sio chawa. Lakini Wasafi ni chawa na Lissu aliwahi kukubali kuhojiwa nao wakaishia kufuta kipindi.
 
Na ndo hapo hadi leo sera za chama hazijulikani zaidi ya lawama
 
Kuna jamaa anaitwa John Marwa na online TV yake sio chawa. Waandishi kama Jenerali Ulimwengu sio chawa. Lakini Wasafi ni chawa na Lissu aliwahi kukubali kuhojiwa nao wakaishia kufuta kipindi.
Ahahahahaha! Jenerali Ulimwengu ana TV au Redio? Huyo mwingine hata sijui! Ahahahahaha!!
 
Huyo Gerald, dish limeyumba? Hana habari ule mdaharo ambao makatibu wakuu wa CHADEMA na ACT walitokea, lakini wa CCM akakimbia? Au unafiki unaua kumbukumbu yake huyo Gerald?
 
Kama wewe ni mhenga humu JF ungelijua msimamo wangu kuhusu Jenerali Ulimwengu. SIMKUBALI KABISA!!
Kwanini humkubali? Jenerali ana mapungufu yake kama binaadamu yeyote lakini kwa kiwango kikubwa anasema kweli kuhusu kinachoendelea ktk Tanganyika yetu. Pia kwa sasa hivi ukiacha tatizo la uchawa, tasnia ya habari imeharibika kabisa na kukosa weledi wa kutekeleza majukumu yao. Yaani hata kama wana habari wetu wangekuwa sio machawa, bado viwango vyao vya kitaaluma ni vya chini mno.
 
Ukiwaambia ukweli wanakuwa wakali na matusi, na hapo ndio hawajachukua madaraka,wakichukua nchi itakuwaje?
Mtu anaamini kwa kuwa chadema haipo madarakani basi makosa na mapungufu ya hiko chama ni halali tu kuwepo haina shida wala hakuna uhitaji wa kukosoa kisa tu chadema haipo madarakani. Kwanza huwezi kukuta wanakubali mapungufu ya viongozi wao, wao kutwa ni kuwasifia tu kuwa wana akili sana yani kwa sababu wapo chadema basi hiyo inawafanya wawe na akili sana ila wakihama tu chadema wanageuka wajinga hapo hapo.

Ni wakosoaji wasioamini kwenye kukosoana, wao wanaamini ccm tu ndio wa kukosolewa.
 
Back
Top Bottom