Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Gerald Ibrahim maarufu kama SERIKALI ni mkulima na mfanyabiashara pia ni mkazi wa Kijiji cha Mpeta, Wilaya ya Uvinza, Mkoani Kigoma.
Mwaka 2018 yalitokea mapigano baina ya wananchi na Jeshi la polisi wakati kuwaondoa wananchi katika ardhi ya Kijiji cha Mwanduhubandu, Mpeta Magharibi kiasi cha Kutokea mauji na raia na polisi wawili.
Bunduki mbili aina ya SMG na bastola moja zilizokuwa zinatumiwa na Polisi katika Operesheni hiyo zikapotea katika vurugu hizo.
Hayati Magufuli aliagiza serikali ikae na wananchi wa Mpeta kwa karibu kumaliza mgogoro kwa amani bila kumwaga damu.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kigoma wakati huo alikuwa Samson Nyaikanga. Ndiye alimtafuta GERALD IBRAHIM kupitia katibu tarafa Bwana Thomasi Sangai wakati huo,
Thomasi Sangai kwa sasa yupo ofisi ya Mkuu wa Mkoa KIGOMA, ambaye ndiyo mwenye namba za simu 0767 985122.
Gerald Ibrahim aliitwa na kupewa maelekezo na watu wa usalama wa Taifa kazi ya kuwatuliza wenzie kwa amani bila vurugu wakati huo kutafuta bunduki mahala zilipo.
Makubaliano yalimtaka atumie gharama zake na kwamba baada ya kufanikisha atarudishiwa gharama zake na kupewa zawadi ya donge nono la kiasi cha shillingi millioni 15.
Gerald Ibrahim alianza kuifanya kazi huku akihofia changamoto za kutaka kuuwawa pale wananchi watakapogundua kama anashirikiana na serikali maana kwa wakati ule walikuwa na hasira nyingi,
Gerald alianza kufanya kazi hiyo 18/11/2018 na kazi yote alikamilisha na kutoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa Kigoma na vyombo vya linzi na Usalama kuwa kazi ameikamilisha kwa asilimia 100% kufikia April 2019.
Ambapo mgogoro wa Wananchi uliisha na bunduki mbili pamoja na bastola vilipatikana.
Baada ya kukamilisha alimuandikia Mkuu wa wilaya ya Uvinza Mheshimiwa Mwanamvua H.Mrindoko barua ili alipwe gharama zake na zawadi ambayo walimuahidi lakini hakupatiwa chochote.
Gerlad alimuandikia barua Mkuu wa Mkoa KIGOMA kukumbushia ahadi yao, hakufanikiwa, akamua kumuandikia barua IGP, pia hakufanikiwa.
Alimuandikia barua Waziri wa Mambo ya ndani, Wizara ya mambo ya ndani walimuita Gerald na kumuelekeza aende kwa RAS Kigoma wamlipe madai yake.
Gerlad aliporudi mkoani Kigoma hakulipwa chochote na RAS, ndipo akaamua kumwandikia barua Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa bahati mbaya hakujibiwa lolote.
Bahati nzuri Gerald alipata taarifa Hayati Magufuli atakuwa eneo la Laela, Sumbawanga Mkoani Rukwa
Alitoka Kigoma kwenda Rukwa kuona kutafuta msaada, kwa bahati nzuri alifanikiwa kukutana na wasaidizi wa Rais Magufuli.
Gerlad alipokuwa anatoa malalamiko yake, wasaidizi wa Magufuli walisema Rais Magufuli analikumbuka na kulijua suala lake, wakasema Mh. Rais ameshalipa madai haya unayodai kwa kazi nzuri aliyoifanya.
Wasaidizi wa Rais waliwasiliana na Mkuu wa mkoa Kigoma na Gerlad
akaamuliwa arudi nyumbani Kigoma na jambo hilo tayari kwa Mkuu wa Mkoa amelishughulikia tayari.
Gerald alipigiwa simu akiwa Kigoma,akaelekezwa afike ofisi ya Mkuu wa Mkoa, alipofika alikuta kamati ya ulinzi na Usalama yote ikiwa imeketi.
Kitu cha ajabu alipofika alikaguliwa kama ana vinasa sauti na simu yake ya mkononi wakamnyang’anya.
Viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama walimueleza wampe shillingi milioni mbili, ila pia siyo kwa kusaini mahala popote bali akachukue fedha hizo sheli (petrol station) kwa Bella,
Gerlad alizikataa fedha hizo na kikao kiliisha bila muafaka wowote, mara ya pili akaitwa tena kwenye kikao cha Ulinzi na Usalama Mkoani, ikaonekana wameamua wamlipe milioni sita, pia Gerald hakukubali na kikao kilimalizika bila muafaka,
Mara ya tatu walipo muita tena kwenye kikao cha kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoani
Siku hiyo Kamati ilihitimisha kwa kusema pesa zilitoka na wameshamlipa Gerald, pia taasisi zingine zilimpa zawadi baada ya kazi hiyo kama vile ofisi ya Mkuu wa mkoa, Wizara ya Ardhi pamoja na TFS
Wakamalizia kwa kusema Kwamba wanayo taarifa kuwa baada ya kupewa pesa hizo ailienda kufanya starehe Dar es Salaam ikiwemo na kununua gari,
Kwa hiyo amerudi tena kudai madai yasiyokuwa ya halali wakati madai yake yote yameshalipwa. Gerald aliamua kumuandikia barua Mh.Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mara ya Pili
Baada ya muda mfupi ofisi ya Waziri Mkuu walimtafuta Mkuu wa Mkoa wa wakati huo Tobiasi Andengenye ambaye alikiri kumtambua na akaomba yeye na Gerald, waonane Kigoma alipwe madai yake.
Gerald alipofika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mkuu wa Mkoa akamuambia ni kweli nina maelekezo yako kutoka kwa waziri Mkuu
Kweli ulifanya kazi nzuri hatukatai ila Waziri Mkuu hajaelekeza ni mfuko gani ukupe hizo fedha hapa mkoani.
Wakamuuliza kama aliakuwa na namba ya Waziri Mkuu wachukue mawasiliano yake ili wapige wapate maelekezo.
Gerlad aligundua maneno yale ni mtego wa wao kutaka Kujua kama alikuwa anafanya mawasiliano na Waziri Mkuu
1. Alipokwenda Waziri Mkuu Kigoma kwa ziara ya chama alipouliza mwananchi mwenye kero, Gerlad alipoinua mkono
ulishushushwa chini akaambiwa atulie atalipwa na vitisho Juu kama angekaidi kuendelea kunyoosha mkono Juu.
2. Waziri Mkuu alipokuwa na kikao cha NSSF, Gerlad aliifika alizuiliwa kuingia na kumuweka kwenye gari aina ya Landcruiser kisha wakafunga milango huku gari ikiwa ‘silencer’ na AC imewashwa.
Gari alilofungiwa Gerlad lilitangulia uwanja wa ndege Kigoma na Gerald akiwemo ndani ya gari hilo kafungwa kwa nyuma.
Waziri Mkuu alipofika uwanja wa Ndege, walimtoa Gerald wakamficha kwenye chumba mojawapo pale airport na kuwekewa bastola kichwani kuwa akipiga kelele anauwawa.
Baada ya Waziri Mkuu kuondoka
walimtelekeza pale pale uwanjani mpaka alipoamua kutoka kwa miguu uwanja wa ndege.
3. Siku moja Hayati Magufuli alifika Mpeta alisimama na kusalimia. GERALD alipofika kwenye mkutano alichukuliwa na askari polisi wawili ambao walisema wamepata taarifa kuwa ameunda kikosi cha kutaka kumuuwa Rais.
Gerlad ailivutwa pembeni akapigwa sana kabla kuja kusaidiwa na bodigadi wa Raisi ambaye alikuja kuzuia wasiendelee kumpiga
Gerald akiwa mwezi mzima amelala nyumbani kwake akifanyiwa
matibabu, alipopata nafuu aliamua kuanza upya kwenda kwa Waziri wa
mambo ya ndani ambapo Waziri wa Mambo ya ndani aliunda tume kupitia ofisi ya IGP.
Tume aliyounda ikafika Kigoma na kufuatilia matukio ya Gerald yote, mwisho wakamuelekeza RCO ampe majibu ya malalamiko yake na ayachukulie hatua haraka sana
RCO na yeye alikuwa hampi majibu ya kutosheleza badala yake alikuwa anamtengenezea kesi, haya yote yanatokana na madai na maelekezo waliyokuwa wanampatia
Tume mbalimbali za Rais Magufuli zilifika kumuhoji ili aseme uongo kwa kuwasingizia wananchi kuwa mapigano yale walileta wanajeshi wa nje ya nchi.
Gerlad hakusema uongo, hakupenda kusema uongo maana alijua anaweza kuliangusha Taifa lake na taarifa zote walizokuwa wanapata huko lkulu kuhusu mgogoro wa Mpeta,Wanduhubandu zilikuwa zinapitia kwake au kutoka kwake.
Kwa malalamiko haya ni dhahiri pesa ilitoka lakini Gerlad kama mlengwa wa pesa hizo
hakupata hivyo kwa busara zake aliomba msaada kwa kila kiongozi mwenye dhamana ili aweze kupata haki yake.
(1) Barua kwenda ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Uvinza ya tarehe (2) Barua kwenda kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma ya tarehe 12 October 2019 (3) Barua kwenda kwa Mkuu wa jeshi la Polisi Tz (4) barua kwenda kwa ispekta generali wa polisi ya tarehe 26 September 2019 (5) barua kwenda Waziri wa Mambo ya ndani ya tarehe 10 November 2024 (6) barua kwenda Waziri Mkuu ya tarehe 22 March 2024.
Tarehe 8 July 2024 Gerald alifika ofisi ya IGP Dar es salaam na kuelezwa kuwa anatakiwa afike ofisi ya IGP alikua huko ofisi ya Dodoma, Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.
Tarehe 9 July 2024 Gerald alipofika Dodoma na alikukutana na danadana za nenda rudi nyingi na
mwisho hakuonana na IGP.
Gerald aliamua kutafuta mawakili ili kufungua jalada la madai ya stahiki zake na hatua za awali zimekwisha kuanza kufanyika chini ya mawakili,
Gerlad Ibrahim aliamua kurudi Kigoma ili kujipanga vizuri kwa ajili ya kesi aliyoanza kuiandaa, lakini cha kusikitisha tarehe 4 August 2024 siku ya Jumapili saa tano asubuhi
Alivamiwa na watu wakiwa na gari aina ya Landcluiser na kumteka huku wakimtelekeza mtoto wa umri wa miaka 5 aliyekuwa amebewa na Baba yake, jina la mtoto ni John Gerald Ibrahim
OCD wa wilaya ya Uvinza aligoma kutoa RB tangu tarehe 04 August 2024 kwa ndugu wa Gerald Ibrahim kuhusu kutekwa na kupotea kwa Gerald Ibrahim
Mpaka ndugu walipoomba msaada polisi makao makuu ndiyo OCD Uvinza ndiyo akaridhia kutoa RB siku ya tarehe 07 August 2024 RB yenye namba UVZ.CID.PE.12.2024
Leo ni siku 20 sasa zimepita tangu Gerald Ibrahim a.k.a Serikali atekwe na Kupotea juu ya uso wa Dunia.
Bwana Gerald Ibrahim namba zake za simu zilikuwa ni 0762524459 au 0623515065 au 0687117991.
Mpaka sasa vituo vyote vya polisi havina taarifa ya ndugu Gerlad Ibrahim wala vyumba vya kuhifadhia maiti hakuna Jina la Gerald Ibrahim.
Namba za mke wa Gerald Ibrahim ni 0695152220.
Nawaza kama siyo Gerald Ibrahim kusukumwa na mapenzi yake kwa nchi yake
Na kuamua kupambana kutafuta silaha zile huenda muda huu zingekuwa mtaani mikononi mwa watu wabaya zinatumika kuondoa uhai wa ndugu zetu au rafiki zetu.
Kama Gerald Ibrahim a.k.a Serikali asingefanya wema kwa Jeshi la polisi na kuingia katika mgogoro wa kudai ahadi ya lile donge nono huenda angekuwa uraiani kama sisi leo hii.
Boniface Jacob
Ex-Mayor
The voice of the silenced Majority.
0712 239595.