Gereza la Hazwa

Gereza la Hazwa

STORY: GEREZA LA HAZWA
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: Bux the storyteller
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

UKURASA WA MIA NA MBILI

TULIPO ISHIA UKURASA WA MIA NA MOJA

“Niliamua kuja kwenye nchi hii na kuyaishi maisha ya kawaida tu nikaamua kuanzisha familia nyingine napo mkaona haitoshi mkawa mnayarudia yale yale, mkaichukua familia yangu tena halafu unakuja bwana mdogo kama wewe unaongea mbele yangu kwamba unatamani kukutana namimi kwenye maisha yako, hiyo kauli yako una dakika tano tu za kuitekeleza vinginevyo utajuta maisha yako yote, ndani ya hizo dakika tano ndio muda pekee ambao unatakiwa uyatetee maisha yako kuanzia muda ambao nitaacha kuongea hivi sasa, wewe utakuwa mtu wa kwanza kabisa nahitaji ushuhudie Zakaria mwenyewe mkatili kuliko kiumbe chochote anavyokuwa kwenye maisha yake kama utakuja kutamani tena kuonana naye tena kama utafanikiwa kuishi leo” Aami maelezo hayo yalimchanganya maana yalichanganyikana na vitisho alitaka kuona mtu huyo ambaye alikuwa anatamani sana kupimama naye uwezo atafanya nini kama alivyokuwa ametoka kusema.

Macho yake yakiwa makini kumuangalia Zakaria aliona mtu huyo anauchomoa upanga wake kwa nguvu kisha kile kifundo cha ule upanga alijipiga nao kwa nguvu kwenye mbavu yake macho yalibadilika na kuwa mekundu sana ghafla, sura akiwa ameikunja kwa maumivu makali, moja, mbili, tatu mwanaume huyo alijifyatua hiyo sehemu kwa kasi unaweza ukahisi ni jini linakuja wakati huo Aami alibaki anashangaa alizikoki bastola zake haraka na kumuelekezea mwanaume huyo alikuwa tayari kumshambulia.

ENDELEA…………………
“Mhhhhh mhhhhhh ndio maana kuna muda mimi huwa siamini sana kama watu wote tuliumbwa na MUNGU mmoja tu pekee, haya mambo ambayo nimeyashuhudia hapa leo yamenifanya niache kabisa kujiamini kwenye maisha yangu inaonekana bado mambo mengi sana kuhusu dunia hii siyajui yaani haiwezekani mwanadamu umuue mwanadamu mwenzako kwa staili kama hii aisee kuna wanadamu ni wakatili hata shetani mwenyewe anakaa darasani kujifunza kwao, nimeogopa sana tena nimeogopa mno (alimeza mate) mara ya kwanza wakati nipo nje ya idara ya polisi niliwahi kujiaminisha kwamba nikilivaa hili vazi nitakuwa mtu wa kuogopwa mno na mtu hatari zaidi nchini kwa sasa nimekuja kugundua hakukuwa na taarifa ya kweli yoyote niliyokuwa naiwaza zote zilikuwa ni ndoto tu huenda mimi ni kiumbe dhaifu sana tena sana mbele ya watu na inawezekana kuna watu licha ya vazi langu la polisi bado huwa wananiona mlaini kama mtoto wa kike tu nadhani bado ninahitaji kujifunza kuhusu walimwengu pamoja na dunia yao wanayo iishi naogopa sana” Afande Chiko aliongea baada ya kuikagua miili ya watu watatu ambao walikuwa wameuawa kikatili sana ndani ya hoteli ambayo Zakaria alitoka muda sio mrefu na hawa ndio polisi ambao alipishana nao muda sio mrefu wakati anaondoka na gari yake eneo hilo, alikuwa hajawahi kukutana na kesi ya mauaji ya kutisha sana namna hiyo jasho lilikuwa linamtoka na mwili ulikuwa unamsisimka sana, aliwaza vipi kama upanga huo ungetua kwenye shingo yake yeye alimeza mate kwa shida sana wakati huo afande mwenzake ambaye alikuwa ni rafiki yake alikuwa ameishika laptop mkononi wakati anamsikiliza mwenzake huyo akiwa anaongea, laptop hiyo ilikuwa na video fupi ambayo ilichukuliwa kwenye kamera za humo ndani, aliifungua na kumgeuzia mwenzake aliyekuwa anaongea ili waweze kuiona wote wawili.

Waliangalia wote kwa makini lakini afande Chiko alishindwa kuendelea aliyafumba macho yake alizidi kuwa na hofu sana hakuwahi kuamini kwamba kuna wanadamu hatari na wakatili sana namna hiyo.

“Hawa mbona wamekufa kawaida tu, hii dunia bado hujayaona mengi kumbe Chiko kuna wakati niliwahi kuchaguliwa Kwenda kudumisha amani kule Kongo nilikuta na mtoto mdogo wa miaka nane anamalizia kumuua mwanajeshi mwenye nyota zake begani baada ya hapo alimkata kichwa kisha akaanza kunyofoa nyama moja moja kwenye mwili wa mwanajeshi huyo na kuil…….”

“Hey, Lama ujue unazingua mwanangu sasa unavaa hilo vazi la nini kama ulienda kulinda amani na unakuta mwanajeshi anauawa ukashindwa kuingilia kati hilo zoezi?” Chiko alishangazwa na mwenzake huyo kwa maelezo yake.

“Unakurupukaje kabla ya kuanza kujiuliza huyo mtoto alimdhibiti vipi yule mwanajeshi mpaka akaweza kumuua mtu mwenye mwili wa mazoezi sana kama yule? mimi nilijificha kwa sababu sikujua yule mtoto nyuma yake kuna nani na nani, mara nyingi wale huwa wanakuwa chambo tu ila wavuaji wenyewe huwa wanakuwa pembeni wakishuhudia Samaki ujichanganye ukiingia tu kwenye ndoano yao umeisha. Hii dunia kuna watu ni makatili sana lakini ukiangalia asilimia kubwa ya watu makatili wote huwa wanatengenezwa na ulimwengu, ukiona mtu anawaua watu kikatili namna hii usimlaumu kwanza huenda kuna sababu nzito sana nyuma yake, kwa mimi ningemlaumu sana kama angekuwa anaua halafu anaondoka na viungo vya mwili ningejua moja kwa moja kwamba mtu huyu anafanya biashara ya kuuza binadamu wenzake sasa kaua halafu kaacha kila kitu ina maana alikuwa ana kisasi nao hawa sema sisi polisi kuna muda ukurupukaji wetu na kujifanya wajuaji ndivyo vitu ambavyo huwa vinatuponza sana”

“Hawa wanaume watatu siku kadhaa nyuma ndio walio daiwa kumuua rafiki yetu afisa wa polisi Karimu na leo wao wameuawa sasa wewe huoni kama kuna muunganiko wa matukio hapa? cha msingi hii kesi sisi tukae pembeni tusije tukajichanganya kwa mambo ambayo hayatuhusu” Lama alimpa elimu kidogo mwenzake kwa kile ambacho yeye alikuwa nacho kwenye kichwa chake.

“Mhhhhh ndugu yangu sasa tunaiachaje kesi kiholela sana namna hii mwanzoni kabisa hivi? Ujue nilijua wewe utanipa moyo kumbe wewe ndiye muoga hata zaidi yangu, mimi nilitamani sana kumuona mtu huyu anaye yatenda haya matuk…….”

“Hebu kaa kimya Chiko usitake kuanza kunidanganya mimi kama mtoto mdogo juzi tu hapa vibaka wawili tu Keko hapo wamekupiga nusu kukuua pona pona yako niliwahi kuja leo unaanza kunipigia kelele eti unataka kukutana na jitu kama hilo? Hivi umejiuliza kwamba kwanini kesi ya Karimu wakubwa wameamua kuimezea kama haijatokea? Endelea kujishaua mwenzako hapa nilipo mke wangu ni mjamzito inabidi nimlee mwanangu kwa mikono yangu miwili na kwa jasho langu akikua ajivunie uwepo wa baba yake duniani. Juzi nimepata taarifa za siri kwamba walitumwa makomando wa hali ya juu sana kumtafuta mtu huyo mpaka muda huu tunavyo ongea hakuna komando hata mmoja ambaye anaweza kutembea vizuri kwa miguu yake na nasikia komando mmoja amekufa japo wameliweka hilo kama siri nzito sasa kama unataka kufa sawa kamtafute na uoga wako huo mtu mwenyewe mifupa yako ina maji kibao milaini kama mtoto mdogo ukipigwa ngumi moja tu mpaka usubiri dakika kumi ndo ipoe unaanza kusema ukawatafute watu mjinga wewe” Chiko alikuwa anaogopa sana ndiyo maana alimpa taarifa rafiki yake Lama ambaye kwa namna moja ama nyingine alijua ni lazima atamfariji kumbe huyo ndiye ambaye alikuwa anayajua madhara ya hayo mambo kuliko hata yeye, walianza vizuri lakini walimaliza vibaya ambapo kila mtu aliondoka na njia yake hawakuhitaji kuendelea na kesi hiyo ambayo ilionekana kususwa mpaka na wakuu wa nchi.


Chumba kilikuwa kimya sana hakuna hata mtu mmoja ambaye alikuwa anatoa kauli, mkuu wa majeshi alikuwa ameingia ndani ya chumba hicho kuwajulia hali vijana wake, kilikuwa ni chumba kikubwa ambacho kilikuwa maalumu kwa ajili ya kuwatibia makomando hao ambao walikuwa hawaonekani hovyo mtaani na kama ungekutana nao mtaano basi usingekuwa na uwezo wa kuwatambua kwamba ni makomando maisha yao yalikuwa ya siri sana kwa sababu ilikuwa ni hazina ya serikali. Mzee huyo aliwaangalia kwa huzuni sana aliwaonea huruma mno vijana hao sio kwa sababu tu kwamba walikuwa wamepunguza nguvu jeshini hilo halikuwa tatizo kubwa sana kwa sababu alikuwa na hzina ya makomando wa kutosha ila aliwaonea huruma kwa sababu walikuwa wanajitoa kwa ajili ya nchi na ndiko huko ambako walipata majeraha yao ya kutisha hayo huku wakiwa wamempoteza mwenzao mmoja Zakayo, huyo ndiye alikuwa mfupi zaidi kati yao na ndiye ambaye alikuwa mcheshi mno mara nyingi wakikutana mtu huyo alikuwa anawafanya muda wote wawe wanacheka tu lakini leo hakuwa mmoja wao hivyo hakukuwa hata na mmoja wao ambaye alikuwa na hamu hata ya kuongea kwa wale ambao walikuwa macho baada ya kupata matibabu kutoka kwa madaktari maalumu ambao walitumwa na mzee huyo.

“Nimepokea simu kutoka kwa mheshimiwa raisi taarifa zake ni za kusikitisha lakini akiongea yeye ndiyo basi jambo linakuwa limeisha hakuna kingine cha kuweza kukifanya, ameagiza kwamba hili jambo ambalo tulikuwa tunalifuatilia tuishie hapa hapa huko kuliko bakia anaenda kulitatua yeye mwenyewe na anajua namna ya kulimaliza hivyo anashukuru sana kwa mchango wenu wa kujitoa kwa dhati na kulipambania taifa kama wapambanaji wa kweli, hivyo kwa kutambua mchango wenu na mlicho kifanya ametenga fungu kwa ajili yenu kila mmoja wenu kwenye akaunti yake ataingiziwa shilingi milioni mia tano na mwenzenu ambaye ameshatangulia kesho mtamuaga mwili utapelekwa kwao kwa ajili ya mazishi na pesa hizo zitaingizwa kwenye akaunti ya mkewe, kama kuna mtu ana swali tutaongea kwa wakati mwingine tukipata nafasi ya kuonana tena” mzee huyo hakuwa na muda wa kuwajibu maswali yao alikuja hapo kutoa maagizo ambayo yalitoka kwa mheshimiwa raisi na yalihitajika kuchukuliwa hatua haraka iwezekanavyo wanajeshi hao kila mmoja wao alipewa ruhusa ya mwaka mmoja wa kupumzika hivyo hawakutakiwa kujihusisha na chochote kwa ule muda.

“Koh koh koh, hili jambo limenishangaza sana kwanini kirahisi sana namna hiyo walipotezee hili jambo kwa watu kama wale hamuoni kama ni hatari kwa taifa letu?” aliongea kijana mmoja ambaye mkono wake ulikuwa umevunjwa vibaya hapo alikuwa amewekewa smenti, wenzake waligeuka na kumwangalia na kusikitika sana.

“Ukiona jambo hadi raisi kaingilia kati jua lipo sehemu za juu sana na usidhani kwamba wewe ndiye pekee unaye tegemewa na nchi wapo watu wengi sana ambao ni imara kuliko hata sisi nadhani wamefanya hivyo kwa sababu hili jambo limeonekana kuwa nje ya uwezo wetu, tulikuwa wengi sana ona kilicho tukuta sasa je kama angeenda mtu mmoja au wawili nadhani wangekuwa walishakufa wote, hali zetu zitakapo kaa sawa wote tutatawanyika kila mtu aende kwao au kwake tutakutana baada ya huo mwaka mmoja kwa mara nyingine tena” aliongea Gideone mwanaume ambaye ndiye aliyekuwa kiongozi wao hakutaka kupingana hata kidogo na kauli ya mkubwa wao alijua hiyo ilikuwa ni sheria na moja kwa moja ilitakiwa kufuatwa.

“Mini naungana nawewe moja kwa moja kwa hali tuliyo nayo sasa hivi hatuwezi kupambana bali tutakuwa ni mzigo ambao nasisi tutahitaji kusaidiwa kikubwa tumshukuru mheshimiwa katukumbuka na kutujali, ila mpaka sasa sielewi kitu kimoja iliwezekana vipi wanaume saba tukapigwa na mtoto mdogo sana namna ile aisee nilijiona nakufa pale pale sikuona nafasi ya mimi kuendelea na maisha mengine tena duniani niliogopa sana” alikuwa ni kijana mwingine ambaye naye mkono wake ulikuwa umewekewa chuma.

“Umri huwa ni namba tu unajua watu wanao kulia nchi za wenzetu wako mbele ya muda sana, kazi ambazo wewe umeenda kuanza kujifunza na kuzifanya baada ya kumaliza masomo wenzako wanaanza akiwa na miaka mitano tu mpaka aje afikishe miaka ishirini linakuwa jitu la kutisha na ndicho nilicho kiona kwa yule kijana, ni mdogo sana kwa muonekanao ila ni mtu hatari sana yule, sijui aliingiaje mpaka akawa anatafutwa na serikali sitaki hata kujua sana ila nakiri yule jamaa sitamani nije nikutane naye kwa mara ya pili asante yake Hamisi kuwahi na silaha yake vinginevyo tungekufa” Hamisi aligeuka baada ya kusikia mwenzake mmoja akimshukuru, huyu ndiye pekee kwenye hilo kundi aliyekutana na Zakaria, alikatwa mkono wote na kuteguliwa mguu, mguu ulikuwa umenyooshwa tayari ila mkono ndo ilikuwa basi tena alifungwa bandeji.

Alijikaza na kukaa kwenye kitanda chake hicho kisha akatabasamu baada ya kuwangalia wenzake
“Huyo bwana mdogo ambaye mnasema ni hatari ni wa kawaida tu tena sana, huyo jamaa niliyekutana naye mimi nimekuja kuelewa kwanini taarifa zake zinafichwa sana leo usiku nimeingia kwenye mtandao mmoja wa siri kutafuta hilo jina nimepewa historia ya maisha yake (aliwasimulia wenzake kwa ufupi walisisimka sana baada ya kusikia stori hiyo) huyo jamaa siyo binadamu ni kama jini, ni mwepesi isivyo kawaida akishika upanga kwenye mkono wake ni zaidi ya silaha zangu ninazo tumia kurushia risasi, ngumi yake ni kama chuma kuanzia leo najiweka kando na haya mambo mimi bado ni mdogo sana ndani ya huu mwaka natafuta mke nikaoe tu kwa namna nilivyo muona yule jamaa akiwaua wale watu sita pale angekutana na sisi wote hakuna ambaye alikuwa na uwezo wa kuzimaliza dakika hata tatu akiwa amesimama tungekuwa tumekufa mpaka sasa ila namshukuru MUNGU sana hili vazi langu la jeshi limeniokoa sana anaonekana ni mtu anaye liheshimu sana hili vazi” maelezo yake yalimuacha kila mtu hoi, walikuwa nane na sasa walibaki saba wakiwa majeruhi na mmoja wao ambaye hakukatwa sehemu yoyote alikuwa amepotewa na fahamu zake mpaka muda huo hakuwa mwingine alikuwa ni Rafael yeye alilala kitanda cha juu zaidi ya wote.

“Mshenzi wewe nakuua nakuua mimi huwezi kupigana namimi, hii nchi sio ya kufanyia kila uhalifu nitakufunza adabu mjinga mkubwa wewe” Rafael alikurupuka kutoka kwenye huo usingizi na kuruka mpaka chini, alipanga ngumi akiwa ana hofu sana, jasho lilikuwa linamtoka mno alijihisi bado yupo mbele ya Aami, alikuja kukaa sawa na kushangaa wenzake wapo vitandani wengine hawana mikono, alitulia na kukaa chini alitoa machozi mno wenzake walimsikitikia mwenzao alikuwa kwenye presha kubwa akihisi mtu huyo bado alikuwa karibu yake.

Wanaume wamenyoosha mikono na kujiweka kando vita ilikuwa haiwahusu hata kidogo, nani anaenda kumzuia Zakaria au Aami? Kumbuka sasa ameanza kuitumia ile sehemu yake ya ubavu ambayo Salem Malek aliwahi kuonywa na Razack Hakimu kwamba kijana huyo asije akaguswa kwenye hilo eneo na yeye ndiye aliye mtibia kijana huyo leo alikuwa amejipiga mwenyewe mbele ya kijana Aami sijui anaenda kuwa vipi ikiwa amemuahidi Aami kwamba anaenda kuwa binadamu wa kwanza kumshuhudia uhalisia wa nguvu zake zote za mapigano………102 naweka nukta hapa tukutane tena wakati ujao.View attachment 2630348
Mkuu huwe unatag🙌🙌
 
Back
Top Bottom