Gereza la Hazwa

Gereza la Hazwa

STORY: GEREZA LA HAZWA
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORY TELLER: Bux the story teller
AGE: 18+

UKURASA WA SITINI NA SITA

TULIPO ISHIA UKURASA WA SITINI NA TANO
"Mhhhhhhhhh ni hatari sana kama dunia nzima ingekuwa na watu wenye akili za hatari sana namna hiyo nimeelewa kwanini maraisi wengi wanapokuwa wanawateua viongozi wa usalama anatakiwa awaweke watu anao waamini mno kwa sababu hao ni rahisi sana kumtoa pale alipo" aliongea kamanda huyo akiwa tayari kuitekeleza amri ya mkubwa wake. Huyo alikuwa ni kiongozi wa siri sana wa kundi moja la makomando ambalo lilikuwa linaundwa na watu kumi tu pekee ambalo alilijua mkuu wa majeshi pekeyake, LDS10S ndilo lilikuwa jina la hao makomando na huyo 01THE FIRST alikuwa ndiye kiongozi wao, hiyo 01 ilikuwa ni kinyume cha 10 yaani kati ya wale kumi hiyo FIRST ilimaanisha yeye ndiye wa Kwanza kwa hao wanaume kumi wa kazi ambao mkuu wa majeshi alisema kwamba hakuna watu wa hatari kuwazidi hao wanaume ndani ya nchi ya Libya.

ENDELEA..........................
DAR ES SALAAM na VITONGOJI VYAKE
Hali ilikuwa tulivu sana kama ilivyokuwa kawaida kwa jiji hili pendwa kama wengi wanavyopenda sana kulinakshi na kuliita hivyo, watu wake walikuwa wanayafurahia maisha ya mkoa wao kwa sababu utulivu ulikuwa upande wao hali ya joto la kutosha uliwafanya kuvaa nguo nyepesi nyepesi na wengine kutembea vifua wazi, ni hali ya kawaida sana ndani ya hili jiji kila mtu huwa anajali mambo yake mwenyewe. MUNGU kawabariki amani kipi kingewanyima furaha? Licha ya heka heka za kutafuta namna ya kuipeleka mikono yao vinywani bado walikuwa wanayo furaha ya kutosha kupewa uhai ambao walijua wanaweza kuitumia kutafuta chochote kitu na kwa muda wowote ule.

Hali ilikuwa tofauti kabisa kwa kijana mmoja jioni hiyo wakati kiza ndo kimeanza kuingia alikuwa hana raha kabisa, uso wake ulifura kwa mawazo ambayo yalitoa kabisa tabasamu la uso wake alighafilika mawazo yalikuwa yamemchota mbali sana. Ni ndani ya kituo cha polisi cha Mburahati kijana ambaye jina lake lilikuwa linajulikana kama Karimu alikuwa amejiinamia kwenye meza moja humo kituoni, maisha kwake yalikuwa yanaenda kwa kasi mbaya sana hakuhisi kama mambo yalikuwa mazuri kwa upande wake kama alivyokuwa anasikia watu wengine wakiwa wanaongea juu ya hilo jambo. Ni siku kadhaa tu licha ua udogo wake kutokana na umashuhuri wake na weledi wake kwenye kazi ya vazi la polisi ambayo aliiheshimu sana na kuipenda kuliko kitu chochote kile alikuwa ni mtu mkubwa sana ndani ya jeshi la polisi, cheo cheke cha ASP kilimpa heshima ndani ya kituo kikuu cha polisi kanda ya Dar es salaam OSTERBAY POLICE STATION, aliheshimika sana lakini kwa sasa ilikuwa imebaki kama historia ambayo alihitaji kuamka ndotoni ili isiwe ya kweli bahati mbaya sana haikuwa ndoto ilikuwa ni kweli kwa kila kilichokuwa kinaendelea.

Mfadhaiko ulijionyesha wazi kwenye taswira ya uso wake, siku kadhaa nyuma alikuwa anaheshimiwa mno licha ya udogo wake wa umri lakini leo wale waliokuwa wakimheshimu ndio waliokuwa wakimcheka sana kwa kuporomoka kwake tena na kuletwa kwenye kituo kidogo kama hicho kutoka kituo kikubwa kama kile, alielewa nini maana ya maisha fitina zilifanya akakikosa kiti chake hicho kwa wakubwa wake, ni mambo ya kawaida sana makazini kuwekeana fitina kubwa hasa pale unapokuwa umepewa nafasi kubwa lakini hakuwahi kufikiria kama hilo jambo lingeweza kutokea kwa upande wake yeye hakukubaliana nalo kabisa alihitaji kuirudisha heshima yake ya vazi lake na alijua kabisa ile nafasi ni ya kwake yeye tu

"Hakuna mtu anaweza kunitoa kwenye nafasi yangu kiwepesi sana namna hii, mimi ni kijana ndiyo lakini sijaona mtu mwadilifu na mchapakazi kama mimi kwenye ile nafasi lazima niirudishe nafasi yangu kwa gharama yoyote ile" alitamka maneno hayo kwa msisitizo sana, sasa ni njia gani ambayo ilikuwa inaweza kumfanya arudi kwenye nafasi yake? Alitazama kwenye meza ambayo alikuwa ameilalia na kutabasamu.

Hapo palikuwa na file moja ambalo alilivutia upande wake na kulifunua, lilikuwa na kesi moja ambayo ilikuwa imetokea ndani ya jiji la Arusha, faili hilo lilikuwa linaonyesha picha za wanaume watatu ambapo kati yao mmoja alikuwa ni mweusi na wawili walikuwa ni waarabu, kuvutiwa kwake kuisoma habari hiyo ni kwa sababu alijua kitu ambacho kilikuwa kinahitajika ndani ya hiyo kesi. Ilikuwa inahusu wanaume hao watatu ambao walivamia hospitali ya mkoa wa Arusha na kumtishia mganga mkuu wa hospitali hiyo, ukiacha hilo pia nje ya hiyo hospitali walimkuta dereva tax ambaye alikufa kifo kibaya sana mwili wake ukiwa umekauka na kuwa mweusi na inasemekana mtu huyo alitokea airport na kwa mujibu wa taarifa ambazo zilikuwepo ni kwamba watu hao watatu huo muda walitokea airport maana yake kulikuwa na uhusiano mkubwa sana kati ya kifo cha dereva huyo na hao watu.

Swali la msingi ambalo lilitakiwa kupatiwa majibu ni kwanini hao watu waende hospitali kwa kuvamia kwa nguvu? Kwamba hawajui utaratibu wa hospitali? Jibu ni hapana sasa kwanini wavamie? Hilo alitakiwa kukupatia ufumbuzi haraka sana, alisoma chini yake kidogo ili kupata taarifa mwanini faili hilo lililetwa Dar es salaam, aliona taarifa ikisema kwamba watu hao walielekezwa na daktari huyo kwamba wanamtafuta mtu mmoja ambaye anaitwa Kani huku Dar es salaam alijulikana kama tajiri Kanivasi Zagota alikuwa ni mtu mwenye vyake vya kutosha ambaye hata kumuingilia kwake haikuwa rahisi sana namna hiyo, hivyo walijua wazi kwamba watu hao ni lazima wangehitaji kuja mpaka jijini Dar es salaam ili kumtafuta mtu wao ndio maana baada ya hospitali kufungua mashtaka zidi ta watu hao faili lilitumwa ndani ya polisi wa ukanda wa Dar es salaam.

Hiyo bado haikumridhisha sana aliwaza sana kwanini watu hao wasianze uchunguzi huko huko alisikitika na kutingisha kichwa chake kwa sababu aliwajua polisi wenzake namna walivyo hapo kuna sababu ya uoga na maslahi yao akawa amejua kwanini hawajafuatilia huko, swali lake la pili kwa kesi ilivyokuwa ilitakiwa faili hilo liende kituo kikuu cha polisi OSTERBAY maana yake kuletwa hapo ulikuwa ni mtego na nafasi ya pekee ambayo wakubwa zake walimpatia ili aweze kuitetea nafasi yake kama ataweza, hapo sasa alijiridhisha na kupata majibu yake yote, alitabasamu kinyonge sana halikuwa jambo rahisi sana kulifuatilia alielewa anaenda kumgusa mtu tajiri sana ambaye kwa namna moja ama nyingine lazima kuna wakubwa wake wa kazi wanashirikiana naye hilo alikuwa na uhakika nalo sana hakuwa mgeni na hiyo kazi yake.

Alisimama na kujinyoosha mifupa ikaitikia, hakuwa kijana wa hovyo mwili wake ulikaa kiume ndio maana alikuwa akijiamini, mikono yake ilimpa uhakika wa jambo lolote lile anapokuwepo, mafunzo makali ambayo aliwahi kuyapata yalimpa umaarufu sana kwenye mapigano ndio maana akiwa bado kijana mdogo alikipata hicho cheo chake.

"Naenda sehemu mbaya sana kuanza kuwagusa mpaka wakubwa lakini sina namna nyingine ya kufanya lazima niifanye hii kazi na kuirudisha nafasi yangu" aliongea huku akijifuta usoni moyoni alikuwa anatetemeka sana, aliiangalia saa yake ndipo alipogundua kwamba muda ulikuwa umeenda sana alitakiwa kuwahi kurudi nyumbani hata hivyo hakuona kama ulikuwa ni muda sahihi wa kwenda kwake kuna mtu ambaye alitakiwa kwenye kumuona majira hayo ya usiku ikiwa inaelekea saa mbili za usiku. Alichukua koti lake dogo na bastola yake ambayo alihakikisha kama ilikuwa na risasi za kutosha ndani yake akaiweka sawa na kuipachika kiunoni kwake kisha akatoka humo ndani na kupanda kwenye pikipiki lake la gharama ambalo lilimfanya atambe sana kila alipokuwa anapita.

Saa mbili na nusu alikuwa anapaki pikipiki yake sehemu ambayo ilikuwa na mgahawa, ni maeneo ya Mbezi kwa Zena alionekana kuwa mwenyeji sana ndani ya hilo eneo, alipita mpaka nyuma ya mgahawa huo kulikuwa na nyumba moja ndogo ila nzuri sana, hakupita mlangoni bali aliruka ukuta baada ya kutua ndani tu alijifunga kitambaa usoni kwake kilicho saidia kuiziba kabisa sura yake akawa haonekani zaidi ya macho yake na mikononi alivaa gloves. Hiyo nyumba hakuonekana kuwa mgeni nayo sana japo aliingia mwa wizi, ndani ya nyumba hiyo alikuwa anaonekana kijana mwingine ambaye muda mwingi alikuwa ameyaelekeza macho yake kwenye komputa yake kubwa pembeni zikiwepo komputa zingine nyingi za kutosha, machoni alikuwa amesheni miwani ya kazi, alihisi kama kuna kitu aliigeukia moja ya komputa ndogo ya pembeni na kubongeza batani zake kadhaa tu ikamletea mazingira ya nje ya nyumba yake hiyo.

"Shiiiiit ni mpuuzi gani ananivamia kipuuzi hivi" aliongea huku akitoa bastola yake kwenye droo na kuizima mitambo yake kisha akafunga hiyo sehemu ambayo ilikuwa ipo pembezoni mwa kabati kubwa la nguo chumbani kwake, ilikuwa ni sehemu ya ukuta tu ambayo kuna sehemu alikuwa anagusa kwa mkono wake wa kulia zinatokea namba ambazo zilimhitaji pia kuingiza namba kadhaa ili ukuta huo ujigawe na kutengeneza mlango wa kuingilia huko alikokuwa anafanyia kazi zake za siri sana, alitoka mpaka sebuleni na kuufungua mlango kisha akauegesha tu na kukaa nyuma ya mlango alijua huyo mtu wa nje anajua kwamba bado hajamshtukia, alihitaji kumjua ni nani huyo hasa ambaye anavamia kishamba namna mapema yote hiyo, kwenye mlono wake bastola yake ilikuwa imekaa vizuri sana.

Baada ya dakika moja alihisi kama kuna mtu anatekenya kitasa cha mlango wake altabasamu mtego wake ulikubali, ndani kulikuwa kimya sana zilikuwa zinasikika sauti za muziki kwa mbali tu ambao ulitoka kwenye redio aliyokuwa ameiwasha hapo sebuleni na sauti hiyo ndiyo iliyompa moyo mvamiaji kwamba ndani yake mwenyeji hakuwa makini na chochote.

Ni kama walikuwa wanaviziana kwani baada ya kuingia tu mwanaume huyo alitanguliza kurusha koti lake ambalo ,lilidakwa kiwepesi sana na mwenyeji cha ,ajabu alijikuta ameliweka chini ya ulinzi koti kwenye mkono wake, alilaani sana hicho kitendo wakati anainua macho yake juu yeye ndiye aliyekuwa amewekwa chini ya ulinzi na mvamiaji, bastola yake ilikuwa mkononi na hakufua dafu ila hakuwa na wasiwasi alitabasamu kitu ambacho kilimpa hofu hata mvamiaji alihisi huenda humo ndani kuna watu wengi hivyo akageuza jicho lake pembeni bastola akiwa amemuelekezea mtu wake hilo lilikuwa ni kosa, mwanaume huyo aliitoka miwani yake usoni na kuirusha kwa huyo mgeni wake wake ambaye aliikwepa hapo naye akapata nafasi ya kumnyooshea mtu huyo bastola hivyo wote wakawa wanaangaliana huku wamewekeana bastola.

Sheria za mapigano wote walionekana kuzijua vizuri, waliinama kwa pamoja na kuziweka bastola zao chini kisha wakazipiga mateke zikaenda pembeni waliipanga mikono yao, mgeni alikuja kwa kasi kwa sarakasi safi sana na kuzunguka na teke moja safi lakini mwenyeji aliepa kwa weledi sana na kupelekea teke hilo la nguvu kupita hewani tu, naye akarudisha mapigo ya haraka sana ambayo yalipanguliwa na mgeni kwa umakini sana, uwezo wao ni kama ulikuwa unaendana sana walishambuliana kwa dakika mbili mpaka pale walipopigana ngumi nzito sana za vifua na kila mtu akarudi nyuma kidogo kwa maumivu.

Mvamizi akiwa kwenye vazi lake jeusi usoni, alitabasamu kwa ndani na kuvikunja vidole vyake ilikuwa ni hatari akipata hasira ndivyo alikuwa anafanya kwenye ulingo wa mapigano hapo asingekuwa na huruma na mtu ambaye angeonekana mbele yake ila cha ajabu alishangaa yule mwenyeji wake anainama chini akaokota koti la huyo mvamizi pale chini na kumrushia kisha akaelekea kwenye friji akachomoa vinywaji viwili vya baridi kimoja akamrushia huyo, mvamiaji, hata yeye pozi lilimuishia ikabidi akidake tu hicho kinywaji wakati huo mwenyeji wake alielekea kwenye sofa na kukaa.

"Mhhhhh kwamba unanijua sana kiasi hicho?" Aliongea huku akivua hicho kitambaa chake usoni na kwenda kukaa kwenye sofa la pili yake, aliuwa ni Karimu kijana polisi mwadilifu huyu ndiye aliyekuwa amefika kwenye hiyo nyumba.

"Unahisi unaweza ukaniigizia mimi wewe, tangu umeingia hapa nilikuwa najua ni wewe hapo hakuna mtu mwenye akili zake timamu anaweza kuvamia saa mbili saivi tena akaingia kiboya hivyo" huyu alikuwa ni rafiki yake ambaye wamekua wote na wamesoma wote mpaka mafunzo ya jeshi la polisi waliyapata pamoja japo mwenzake alibahatika na kuchukuliwa moja kwa moja ndani ya idara ya usalama wa taifa akiwa anafanya kazi kama miongoni mwa wana IT (Information Technology) ndani ya idara hiyo.

"Hahahaha hahaha za siku nyingi kidogo" Karimu aliongea huku akipiga funda lingine la kinywaji
"Pole wewe hapo kwa majanga yaliyo kukuta nasikia umeshushwa mpaka kuwa polisi wa kawaida sana niliskitika sana mtu kama wewe kupata aibu kubwa namna hiyo"

"Hizi habari umezijuaje?
"Wewe ni rafiki yangu wa kufa na kuzikana na unalijua hilo lakini pia usisahau kwamba mimi ni nani kwenye upande wa mitandao unadhani kuna habari gani itatokea hapa nchini nisiijue mimi?" Rafiki yake aliijua mitandao kuliko hata chakula ndiyo maana hata ndani ya idara ya usalama walimuweka kwenye kitengo hicho nyeti cha taarifa kwa sababu walimjua vyema uwezo wake. Baada ya kuona mwenzake bado ameduwaa tu ilimbidi aendelee kuongea.

"Haya niambie hicho kilicho kuleta"
"Kwahiyo kuja kwako mpaka niwe na kitu kilicho nileta?" Alilalamika Karimu mbele ya rafiki yake

"Hauna lolote hujawahi kunitafuta kama hauna shida hivyo najua yamekukuta huko ndio maana umekuja kunitafuta" alimeza mate baada ya kuambiwa hayo maneno kwa sababu ndio uliokuwa ukweli wenyewe.

"Kuna taarifa nazihitaji"
"Nifuate"

Je ni kweli atayaweza haya mambo ya kuwafuatilia wakubwa ili tu kulinda nafasi yake kazini? Kijana mdogo anajiingiza kwenye vita za wakubwa.....acha 66 tuishie hapa

Bux the story teller
Chao.View attachment 2519734

Sent using Jamii Forums mobile app
Nitarudi kusoma
 
Njoo basi hata kidogo
Alen nae anazingua
 
Anazingua te na? [emoji23][emoji23][emoji23] watu mnapenda sana mambo ya kijana wa Tandale.

Baadae kidogo nikifika home naiweka
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom