Pre GE2025 Gerald Hando: Uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ulikuwa na mizengwe mingi sana ndani ya CCM kwenyewe

Pre GE2025 Gerald Hando: Uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ulikuwa na mizengwe mingi sana ndani ya CCM kwenyewe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wanaopiga kura za maoni za maoni ni wajumbe, tulikuwa wagombea 176, walipata kura ni 55, kuna wagombea 125 wameambulia kura sifuri, hivyo kura yangu moja ina thamani sana!.
P
Sana aiseee.... Bila shaka aliyekupigia ni jamaa yako wakaribu sana.
 
Mkuu Cannabis , msema kweli mpenzi wa Mungu, ile kura moja mimi niliyopata, haikusababishwa na kupigwa zengwe, bali nilivuna nilichokipanda. Na nilikubali matokeo kwa roho safi Uchaguzi 2020 - Wana JF, nipeni Pole. Msinicheke wala msinibeze; nimegombea ubunge Kawe kupitia CCM nimeambulia kura 1. Ama kweli CCM ina wenyewe!
P
Hapana mkuu, kuna zengwe walipiga.... kwenye uchambuzi wa sheria na masuala ya kitaifa kwenye wale uliokuwa unashindana nao hakuna hata mmoja anayefikia nusu ya uwezo wako , kuna zengwe lilipigwa ndio maana hata kamati kuu bado ilikuja na jina lingine mfukoni...hata hivyo nasikia wana kawe wametelekezwa na mbunge wao
 
Wanaopiga kura za maoni za maoni ni wajumbe, tulikuwa wagombea 176, walipata kura ni 55, kuna wagombea 125 wameambulia kura sifuri, hivyo kura yangu moja ina thamani sana!.
P
kuna watu hawakuelewi, ccm kukuachia kura yako ni bahati kubwa, na walikuheshimu sana.

Huwa wana toa SIFURI mara nyingi, yani hata kura yako wanachukua.

Ulijitahidi sana au ndio ulitumia ule mkakati wa piga kura na usiondoke kituoni, linda kura yako?

Watu hawaelewi wajumbe 125 kupata SIFURI ina maana kubwa kiasi gani ndani ya CCM.

Unatakiwa upate SIFURI na UFURAHI, yani lose all, and be happy.

Ukikasirika, au hata kutilia shaka hilo, uteuzi hupati, na utaambiwa wewe siyo ccm.

Hongera sana kaka.
 
Yeye hakutaka kusema hivyo kwa ajili ya wapinzani lakini alikuwa akieelezea uhalisia uliokuwepo siku hizo maana hata hiyo kuangukia pua haimaanishi kwamba lazima wapinzani washinde ila ni tahadhari kwa hao waliopita kwa mbeleko kwamba uwezikano wao kurudi ni mdogo.
Ni mdogo sana,kawe,Siha, Arusha mjini,Masasi,Tanga mjini, Kilimanjaro yote, Mbeya,Dar nk!
 
Akiongea asubuhi kwenye uchambuzi wa gazeti la Raia Mwema bwana Hando amesema ndani ya CCM uchaguzi mkuu 2020 kulikuwa na mizengwe mingi sana katika kuwapitisha madiwani na wabunge jambo linalowafanya wabunge na madiwani wengi sana wa CCM kuangukia pua kwenye uchaguzi wa mwakani.
Wajimumbe wote wakatoswa.......Steve Nyerere alilia machozi.
 
Yeye hakutaka kusema hivyo kwa ajili ya wapinzani lakini alikuwa akieelezea uhalisia uliokuwepo siku hizo maana hata hiyo kuangukia pua haimaanishi kwamba lazima wapinzani washinde ila ni tahadhari kwa hao waliopita kwa mbeleko kwamba uwezikano wao kurudi ni mdogo.
Huto Tlalaatlaa hamna kitu. Achana naye...ukweli unamuuma
 
Wanafiki tu. Mbona hamkuthubutu kusema kipindi kile chuma kikiwepo.
 
Back
Top Bottom