Gereza la Hazwa

Gereza la Hazwa

STORY: GEREZA LA HAZWA
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: Bux the storyteller
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

UKURASA WA MIA MOJA NA NANE
TULIPO ISHIA UKURASA WA MIA MOJA NA SABA
“Kule tayari kuna vijana wangu wa usalama wa taifa wanamfuatilia kila hatua anayo ipiga nilihitaji nimuweke kwenye mkono wangu kabla wewe hujampata kwanza ila nilikuja kugundua mambo mawili, kwanza ni mtu mwenye ulinzi mkali sana japo hilo halikuwa tatizo kubwa lakini jambo la pili ni kwamba yule mtu ni mtu tajiri sana hivyo akipotea kiwepesi sana bila sababu za msingi wananchi wataanza kuhoji mno ukizingatia anawasaidia kwa misaada yake ya kuficha kile anacho kifanya hivyo nilikuwa nimeanza kwanza kukusanya taarifa zake ili niwe na ushahidi wa kutosha kumtia mbavuni hivyo vijana hao nitawapigia simu waondoke kule usije ukawakuta ila watakupatia taarifa aliko usiku huu, nakusikiliza kama kuna lingine” sasa heshimiwa alikuwa na amani na alikuwa anongea kijasiri sana baada ya kuona amani ya nchi ingekaa mahali pake.

ENDELEA………………………….
“Kuna mwanaume mmoja wa kiarabu kutoka Dubai anaingia siku ya kesho kutakapo kucha yeye akiwa na familia yake yote, huyo mtu amefunga safari kutoka huko Dubai kuja Tanzania kwa ajili yangu, baada ya familia yangu kuuawa kule Libya na mzee mmoja, nilienda kuiua familia nzima ya mzee yule kwa sababu wote walikuwa ni wahusika wa hayo mambo ambayo yalikuwa yametokea, lakini kuna kosa dogo nililifanya miongoni mwa watu wa ile familia ambao walipona huyu naye alikuwepo, nilienda kwa hasira bila hata kufuatilia chimbuko la familia vizuri hivyo nikahisi nimewamaliza wote kumbe huyu ndiye mtoto mkubwa na ni kwa muda mrefu sana yeye alikuwa anakaa mbali na familia na ndiye huyu anayekuja hapa Tanzania kunitafuta mimi ili aniue lakini kabla ya kuniua lengo lake anahitaji kiasi cha bilioni zaidi ya 900 za kitanzania ambazo nilizchukua kwenye kampuni ya baba yake na hicho ndicho yeye anacho kihitaji zaidi yupo tayari hata kuniacha hai endapo tu nitamoatia hizo pesa pamoja na utajiri wangu yeye kuhusu baba yake kufa hana shida na hilo jambo sana shida yake kubwa ni pesa”

“Na mimi siwezi kumpa hizo pesa kwa sababu nahitaji baada ya kumaliza hili hizi pesa nizisambaze kwenye vituo vya watoto yatima kuanzia Tanzania, Libya na barani Afrika kwa ujumla kwa watoto wenye uhitaji, walemavu na wazee ambao hawajiwezi bila kuwasahau wamama wajane. Lengo la mimi kukuomba msaada huu sina shida ya kwamba unisaidie ulinzi wala kunilinda ninacho kihitaji kwako ni kunipatia taarifa za mtu huyu atakapo tua kwenye uwanja wa ndege mpaka sehemu atakayo ifikia kwa sababu kesho kutwa ndiyo siku ambayo inatakiwa aivute pumzi yake ya mwisho ya yeye kuwa hai, kama ukinisaidia kwa hilo tu nitashukuru sana nadhani msaada wako utakuwa umeishia hapo kutakako baki huko nitamaliza mimi mwenyewe” maelezo ya Zakaria yalimsisimua sana mzee huyo kwa aina ya mauaji ambayo alikuwa anayasimulia yalikuwa yanamsisimua kila aliyekuwa anayasikiliza vizuri hilo eneo, mheshimiwa alijikohoza kidogo ili kujipa nafasi ya kuongea.

“Kuna kitu kingine chochote unakihitaji zaidi ya hiki?”
“Ndiyo”
“Kipi?” baada ya kuulizwa hilo swali aligeukia alipo Josephene na Stephano
“Nahitaji unilindie wale watu wawili nitakapokuwa kwenye kazi zangu huko hata kama kuna tatizo likinikuta basi hakikisha unawatunza vizuri kwenye maisha yao, wale ni watu wa mtaani tu lakini wamejitoa maisha yao kuweza kunisaidia mimi hapa ingali hata hawanijui kabisa hivyo nitakuwa mkosefu wa fadhila kama nisipo hakikisha usalama wao, nitashukuru sana kama utanisaidia kwa hilo”

“Ok nitakupa maneno yangu juu ya hilo lakini imewezekana vipi binti wa mtaani kama huyu kujitoa kwa mtu hatari kama wewe namna hii?”

“Hakuna anacho kijua kuhusu mimi na sitaki ajue mpaka siku namaliza hii kazi nitamwambia mwenyewe then atachagua yeye upande wa Kwenda ila nataka nimbadilishie maisha yake anastahili kuishi maisha mazuri sana nimekuja kugundua ni binti mmoja mwenye moyo wa pekee sana”
“Je unahitaji kuiona familia yako?”
“Unajua kwanini huwa sitaki kukutana nayo?”
“Sijui”

“Kwa sababu nahofia sana usalama wao, kuishi karibu na mtu kama mimi ni hatari kubwa sana kwa upande wao, usalama wao unakuwa hauna maana tena ndiyo maana nahitaji kukaa nao mbali, mimi nimezaliwa simjui hata mama yangu, baba yangu siwezi hata kuikumbuka sura yake nimebaki tu kusifiwa mimi ni miongoni mwa watu matajiri zaidi ndani ya Afrika lakini sina furaha kabisa, natamani sana niwajue ndugu zangu, natamani niione familia yangu iliyobaki lakini siwezi sitaki kuwaletea matatizo, mimi ni mtu ambaye nimekutana na mambo mengi sana magumu na mabaya tena ya kutisha sana ndiyo maana nahitaji kila aliye husika na hili hapa niweze kumlipa kile anacho stahili, sasa naweza vipi kuwa karibu na familia ambayo najua moja kwa moja nitawaletea madhara?”

“Hapana siwezi acha niendelee kuishi kama mkiwa, acha nijifanye kama sijawahi kuwa na familia wao kuishi kwa amani na furaha bila mimi hicho ni kitu bora zaidi kwangu sitaki niende kwao na kubadilisha hali ya maisha waliyokuwa nayo tangu mwanzo sitaki kuonekana kuwa tatizo kwa upande wao acha waishi kwa furaha” aliongea kwa uchungu sana mwanaume huku akitoa machozi linapokuja suala la familia kwake kilikuwa ni kitu ambacho kilikuwa kinamuuma sana alikuwa anakumbuka mbali sana, aliongea kwa hisia mno lakini hakujua kama nyuma yake kulikuwa na kundi la watu kama ishirini hivi walikuwa wanamsikiliza, mwanamke mmoja mzee alikuwa anajifuta machozi akiwa anasikiliza kijana huyo akiongea kwa uchungu sana.

Huyo alikuwa ni bibi yake kabisa mzaa mama yake, huyo ndiye aliyekuwa mama mzazi wa SEKELAGA PHILEBERT, siku ile mheshimiwa raisi anasema kwamba anaenda Bagamoyo kwa ajili ya kuongea na familia hiyo hakuenda kuongea nao bali alienda kuwachukua kwa sababu alikuwa amewaahidi kwa muda mrefu sana kwamba angehakikisha wanakutana na kijana wao Zakaria Mansour kwa sababu alikuwa ana uhakika kwamba ni lazima angekutana na mtu huyo tu ndiyo maana muda ule baada ya kumpata Josephene alijua kwamba itakuwa ndiyo sababu rahisi ya kumfanya Zakaria kufika hapo, licha ya kuhitaji kuongea naye lakini lengo kubwa zaidi kumleta mwanaume huyo hilo eneo ilikuwa ni kumkutanisha na familia yake. Ukimya ndio uliomshtua sana Zakaria licha ya kuongea hivyo alishangaa kila mtu yupo kimya akiwa anamwangalia yeye pekee ndipo alipoweza kugeuka nyuma alishangaa watu wemgi mno walikuwa kwenye hiyo kordo, wazee wawili wa kike na wa kiume wakiwa mbele alimwangalia vizuri sana huyo mwanamke mzee ambaye alikuwa nyuma yake alikuwa anafana naye sana ilimlazimu kujishika ngozi yake ya usoni ili kuhakikisha.

Jibu lake lilikuwa rahisi sana huyo alikuwa ni bibi yake mzaa mama, aliwahi kuambiwa kwamba yeye anafanana sana na mama yake, naye mama yake alifanana sana na amama yake mzazi hivyo yeye kufanana na mwanamke huyo kwa sababu mama yake mzazi alikuwa amekufa kwa muda mrefu sana ilimaanisha kwamba huyo ndiye bibi yake kabisa, alimkimbilia mwanamke huyo ambaye alikuwa ameenyoosha mikono kumsubiria mjukuu wake aje walikumbatiana kwa hisia sana, ilikuwa ni kwa mara ya kwanza kukutana na kijana wao ambaye walihesabia kwamba alikuwa ameshakufa kwa muda mrefu sana sasa walikuwa wapo pamoja. Huyo alikuwa mtoto wa pekee wa binti yao wa pekee ambaye familia hiyo ilibarikiwa kumpata walihisi kama wanamuona mtoto wao kwa sababu Zakaria alikuwa anafanana sana na mama yake mzazi kuliko hata baba yake mzee Mansour Jr.

Mheshimiwa raisi alipeana mkono na mkurugenzi wa usalama wa taifa kukamilisha jambo hilo haikuwa rahisi sana lakini hawakukata tamaa, alikuwa amewakamilishia ahadi familia hiyo kama alivyokuwa ameahidi kwa mara ya kwanza, hakuna kitu bora duniani zaidi ya familia as the saying goes GO EAST, GO WEST, HOME IS ALWAYS THE BEST, utakutana na watu wengi sana duniani, utakuwa na marafiki wengi sana duniani ila hao mtaachana siku moja pale kila mtu atakapo kuwa anahitajika kwao ila hata wewe utahitaji Kwenda kwenu, usije ukaa ukaisahau familia yako, familia ni kitu bora kuliko hata haya maisha ya pesa ambayo vijana wanajisifia nayo mjini, familia ni zaidi ya utajiri, familia ni zaidi ya rafiki na hao ndio watakao kuzika na kukukumbuka siku zote za maisha yako.

Zakaria alikuwa mwenye furaha sana, leo naye alikuwa ni mtu ambaye anaweza kukaa sehemu na akasema nina familia watu wakamuelewa, alihisi ametua mzigo mzito sana kwenye nafsi yake, alikuwa na sehemu ya kuegemeza bega lake wakati ambao angehisi kulia hichi kilikuwa kitu bora zaidi kwake, familia yake yote walikuwa wanajua kila kilichokuwa kimemkuta kwenye maisha yake hakuna ambaye alikuwa anahitaji kumuuliza ili kumkumbushia yale machungu ambayo alikuwa amesha yasahau tayari, alimuita Josephene na kumtambulisha kwa familia yake kuanzia sasa alikuwa ni mmoja wao kwa sababu ndiye aliyekuwa mke mtarajiwa wa Zakaria ilikuwa ni furaha kubwa sana kwa upande wao wote. Zakaria alimuingizia Stephano kile kiwango cha milioni miatano kama alivyo ahidi na kumuomba mheshimiwa raisi amsaidie kutekeleza hilo jukumu lake sasa rasmi alikuwa aningia kazini kwa mara ya mwisho Kwenda kuwasafisha wale ambao walikuwa wamesalia salia na usiku huo alikuwa anaenda kumalizana na Kanivas Zagota.

“Hakikisha unarudi ukiwa salama” ilikuwa ni kauli ya bibi yake ambaye alikuwa na tabsamu huku machozi yakiwa yanamtoka kama unavyojua bibi kwa mjukuu wake mapenzi huwa hayapimiki kabisa, alimkumbatia bibi yake na kumfuata Josephene ambaye alikuwa kwenye kilio kikali sana alikuwa anahofia anaweza akaenda moja kwa moja na asirudi tena kwa sababu hapo wasinge onana tena mpaka mwanaume amalize kazi zote yeye makazi yake makubwa yangekuwa ni hapo pamoja na familia nzima ya Zakaria mwanaume alimpiga busu kisha akaanza kuondoka akiwa na wataalamu wa komputa George na Rikardo hao kazi yao kubwa ilikuwa ni kumpatia taarifa na direction ya mahali ambapo alitakiwa kuwafuata watu wake ambao alikuwa anawatafuta, wakati anatoka hapo alitazama juu kidogo ya ukuta wa mlangoni paliandikwa SAFE HOUSE, alielewa kwanini mheshimiwa alichagua kuwaleta watu hao katika hilo eneo, alipewa vitu vyake vyote ambavyo alikuwa amechukuliwa na walinzi humo ndani kisha wakapanda kwenye gari na akina Rikardo pamoja na George familia yote walitoka nje kuwaaga wanaume walikuwa wanaenda kuitetea haki ya mnyonge ambayo iliibiwa na sasa Zakaria alikuwa anaenda kulifanya jambo hilo akiwa na baraka za familia nzima pamoja na mheshimiwa raisi wa nchi, aligeuka kuwaangalia watu hao ndani ya hilo geti kubwa ambalo ndani yake kulikuwa na ulinzi mkali sana wakiwa wanampungia mkono, kilicho mpa furaha kubwa sana ni baada ya kuona Josephene yupo kifuani kwa bibi yake, babu yake alikuwa pembeni akiwa mwingi wa tabasamu la furaha, aliwapa mkono wa kwaheri kwa mbali na kuingia kwenye gari kisha gari hiyo iliondoka kwa spidi kali sana hilo eneo.

“Mzee hivi unahisi hiki kitu ambacho umekifanya ni sahihi?”

“Yes kwanini?”

“Huoni itaonekana tunawalinda wahalifu?”
“Sasa hapo mhalifu Zakaria au watu walio mtendea ubaya?”

“Hata kama lakini kwa madhara aliyo yasababisha anahesabika kama mhalifu tu na anatakiwa kuadhibiwa”
“Nisikililize vizuri, sio kila sehemu inahitajika kufuatwa sheria sometime COMMON SENSE huwa ni bora zaidi hasa pale inapohitajika haki, kama sheria ingefuatwa kila mahali hata wewe hapo ilitakiwa kwa sasa uwe jela, huenda hata mimi ningetakiwa niwe nimesha ondoka kwenye hiki kiti kwa muda mrefu sana ila kwanini kuna muda tunatumia COMMON SENSE? Kwa sababu linaponingizwa suala la mwanadamu hakuna ambaye anaweza kufanya vitu kwa usahihi wa asilimia mia na sheria inahitaji usahihi wa asilimia mia je unahisi ni nini kitafanyika? Maana yake nchi nzima au dunia nzima inaweza ikakutwa kwenye hatia. Mashine yenyewe tu ina efficiency ya 75-100%, unahisi kwanini wameweka kuanzia 75% nadhani unaelewa maana yake, hakuna mtu ambaye angekuwa amefanyiwa mambo kama aliyoweza kufanyiwa Zakaria na akaweza kuyabeba moyoni huku walio yafanya wanatembea kwa amani na kukuna vitambi vyao kwanza nimechoka kukamata mijitu ambayo sheria zinayalinda na kuwatoa acha wafe taifa libaki kuwa safi nahitaji nchi yangu irudi kuwa bora kama mwanzo sitaki haya yanayo endelea”

“Kwa sasa ana baraka zangu zote kikubwa tu amenihakikishia kwamba hawezi kumuumiza raia wangu yeyote yule ambaye hana hati basi kwa lolote ambalo litamtokea nitamlinda mimi mwenyewe na hata huko Libya nimeandaa ndege ya kivita ambayo itampeleka na atakapo maliza kazi yake itamrudisha tena Tanzania” hayo yalikuwa ni majibizano kati ya mheshimiwa raisi na Jirio Mtashi mkurugenzi wa usalama wa taifa, wao walikuwa ndani wakiwa wanaangalia kwenye kamera za ulinzi namna mwanaume huyo alivyokuwa anaaga na kuondoka, mheshimiwa msimamo wake alikuwa ameamua kumsaidia Zakaria moja kwa moja kwa gharama yoyote ile.

Kanivas Zagota ndicho kituo kinacho fuata kwa sasa

Wasalaam

Bux the storyteller.
Hongera mr. Fabian
 
Hello wanafamilia wa Story za Bux na mwandishi Febiani Babuya.

Leo nimewaletea andiko lingine fupi.

Kwa wale ambao wanapenda sana simulizi za misuko suko ya maisha pamoja na maisha halisi ya mtaani haswa, basi simulizi ya MIMI NAITWA GAMA ipo kwa ajili yenu.

Simulizi inamhusu jamaa mmoja ambaye alizaliwa kwenye maisha magumu sana tena zaidi ya sana, ukitaka kujua nini maana ya maisha magumu basi wewe lisome jina lake tu hali ambayo inampelekea kuwa muokota makopo mtaani. Ugumu wa maisha yake unamfanya kumtupia lawama zote baba yake mzazi huku akimshuhudia mama yake akifa kikatili mbele ya macho yake mawili.

Anaahaidi kumuua baba yake kwa mkono wake mwenyewe, hasira zake zinampelekea kuishia gerezani kisha kuwa muuaji baada ya kutoka huko.

Maisha ambayo aliyachagua yanamfanya kuishia kuokota makopo na kula jalalani. Mwanaume huyo anafanikiwa kuishi mwaka mmoja tu wa furaha huku mwaka huo ukiacha majonzi makubwa sana kwa familia.

Ni bonge la simulizi hii usiikose kabisa ili uyasome maisha halisi ya mtanzania wa mtaani.

Hadithi inaitwa MIMI NAITWA GAMA na nimeiandika yote mpaka mwisho ila hii haitapatikana huku Facebook,instagram au Jf mpaka ulipie ndo utaweza kusioma.

Unaipata kwa shilingi 1500 tu, yaani elfu moja na miatano tu pekee, yote.

Lipia kupitia namba

0621567672
0745982347

Jina FEBIANI BABUYA

ILI UIFURAHIE WIKIENDI YAKO KWA KUYASOMA MAISHA YA MTANZANIA HALISI WA MTAANI HASWA.

Wasalaam.
Screenshot_20230528-070958_WhatsAppBusiness.jpg
Screenshot_20230528-070933_WPS%20Office.jpg
 
Hii ni simulizi ya kijasusi.....ambayo inamhusu kijana mmoja aliyepatwa kuitwa Jason.

Kijana huyu alikuwa ni mdogo wa jaji mkuu wa nchi ya Tanzania. Ambaye alikuwa akisoma ndani ya nchi ya Marekani.

Alikuwa kijana wa kawaida sana kwenye macho ya watu, ambapo alikuwa na mpenzi wake waliyekuwa wakisoma wote.

Mpenzi wake huyo alikuwa ni Agenti wa CIA bila kijana huyo kujua.

Kisa kinaanzia wapi?

Raisi wa nchi ya Tanzania anapigwa risasi tano za kichwa akiwa Tiptop darajani kwenye msafara wake usiku. Kesi hiyo inaangukia kwenye mkono wa jaji mkuu, ambaye alikuwa ni rafiki wa karibu wa raisi, anaapa kumuua aliye husika mbele ya mahakama.

Jaji huyo usiku mmoja kabla ya hukumu anapewa onyo kwenye simu kwamba aupindishe ukweli siku ya hukumu....

Siku ya HUKUMU.
Anamsomea hukumu ya kunyongwa mhusika ambaye ananyongwa mbele ya mahakama. Baada ya kutekeleza hilo anapokea simu ya kumpa dakika 15 tu za kuiokoa familia yake.

Anakimbia na kufika nyumbani anakuta mkewe amechomwa kisu cha tumbo akiwa mjamzito huku mwanae wa kike akiwa ameuliwa.

Anpiga simu kwa mdogo wake kumpa taarifa lakini naye anatokewa na mtu na kuuliwa huku akiwa amefanikiwa kumtamkia mdogo wake kwamba....."THEY HAVE KILLED YOUR BROTHER" (Wamemuua kaka yako).

Mauaji anayofanyiwa yanafanana na namna raisi alivyo uliwa, sasa kama mtuhumiwa alinyongwa vipi mauaji yawe yale yale kama ya raisi? maana yake muuaji hakufa? INAZALIWA SINTOFAHAMU.

Kijana huyo kwa uchungu anarudi kumzika kaka yake na mheshimiwa raisi wa nchi yake ambaye walijuana vyema kwa mengi yaliyokuwa yamejificha nyuma.

Siku kadhaa baada ya msiba, watu wanakutana na tangazo ambalo linawataka wahusika wa mauaji ya jaji mkuu na raisi wajitokeze ndani ya miezi sita, kisha waombe msamaha kwa jamii atawaacha hai..kama muda huo utaisha bila wao kufanya hivyo basi huyo mtu atafanya anavyotaka yeye..

Hapo ndipo tunaenda kumfunua huyo Jason na kumjua yeye ni nani baada ya kuanza kufanya mauaji ya kutisha.

Inaitwa: MUUAJI ASIYE NA HATIA (KISASI)

Softcopy yake inapatikana kwa shilingi 5000 tu.

0621567672 (WhatsApp)
FB_IMG_1685253683891.jpg
 
0621567672 (WhatsApp)View attachment 2639023
Itakua tamu sana hii
 
Nzuriiii mkuu hilaa tumalizeeh gereza la hazwa hilii tuamieeh uko mkuu!!!!!!
 
Back
Top Bottom