Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Shukrani sana ndugu yangu [emoji120]Unyama ni mwingi, sijaona mwandishi bora kushinda wewe mkuu
Karibu sana bosi wangu tuendelee kuigusa hii kalamu[emoji1666]Good,nasoma mpaka nahisi nacheki move za Scott Ad
RicardoSTORY: GEREZA LA HAZWA
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORY TELLER: Bux the story teller
AGE: 18+
UKURASA WA SABINI NA SITA
TULIPO ISHIA UKURASA WA SABINI NA TANO
Ni muda kidogo hakuweza kusimama kama baba kwenye familia hivyo alikuwa akiitamani sana hiyo nafasi rasmi aliamini hiyo kiu yake inaenda kuisha. Rasmi Zakaria alikuwa anarudi Tanzania na ubaya alikuwa akijua kwamba familia yake ilikuwa ipo tena huenda ipo salama kuliko hata yeye anavyo fikiria na kwa wakati huo familia yake haikuwepo wote walikuwa wamekufa kwa kuuawa kikatili sana tena mkewe alibakwa kabla hajauawa.
ENDELEA...............
Jina la Sky the Magic lilikuwa kwenye skirini kubwa za wanaume wa usalama wa taifa walihitaji kumjua mtu ambaye ilisemekana kwamba alikuwa na taarifa nyingi sana za siri za mtu ambaye alidaiwa kutafutwa na watu wengi sana, zoezi zima lilikuwa likisimamiwa na mkurugenzi mwenyewe wa usalama wa taifa hata raisi alikuwa yupo kando ya hilo eneo akihitaji ashuhudie kile alichokuwa ameambiwa kama je kilikuwa ni kitu cha kweli au alikuwa amedanganywa na Qader.
“Bosi huyu mtu anaonekana kwa sasa yupo ndani ya nchi ya Malaysia”
“Whaaaaat?”
“Ndivyo inavyo onyesha hapa”
“Huku anaonekana yupo MUMBAI” zilikuwa ni sauti za vijana wa IT ndani ya idara hiyo nyeti kabisa ya serikali walikuwa wamekaa zaidi ya masaa manne wakiwa wanamtafuta huyo mtu ambaye alikuwa na taarifa za siri sana.
“Mhhhhhh ni nani huyu mtu ambaye ameingia ndani ya nchi yangu ana uwezo mkubwa namna hii namhitaji kwa gharama zozote zile” mheshimiwa raisi alitoa hiyo amri kwa gharama yoyote ile alikuwa akimhitaji huyo bwana mdogo ambaye alikuwa akijiita jina la SKY THE MAGIC kwenye dunia nyeusi ambako wanaishi watu wasio julikana.
“Hapa nadhani inabidi mpaka atafutwe George” aliongea kijana mmoja kati yao huku akiwa anaendelea kubonyeza tarakishi kadhaa kwenye komputa yake.
“Who is George?” aliuliza mheshimiwa raisi akiwa anamgeukia mkurugenzi wa usalama wa taifa ambaye jina lake alikuwa anajulikana kama Jirio Mtashi.
“Ni kijana wangu wa kazi ambaye nimemsimamisha kazi kwa muda”
“Kwa sababu zipi?”
“Alifumwa na mwanamke akiwa anafanya mapenzi kwenye eneo ambalo alipaswa kupeleka taarifa hivyo alipelekea taarifa kuchelewa”
“Mhhhhhhhh mna uhakika anaiweza hii kazi?” aliuliza raisi kwa msisitizo sana
“Ni kijana mwenye uwezo mkubwa sana kwenye mambo ya mitandao mafunzo yake alimalizia huko marekani ndani ya shirika la CIA sidhani kama kuna kitu kinaweza kumshinda kwa lolote lile”
“Mpigieni simu aje haraka sana hapa namhitaji hili jambo sitaki lilale nataka liishe ndani ya muda mfupi sana ujao”
“Sawa mkuu ngoja nimfuate” mkurugenzi wa usalama wa taifa alitoka mwenyewe ndani ya chumba hicho kubwa kilichokuwa kimejaa mitambo mbalimbali ya mitandao alihitaji kumfuata kijana huyo yeye mwenyewe kwa sababu mheshimiwa raisi alikuwa anamsubiria hapo hapo ndani.
George alikuwa ni kijana mwenye umri wa miaka 30, utundu wake wa kucheza na mitandao akiwa jeshini ulimfanya kupata nafasi pekee ya kuchukuliwa na wavaa suti ambao walimpeleka Marekani Kwenda kusomea utaalamu wake huo, baada ya kumaliza masomo yake alibahatika kuwa mmoja kat ya vijana waliodhaminiwa na CIA kupitia mkurugenzi wake wa usalama wa taifa, huko alienda kufundishwa vitu vingi sana kuhusu mitandao, hakuna hata nukta ya mtandao ambayo ingempita asiielewe kwenye kichwa chake ila bahati mbaya kwake alikuwa na tatizo moja tu pekee, alikuwa anapenda sana wanawake hao ndiyo ilikuwa furaha yake kuna muda alikuwa anasahau mpaka kazi kwa sababu ya wanawake.
Kuna siku moja alitumwa na mkubwa wake kupeleka taarifa ndani ya airport huko nchini Kenya kuna mtu ambaye alitakiwa azuiliwe hapo airport asisafiri kwa sababu alihusishwa na usambazaji wa madawa ya kulevya na alifanikiwa kutoroka ndani ya jiji la Dar es salaam, baada ya kufika hapo alikutana na mrembo mmoja ambaye alikuwa ni mfanyakazi ndani ya airport hiyo, kwa kutumia ushawishi wake mkubwa na mwonekano bomba aliokuwa nao alijikuta akifanya mapenzi ndani ya vyoo vya airport na mwanamke huyo mpaka pale wale wenzake waliokuwa wanamfuatilia kwa nyuma wakitegemea kumkamata mtuhumiwa huyo walipo mkuta yupo na mwanamke. Walishangazwa sana na hilo tukio yaani mwenzao kasusa kazi kisa mwanamke, taarifa ilifika kwa mkurugenzi wa usalama wa taifa ndipo alipo amua kumsimamisha kijana huyo kazi na adhabu kali ambayo ilimfanya kutumikia kifungo cha mwezi mmoja kwenye selo zao kisha akarudishwa mtaani mpaka pale ambapo maamuzi mengine yangefanyika.
Mabibo loyola nyumba namba 700 ndilo eneo ambalo alikuwa anaishi kijana huyo, hakuna mtu wa mtaani ambaye alikuwa anajua kwamba kijana huyo alikuwa ni usalama wa taifa walikuwa wakimwona akitoka na kurudi tu, maisha yake ya mtaani yalikuwa ya kawaida tu ambapo alipanga chumba kimoja tu pekee. Nusu saa tu ilitumika kumfikisha mkurugenzi hilo eneo akiwa kwenye gari yake ya V8 nyeusi, alishuka na kuusogelea huo mlango, kwa ndani alisikia makelele mengi sana hakujiuliza mara mbili kwamba kijana huyo alikuwa na mwanamke ndani. Alikuwa na funguo za ziada za chumba hicho alikifungua na kuingia ndani, wote waliokuwa humo ndani walipigwa na butwaa, alikuwa George na wanawake wawili ambao kwa pembeni walikuwa na vitambulisho wa chuo cha NIT.
Mzee huyo alisikitika tu kisha akamrushia kijana huyo suruali ambayo ilikuwa imewekwa ukutani
“Nakuhitaji ndani ya dakika mbili zijazo”
“Sawa mkuu” aliitikia huku anatetemeka wakati huo bosi wake alikuwa anatoka nje, aliinuka na kuvaa haraka mno
“G unatuachaje kwenye hali kama hii” dada mmoja alitamka kwa msisimko alichukia sana kukatishwa kwenye sehemu ambayo alijihisi alikuwa anaifaidi dunia lakini mwanaume hakusema chochote kile mpaka alipo maliza kuvaa.
“Naweza kurudi au nisirudi ila tokeni hapa sasa hivi ni hatari sana funguo yangu mtaniwekea chini ya mlango mkishakula nikirudi nitawatafuta” aliongea huku akiwa anaifunga suruali yake, kwa nje aliiona V8 ambayo hakujiuliza mara mbili alijitosa ndani na kuushikilia usukani. Huku nyuma aliacha taharuki watu ambao walikuwa karibu na maeneo anayo yaishi walibaki wanajiuliza sana kivipi kijana kama huyo afuatwe na gari ya gharama namna hiyo tena yeye akionekana kuingia upande wa dereva kabisa hata wale waanawake ambao aliwaacha ndani kwake hawakuamini walichokuwa wanakiona wakati huo walikuwa wakichungulia dirishani, mwanaume alilitoa gari kwa kasi sana ndani ya hilo eneo na kutokomea njia ya Kariakoo.
“Mhhhhhhhh hii tabia unapendezwa nayo sana?” mkubwa wake alimuuliza akiwa yupo busy na usukani jasho lilikuwa linamtoka kwa hofu sana.
“Hapana bosi”
“Sasa kwanini unajidhalilisha sana namna hiyo?”
“Huwa nashindwa kujizuia”
“Unashindwa kujizuia au unajiendekeza?” hakuwa na jibu la kumpa mkubwa wake alijifanya kama vile hajasikia.
“Wakati nina umri kama wako hata mimi nilihisi hii dunia ninaiweza sana, nilikuwa nahisi kwamba kila kitu kipo ndani ya uwezo wangu, nilifanya sana starehe kwa wakati ule, sikuwa nikishaurika lakini hakuna kitu kibaya kama kuupoteza muda kwa kuufurahisha ulimwengu, kwa umri wako hapo sasa unatakiwa kuwaza mambo ya msingi sana kuliko kupoteza pesa zako kwa wanawake. kwa kazi uliyo nayo wewe hata ukioa sio mbaya sana nilitegemea kwa sasa utakuwa umebadilika sana na huenda unajiandaa kuwa baba lakini ndiyo kwanza unaonekana kama nimekupa uhuru, huu muda ambao leo unaupoteza kiwepesi sana hivyo ipo siku utaujutia sana na hautakuwa na nafasi nyingine ya kuufidia. Hakuna atakaye kuja kukukumbusha kipi sahihi kwako ambacho unatakiwa ukifanye kila mtu yuko busy na mambo yake, unalipwa pesa nyingi mno lakini hata leo nikikuuliza umefanya nini cha maana sidhani kama utanitajia hata kimoja.
Kuwa kwenye hizi kazi zetu hazikuwekei mipaka ya wewe kushindwa kujiwekeza inatokeaga siku unaweza ukawa nje ya idara unahisi kwa baadae utaishije, wanao utawarithisha nini? jitafakari sana, leo nimeongea nawewe kama mwanangu kwa sababu nina watoto ambao wapo kama wewe nyumbani kwahiyo kuna muda hainiumi au kuniudhi kwa sababu tu mimi ni bosi wako ila kuna muda nikikuona nakuona kama mwanangu” alimaliza maelezo yake ambayo yalimgusa sana George wakati huo alikuwa anafungua mlango walikuwa wameshafika makao makuu tayari.
Hatua za kuelekea ndani ndizo zilizo zidisha uoga kwenye sura ya George baada ya kumuona raisi akiwa amekaa kwenye kiti aliogopa sana hakuwahi hata siku moja kukutana na raisi alijikuta anababaika sana.
“Shikamoo mheshimiwa” alisahau hata kutoa saluti alijikuta akitoa salamu ambayo ilimfanya kila mtu mle ndani acheke kimya kimya bila kujionyesha ingekuwa ni dharau kubwa sana mbele ya mheshimiwa, raisi alitabasamu tu.
“Wewe ndiye George?”
“Ndiyo mheshimiwa”
“Nahitaji huyu mtu anaye jiita THE SKY MAGIC akamatwe kwa haraka sana” George alikuwa ameelewa kitu ambacho aliitiwa hapo alisogea kwenye komputa yake ambayo ilikuwa kubwa kuliko za wenzake na ilikuwa na uwezo mkubwa sana aliotabasamu kwani aliimisi kwa siku nyingi sana alikuwa hajaigusa alijihisi yupo uwanja wa nyumbani,
“Naweza kupata maelekezo ya huyo mtu?”
“Inadaiwa kwamba unaenda kwenye email sehemu ya kuandika unaandika unacho kihitaji kisha kwenye kutuma Kwenda kwa…. Unaigeuza namba yako ya simu mtu huyo ujumbe unamfikia”
“Mhhhhhhhh”
“Kuna nini”
“Sikujua kama kwenye nchi hii kuna mtu mwingine ambaye ana huu uwezo”
“Kwanini”
“Niliwahi kufundishwa kule Marekani watu wa namna hii hata kuwapata huwa ni ngumu sana wanapo yatenda matukio yao hivyo kama asipo tumika mtu mwenye uwezo zaidi yake ni ngumu sana kumkamata”
“Wewe unaweza kumpata?”
“Nipeni dakika tano” kila mtu alibaki kimya kazi walimuachia kijana ambaye walitegemea atawapa majibu ya kueleweka. Zilipita dakika tano akiwa anabonyeza tarakishi kwenye hiyo komputa yake kwa haraka sana kisha akachukua kikaratasi na kalamu ya wino akanakili namba fulani za kirumi ambazo zilikuwa zimechanganywa sana, futa kila kitu na kuziweka namba hizo za kirumi alibonyeza kwa sekunde zingine thelathini tu, alitulia na kuinama chini
“Umefanikiwa?”
“Ndiyo mkuu”
“Sasa mbona umekuwa kinyonge hivyo?” hakuongea kitu akabonyeza tarakishi moja tu kwenye kumputa yake zilikuja codes tano kwenye skrini ambazo zilimshtua hata mkurugenzi.
“Noooo haiwezekani?” mkurugenzi wa usalama wa taifa hakuamini kitu ambacho alikuwa anakiona mbele yake ilimpelekea mpaka akakaa kwenye kitu midomo yake ikiwa mizito sana, mheshimiwa raisi alimgeukia na kumuuliza kwa sauti ya mtu aliyekuwa anahitaji sana kuyapata majibu.
“Who is it?” mkurugenzi wa usalama wa taifa aliinua uso wake kumjibu mheshimiwa.
Unahisi ni nani huyo mtu anaye jiita SKY THE MAGIC kiasi cha kumshtua George na mkurugenzi wa usalama wa taifa?..76 inaishia hapa tukutane tena wakati ujao.
Wasalaam
Bux the storyteller.
Mkuu nilikuwa mihangaikoni ndo nagusa cm sio muda inakujaFEBIANI BABUYA mkuu weka huo uzii
Wazee wa keyboard [emoji119]Ricardo
Shukrani sana bosiHi ngoma kali sana, mwamba unaandika na story imeandikika,
Nimekua nikiisoma toka mwanzo ni kati ya story tamu sana sana, kwani haiishi hamu kuisoma. Hongera sana kamanda
Ahsante sanaaaaaaaaa
Mwamba Fanya mchakato boss. [emoji41]STORY: GEREZA LA HAZWA
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORY TELLER: Bux the story teller
AGE: 18+
UKURASA WA THEMANINI NA TATU
TULIPO ISHIA UKURASA WA THEMANINI NA MBILI
“Unajua shida yenu ni moja mnaweza mkawa mnamjua mhusika na bado mnadai mnaendelea na uchunguzi kitu ambacho ni upotezaji wa muda na mkubwa anahitaji hili jambo lifanyike haraka sana hivyo hilo jambo kuanzia sasa kaa pembeni tuachie sisi tunaanzia ambapo mmeishia” mkuu wa polisi ilimuuma sana lakini hakuwa na namna kupingana na kauli ya raisi ilibidi akubali japo kishingo upande kuipoteza kesi ya mauaji ya Karimu. Mkuu wa majeshi alitoka nje na kuitoa simu yake ambayo alipiga mahali ilivyo pokelewa aliongea kauli moja tu.
“Tukutane kambini ndani ya saa moja lijalo” kisha akapanda kwenye gari na msafara wake ukatoweka muda huo huo.
ENDELEA...............
Chumba kikubwa chenye thamani za gharama sana kilikuwa kimepambwa na sauti za watu wawili ambapo mmoja wao alionekana kuwa kwenye maumivu tofauti kabisa na mwenzake ambaye alikuwa akiongea kwa kujiamini sana, Aami Amadou Mbaye pamoja na Qader ndio ambao walikuwa humo ndani baada ya Aami kuweza kumtorosha kwenye ile nyumba sehemu ambayo alikuwa chini ya ulinzi wa usalama wa taifa, Qader bado alikuwa kwenye maumivu makali sana kwa namna alivyoweza kuteswa kule ambako alikuwepo wakati anahojiwa na mheshimiwa raisi.
“Kwahiyo utaniua?” Qader aliweza kumuuliza kijana huyo mbele yake maana alikuwa amemuahidi hivyo kwamba kama angetaja siri zake basi kamwe asingeweza kumuacha hai, Aami alikuwa amekaa kwenye sofa la upande wa pili upanga na bastola mbili vikiwa kwenye meza moja ya kioo ambayo ilikuwa katikati yao.
“Ningetaka kukuua basi nisinge hangaika kukuleta hapa kwa mara ya kwanza macho yako yakiwa hayajafungwa, ulitakiwa kufa kwenye mkono wangu ila nimeona haina haja ya kukuua kwa sasa bado hauna uwezo wa kunikimbia”
“Kwanini unasema hivyo?”
“Kwa sababu hautaweza kunikimbia wala kuikimbia familia yako na nahitaji kwa sasa uilete hapa Tanzania”
“Hey whaaaaat?”
“Unatakiwa uilete familia yako uwe nayo karibu eneo ambalo unaweza ukailinda hata kama hautakuwa na huo uwezo”
“Niilinde juu ya nani wakati kule waliko ndiko kuna usalama wa kutosha unataka niilete kwenye hatari kubwa kama hii wakati hata mimi mwenyewe sina hata uhakika juu ya usalama wangu mwenyewe?”
“Kipi kilichokuleta kwenye nchi hii?”
“Zakaria”
“Umempata?”
“Hapana”
“Una muda gani tangu uwasiliane na bosi wako ambaye amekutuma uje huku?”
“Mhhhhh hata sikumbuki”
“Unahisi kwa sasa atakuwa anakuwazia kitu gani?”
“Yule mzee ni mtu katili mno kama nilivyo mimi mwenyewe sidhani kama anaweza kuniacha hai kwa sababu imepita muda mrefu sana bila mimi kumtafuta”
“Huyo ndiye atakaye iua familia yako mapema kama ikiendelea kukaa huko Afrika ya kusini ambako ndiko uliko ificha”
“Yule sijawahi kumwambia kitu chochote kuhusu familia yangu wala hajui kama mimi nina familia kabisa hivyo hawezi kufanya hicho kitu”
“Hahahhahh hahahahaha hahahahahah” Aami alicheka sana kiasi cha kumshangaza sana Qader
“Sasa hapa kinacho kuchekesha nini?”
“Umefanya kazi kwa muda gani za aina hii?”
“Kwa muda mrefu sana”
“Usiniaminishe wewe ni moja ya watu wajinga sana kiasi hicho”
“Kivipi?”
“Kuna ile siku niliwahi kukwambia kwenye huu ulimwengu wa kutisha watu hawana roho kama walizo nazo wanadamu wengine ndiyo maana kwao kuua ni kama kumsukumia mlevi kwenye mtaro tu, hakuna mtu hatari kama yule anaweza kukupatia kazi bila kukujua wewe kiundani na kila unacho kifanya kwenye maisha yako, nina uhakika bosi wako ambaye ni kaka yangu anakujua wewe kuliko hata wewe unavyo mjua yeye ndiyo maana amekupaga uhuru wa kufanya kitu chochote na ujisimamie mwenyewe kwa sababu anajua kabisa kwamba huwezi kumkimbia, sasa kama anajua huwezi kumkimbia unahisi ni kitu gani ambacho kinampa uhakika wa kutokuwa na wasiwasi juu yako? Udhaifu wako ni nini? wanadamu wengi huwa wanakurupuka sana kufikiria hasa pale wanapokuwa wanawekewa pesa mbele yao huwa wanasahau kila kitu mpaka maisha yao, kwenye maisha yako kosa kila kitu ila usikose akili utakuwa na maisha mafupi sana au utaishia kuwa mtumwa wa watu fulani ambao watakutumia wewe pamoja na ujinga wako kuyatimiza yale ambayo wanayataka wao nawewe utakuwa unajifanya kwamba wewe ndiye mjanja ila wakisha malizana nawewe baadae wanakuua kabisa” maneno ya Aami yalionekana kumuingia sana Qader kwenye akili yake mtu huyo aliwaza mbali sana kuliko hata yeye alivyokuwa anafikria alijua bosi wake hajui mambo mengi kuliko yeye lakini haikuwa kweli ni kwamba alikuwa anatumiwa kiakili bila yeye kujigundua kabisa.
“Wewe haya yote umeyajuaje?” Qader alimuuliza kijana huyo ambaye kwa umri alikuwa mdogo kwake sana tu lakini kwa upande wa ukomavu na mambo ya kidunia pamoja na akili kijana huyo akionekana kumuacha mbali sana
“Unahisi kwanini leo nimekuja kukuchukua pale nikiwa na sura yangu ya uhalisia kabisa na wakati najua kabisa kwamba eneo kama lile lina ulinzi wa kutosha wa kamera?”
“Kwakweli sijaelewa kwanza nimeshangaa umejuaje nipo pale lakini hata namna ulivyokuwa unafanya mauaji kwa wale watu imefikia hatua nimekuogopa sana sidhani kama nawewe ulizaliwa na wanadamu wa kawaida kama sisi, ndiyo maana baada ya wewe kunitoa pale moja kwa moja nilijua tu kwamba unakuja ni kuniua nimeogopa sana mpaka saivi moyo wangu unanienda kwa kasi mno” maneno ya Qader yalimfanya Aami atabasamu sana mtu huyo alikuwa anamuogopa na ndio ulikuwa uhalisia wake kilikuwa kiumbe cha ajabu mno pale anapo amua kulificha tabasamu lake hilo na kuuonyesha vizuri upande wake wa pili.
“Kuhusu mimi kukupata vipi pale ni ishu ndogo sana ambayo siwezi hata kukujibi ila leo nilifanya vile kwa sababu kuu mbili, ya kwanza nilitaka unione uhalisia wangu upoje napokuwa kwenye ngozi yangu halisi ya kikatili mno ambayo huwa siwi na akili za kibinadamu kama ambazo tunazitumia kuongea hapa muda huu nadhani hilo umelithibitisha wanaume wa kazi kama wale nimewaua wote kwa dakika tano tu na nikafanikiwa kuondoka nawewe lakini sababu ya mhimu zaidi nilitaka hawa watu wanione moja kwa moja sitaki tena kufichana nao chochote nataka nipambane nao wakiwa wananijua sasa naenda kuwaonyesha uhalisia wangu”
“Mhhhhhhh huwa ni ngumu sana kupambana na serikali pale wanapo amua kumfuatilia mtu moja kwa moja kwa sababu serikali huwa zina watu wa hatari sana huenda wengine ambao ni wabaya kuliko hata wewe huwezi kushindana na jeshi la nchi” Qader hakuwa na uhakika na alichokuwa anakiogea lakini alihisi yupo sahihi kupambana na nchi nzima ilikuwa ni kazi ngumu sana.
“Hahahaahahah ndiyo maana sijakuua nimekuacha hai”
“Heeeeee kwanini?”
“Kwa sababu nataka ushuhudie kwa macho yako kitu ambacho kinaenda kutokea kwenye nchi hii”
“Hii ndiyo sababu kubwa iliyo kufanya wewe ukaniacha mimi hai?” Qader hali ilikuwa inaendelea kumuelemea alianza kujihisi joto kali sana licha ya ndani ya chumba hicho kikubwa kuwa na kiyoyozi cha kutosha ambacho kilileta hali ya hewa nzuri sana ila bado moyo wake ulikuwa ni wa moto sana.
“Siku kadhaa nyuma walikuja watu kwenye nchi hii wapo watatu tu, hao watu wanafanya matukio yao hadharani bila uoga na wanaacha mpaka ushahidi wa wao kuhusika moja kwa moja na hayo matukio ndiyo maana niliamua kuja kukuchukua haraka kwa sababu kama wangekupata watu hawa huenda siri zangu ungewapa na hicho ndicho ambacho nisinge ruhusu kabisa kiweze kutokea”
“Watu gani tena hao mbona unanichanganya?”
“Watu wa bosi wako”
“Noooo nooooo haiwezekani bosi asingeweza kutuma watu wengine bila kunipa mimi taarifa kama kulikuwa na ulazima wa kuwaleta watu hao au la namimi ndiye mtu ambaye ananitegemea sana na kuniamini kuliko mtu wake yeyote yule” Qader aliongea kwa kujiamini na alijiona yupo sahihi kabisa kwa maelezo yake.
“Kuwa makini sana na huo mdomo wako hususani kwenye mambo ambayo hata huyajui yaani mtu kama yule ndiye akutegemee kijana dhaifu sana kama wewe? mtu ambaye huwezi hata kujilinda wewe mwenyewe na unasema kwamba eti anakutegemea? Wewe ni kibaraka wa chini sana kwake ana watu wengi sana ambao wana uwezo hata mara kumi yako nadhani hata yeye bado haumjui vizuri kwa namna alivyo huwa unamuona kama mtoto wa mama sana yule siku ukija kumjua utajuta maisha yako yote” mwanaume aliendelea kutoa jasho baada ya kuendelea kuambiwa mambo ambayo yalizidi kumtisha.
“Sasa wewe uliwajuaje kama ni watu wa bosi?”
“Hao watu nasikia walitekeleza tukio la kumuua dereva tax mmoja ndani ya Arusha na tukio lao halikuwa na kificho chochote kiasi kwamba taarifa zikawa zimefika kwenye vyombo vya usalama ambapo kwa bahati mbaya sana taarifa zilivuja mpaka ndani ya jeshi la polisi ambapo kesi ya kuwatafuta hao watu alibambikiziwa bwana mdogo mmoja ambaye inadaiwa aliahidiwa kurudishiwa cheo chake ambacho alikuwa amekipoteza, bwana mdogo huyo aliwatafuta watu hao mpaka kuwapata sehemu ambayo walikuwa wamefikia hotelini, alijiamini sana bila kuwajua watu ambao alikuwa anawatafuta, alienda mpaka huko hotelini kwa lengo la kuwakamata walimuua kikatili sana na kuondoka eneo hilo” Aami alielezea kwa usahihi sana.
“Sasa hiyo inahusiana vipi nawewe kuweza kuwajua kwamba ni watu wa bosi?”
“Siku ile baada ya kusikia yale mauaji mimi nilienda mpaka kwenye lile eneo nikijumuika na polisi ambao walikuwa wamefika pale, yule kijana baada ya kuuliwa kuna kadi ilikuwa imechomwekwa kwenye shingo yake, kwenye mwili wake waliikuta picha ya watu hao ambao walikuwa wamemfanyia hilo tukio baada ya kuwaona watu hao sikuwajua ila kilichokuja kunifanya niwajue ni baada ya kuiona ile kadi ambayo walikuwa wameichomeka kwenye shingo ya yule bwana mdogo. Zile kadi anazitumia kaka yangu tu dunia nzima na zipo chache sana huwa ni alama yake popote ale anapokuwepo ukiiona hiyo kadi basi ujue yeye au watu wake wa karibu hawapo mbali ndiyo maana nilikuwa na uhakika kwamba wale walikuwa ni watu wa brother ambaye ni bosi wako” Qader alihema kwa uoga na kuuliza.
“Kwanini usingewatafuta mapema?”
“Mhhhhh siku ile pale nilitamani sana kuupata mwili wa yule bwana mdogo nilitoweka lile eneo baada ya kuona kuna watu ambao nilikuw a na uhakika kwamba ni usalama wa taifa walikuwa wamefika pale hivyo sikufanikiwa, sikuwa na haraka nao sana nilitaka kwanza niwajue vizuri ni sababu zipi zilizo waleta kwenye nchi hii?” Aami alitulia kwanza ma kumeza funda la maji ambalo aliliweka kwenye mdomo kutoka kwenye bilauri ambayo ilikuwepo mezani.
“Ulipata hizo sababu?”
“Yes, sababu zipo mbili tu na hao walinisaidia mimi sana kuweza kujua baadhi ya mambo mengine ya mhimu, sababu ya kwanza walikuja kuifanya kazi ambayo ilikushinda ya kumtafuta Zakaria lakini sababu ya pili wanakutafuta nawewe hapo pia na walikutana na mtu mmoja ambaye inasemekana ana taarifa zote za Zakaria” sentensi ambayo aliitoa Aami ilimfanya Qader awe na maswali mengi sana ya kuweza kuuliza.
“Kunitafuata mimi kisa nini?”
“Sina sababu ya kwanini wanakutafuta wewe haikuwa mhimu kwangu sana ila nilicho kijali zaidi ni baada ya kugundua kwamba walikuwa wamekuja kumtafuta Zakaria hilo ndilo jambo la msingi sana kwangu kwa sababu nilitaka niondoke kwenye nchi hii kwa muda nikapeleleze kwa umakini kwanza ndani ya nchi ya Libya nijue ni kitu gani ambacho kilikuwa kinaendelea au kama kuna siri ambayo ilikuwa inafichwa namimi siijui”
“Sasa kwanini haujaondoka?”
“Kwa sababu Zakaria yupo ndani ya Tanzania” hiyo taarifa ilimfanya Qader adondoke chini kwa presha, mwili uliloa jasho likaanza kumtoka kama vile yalikuwa ni maji,aliogopa mno baada ya kuipokea taarifa hiyo alikumbuka kwa jinsi Aami alivyo mwambia kwamba hicho kiumbe yeye pekee ndiye ambaye alikuwa ana uwezo wa kusimama naye kwenye ulimwenguni wa mapambano, Qader alitamani kama hizo zingekuwa hadithi za kufikirika tu lakini haikuwa hivyo huo ulikuwa ni ukweli ambao usingeweza kupingika kabisa, alijikuta anaishiwa mpaka nguvu Aami alimsogezea kikombe cha maji mtu huyo hakuwa na haja ya kumuonea huruma kwa sababu hayo mambo aliyaanza yeye mwenyewe.
“Hili jambo umelijua kwa muda gani na ulilijuaje?” Qader aliuliza huku akiwa anajitahidi sana kuweza kujikaza na kunywa maji ya baridi sana kwenye kikombe hicho.
“Dunia inaenda kasi sana kwa sasa inabidi ujitahidi sana uweze kuendana na kasi ya dunia pamoja na ulimwengu kwa ujumla vinginevyo utakuwa na maisha magumu yaliyo pitiliza, kitu cha mhimu zaidi ni taarifa jitahidi sana kadri uwezavyo kichwani mwako uwe na taarifa za kutosha, taarifa ni utajiri, taarifa ni maarifa bila kuwa na taarifa unakuwa kama mfu aliye hai wazungu wanasema INFORMATION IS EVERYTHING IN THIS FOURTH INDUSTRIAL REVOLUTION ERA, ukiwa na taarifa nyingi kujua haya mambo ni rahisi sana” alijibiwa kisomi mno na kubaki ameinamia chini.
Nadhani maelekezo umeyaelewa vizuri mkuu wa majeshi amaagizwa awakamate hao watu wa tatu pamoja na Qader na Aami mwenyewe, Zakaria yupo ndani ya mjengo….83 naweka nukta hapa tukutane ndani ya ukurasa wa 84.
Wasalaam
Bux the storyteller.