Gereza la Hazwa

Gereza la Hazwa

#GEREZALAHAZWA
FB_IMG_1684220330625.jpg
 
STORY: GEREZA LA HAZWA
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: Bux the storyteller
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

UKURASA WA TISINI NA TISA

TULIPO ISHIA UKURASA WA TISINI NANE

“Naenda huko kwa sasa, nipigie kesho asubuhi nakuingizia milioni miatano kwenye akaunti yako ya benki, tumia milioni miambili kutatua hiyo changamoto ambayo inaisumbua sehemu hii ya Manzese na hiyo milioni miatatu ni pesa yako wewe hapo badilisha maisha yako hakikisha unayaishi maisha kwa usahihi bila kumuumiza mtu yeyote kwa sababu ya pesa. Kitu ambacho unapaswa kukizingatia kwenye maisha yako ni kuishi vizuri maisha ni mafupi sana na usije ukaingiwa na tamaa ukataka kukimbia na hiyo pesa yote utakuwa na maisha mafupi sana kwa sababu hakuna binadamu anaweza kunikimbia kwenye hii dunia nadhani hilo unaenda kulithibitisha baada ya kunijua kwa siku kadhaa zijazo unaenda kuniona kwenye kila sehemu ya mitandao ya kijamii na vyombo vya habari” aliongea akiwa anamgonga gonga mgongoni bwana mdogo huyo akiwa anampa business card yake ambayo ilikuwa na namba yake pembeni alitakiwa kumpigia asubuhi ya kesho yake aipate hiyo pesa.

Huyo kijana alionekana kuwa mwaminifu sana kwake kwa namna alivyokuwa anajieleza mbele yake ndiyo maana alimpenda kama mdogo wake na kuamua kumuachia hizo zawadi, walitoka mpaka nje ambapo alisogea walipo wale wamama aliwakabidhi kila mtu fungu lake ambalo lilikuwa bunda lenye pesa za kutosha wamama hao walibaki wanagala gala chini wakimshukuru mwanaume aliondoka mpaka kwenye gari yake na kuelekea alipo Josephene huko Sinza.

ENDELEA…………………..
Ndani ya nchi ya Libya mheshimiwa Malek Salem alikuwa kwenye ofisi yake alikuwa anapokea taarifa ambazo zilikusanywa ndani ya GEREZA LA HAZWA kwamba ni kitu gani kilitokea mpaka mwanaume huyo akaonekana kwamba amekufa, kijana wake ambaye alimtuma Kwenda huko kufanya huo uchunguzi alikuwa ni 01THE FIRST kiongozi wa kundi la LIBYAN DEADLY SECRET TEN (10) SPECIALISTS (LDS10S) ambaye alikuwa komando wa kutisha sana ndani ya nchi hiyo na alikuwa kiongozi wa kundi hilo hatari ambalo lilikuwa na watu wa kutisha sana na hao ndio ambao Zakaria alifanikiwa kuwakimbia siku ile wao wakijua kwamba mtu huyo alikuwa amekufa ndani ya maporomoko yale ya maji lakini visu alivyokuwa amepigwa havikutosha kutoka na maisha yake, siku ile wakati anadondokea kwenye yale maporomoko makubwa walijua huenda tayari alikuwa amekufa lakini alikuwa amefanikiwa kutoka hai, hivyo mwanaume huyo alitumwa huko Gerezani ili ajue ni nani ambaye alikuwa anasimamia shughuli ya siku hiyo atoe maelekezo namna mtu huyo alivyoweza kutoweka ndani ya gereza hilo mpaka isemekane amekufa.

“Nipe ripoti” aliongea huku akiwa anajifunga vifungo vya shati yake alitoka kwenye chumba cha pili ambako kulikuwa na mchepuko wake wa siku zote, aliihusudu sana ngono mheshimiwa huyo raisi ambaye kiuhalisia alikuwa ni mkuu wa majeshi wa nchi ya Libya, mwanaume ambaye alihitaji taarifa kutoka kwake ndiye ambaye aliupanga mpango mzima wa kumuondoa raisi wa nchi hiyo na kumuweka kiongozi wake huyo ilikuwa ni siri ya watu wachache sana ikiwa ni mheshimiwa huyo, mchepuko wake pamoja na hilo kundi lake la hatari sana ambalo alikuwa analiamini mno.

“Yule mtu yupo hai” 01THE FIRST aliongea kwa ujasiri sana akiwa na uhakika na taarifa yake ambayo alikuwa anitoa.
“Nilitegemea hilo vipi unaweza ukaniambia umeweza vipi kujihakikishia hilo jambo?” mkuu huyo aliuliza akiwa anajifuta kwenye uso wake joto lilimuandama sana kwa shughuli ambayo alikuwa ametoka kuifanya muda mfupi tu ambao ulikuwa umepita.

“Nimeenda mpaka kwenye ule msitu na kufanya tafiti kila sehemu ambayo vijana walikuwa naye, kuna kosa dogo lilifanyika ila kosa hilo linaweza kuja kuwa hatari zaidi kwa baadae kama hatutalishughulikia mapema,ni kweli siku ile vijana walifanikiwa kumlegeza baada ya kumchoma na visu flani vina sumu kali sana visu hivyo huwa kwa nje havina majeraha makubwa sana kwa sababu kwa mtu wa mazoezi sana unaweza ukamtazama mwili wake na wala usijue kama amechomwa na visu hivyo huwa vinatengeneza majeraha makubwa sana kwa ndani ya mwili. Kwa namna walivyo nisimulia ilivyokuwa kwa lile giza mtu huyo alikuwa na akili ya ziada sana kwenye kuyafanya mamuzi yake, wakati anafanya maamuzi ya kuruka kuelekea kwenye yale maporomoko haikuwa kweli kulikuwa na mizizi mikubwa ya mti mmoja mkubwa sana ambao upo pembeni kidogo ya yale maporomoko hivyo wakati anaruka alishuka na mzizi mmoja na kujibanza kwenye kuta za ile ardhi ya maporomoko”

“Alikaa hapo kwa muda mrefu mpaka alipo hakikisha kwamba wameondoka naye alitoka kwenye hilo eneo na kuondoka hapo lak………” mkuu wake aliingilia kwanza hayo maongezi kama vile hakuelewa

“Umeniambia visu alivyo chomwa vilikuwa na sumu kali sio”

“Ndiyo mkuu”
“Sasa aliwezaje kutoka na kuondoka kwenye hilo eneo kwenye eneo gumu kama hilo?”

“Baada ya kutoka kule chini ambako alikuwa amejihifadhi, pembeni ya ule mti kuna majani ya mti mmoja hivi huwa ni dawa ya kutoa sumu yoyote kwenye mwili wa mwanadamu hasa kwa mtu ambaye ana jeraha au aliye ng’atwa na nyoka akijipaka na kutafuta hakuna kinacho mkuta anakuwa kawaida kama mwanzo tu na sehemu ile nimekuta majani kadhaa chini yakiwa yamesagika maana yake aliyatumia kujichua kwenye majeraha yake ndiyo maana aliweza kutoka pale akiwa na nguvu mpya kwenye mwili wake” maelezo hayo sasa ndiyo yaliyo mhakikishia mkuu huyo wa majeshi kwamba ni kweli huyo binadamu alikuwa ameondoka hilo eneo akiwa salama kabisa.

“Lakini kule mbele si huwa kuna majoka makubwa na ya kutisha sana?”
“Ndiyo”
“Ile ndiyo njia pekee ya kuweza kutoka mle ndani na kwa mtu kama yule unahisi alitokaje?”
“Yule jamaa ni msomi na mhandisi wa mambo ya uchoraji wa majengo na uandishi wake,akikaa eneo fulani kwa muda mchache tu anaweza kuchora eneo zima kwa dakika tano tu hivyo kwa namna ile sehemu ilivyo kaa kuweza kujua kwamba njia iko wapi kwa mtu kama yule ni jambo jepesi sana”

“Mhhhhh kuna kingine juu ya kupotea kwake?”
“Ndiyo mkuu”

“Nakusikiliza”
“Kuna wanajeshi wawili siku ile majira ya usiku walikuwa wanatoka Kwenda kufuata chakula walipotea jumla mpaka asubuhi hawakutoa taarifa kwamba wamefika sehemu ya kuchukua mzigo hiyo ilileta shaka mkuu wa gereza akawa ametuma watu wafuatilie kwamba ni nini kiliendelea, baada ya kufuatilia ile njia ya kujia mjini walimkuta mmoja akiwa ameuliwa vibaya sana na mmoja hayupo pamoja na gari na ndio usiku ule ule ambao Zakaria alipotea kule”

“Whaaaaaat”
“Ndio mkuu inaonekana alitumia lile gari kuondoka lile eneo”
“So where is he now? Maana nimeona raisi wa nchi ya Tanzania kanipigia simu siku kadhaa akiwa ananiuliza mambo hayo hayo nahitaji huyu mtu apatikane kwa muda mchache sana ujao itakuwa ni hatari sana kwa upande wa usalama wangu kama haya mambo yatajulikana si unajua hata lile gereza japo lipo chini ya nchi ila kinacho fanyika kule ni kinyume na haki za wanadamu hata umoja wa kimataifa ukijua nipo kwenye hatari na ile biashara yangu ya mapigano ya ulingoni itaniletea matatizo nahitaji hili jambo liishe mapema sana” alikuwa ameuliza swali na maelezo kwa ujumla mheshimiwa huyo aliona kabisa mambo yanakwenda kubadilika kwa spidi ya ajabu sana bila kujua mwafaka wake ulikuwa unakuwa ni upi lakini kabla 01THE FIRST hajamjibu chochote mlango ulifunguliwa kwa nguvu sana kuna kijana aliingia na mlango huo kwa pupa sana, 01THE FIRST aliruka sarakasi moja maridadi sana na kusimama mbele ya mkuu wa majeshi kwa sababu kazi yake ya kwanza ilikuwa ni kuhakikisha usalama wa mtu huyo kwa gharama yoyote ile, aliitoa bastola na kumnyooshea kijana huyo alikuwa tayari kumumlazima kijana huyo.

Kijana huyo alipiga magoti akiwa ameinama chini kwa heshima lakini pia alikuwa ameenda kinyume na sheria ya nchi, yeye alijua huyo mbele yake ni mheshimiwa raisi wa nchi hiyo kwani hata sura yake ilikuwa ni ya Salem Malek, raisi analindwa sana na sio mtu ambaye unaweza kumfikia kirahisi sana namna hiyo, 01 alishusha bastola yake baada ya kugundua kwamba huyo alikuwa ni kijana ambaye alikuwa anafanya kazi kweye ofisi ya teknolojia ya taarifa hivyo mpaka kuja hapo alikuwa ana taarifa za maana sana, mkuu wa majeshi alisogea mbele ya kijana huyo na kutamka kwa sauti yake nzito sana.

“Ongea”
“Bosi mtu ambaye ulituambia tuzitafute taarifa zake tumezipata picha zake”

“Whaaaaat” mkuu wa majeshi alimfuata kijana huyo na kumnyanyua akiwa amemshika shingo yake bila kujali kwamba kijana huyo alikuwa amekuja kwa wema tu ila alizihitaji sana taarifa hizo kwa namna yoyote ile.

“Mtu huyo amesambaza picha zake sita mtandaoni na kuandika jina lake halisi” kijana huyo aliongea huku akiwa anatetemeka sana kwani mkuu wao alikuwa amebadilika sana na mwilini mwake siku hiyo hakuvaa suti bali kulikuwa na kombati ya jeshi iliupamba mwili wake, kijana huyo alikuwa na simu mkononi alimpokonya kijana huyo kwa nguvu na kumuachia, aliishika na kuangalia vizuri picha hizo, yes alikuwa ni Zakaria mwenyewe.

“Mmeona kwamba yuko wapi?” alimgeukia kijana huyo akiwa amemkazia macho
“Hizo zimepostiwa kwenye mtandao ambao domain yake inatumika ndani ya nchi ya Tanzania kwahiyo yupo ndani ya nchi ya Tanzania japo hajulikani yupo kwenye eneo lipi maana tumejaribu sana kutafuta hilo jambo baadae tukaja kugundua ni hatari sana eneo alilo litumia wakati anaposti hizo picha ni eneo moja lenye ulinzi mkubwa sana liliua mpaka komputa kumi ofisini wakati tunalazimisha kulijua” baada ya kutoa taarifa hizo mkuu huyo alimgeukia 01 na kumpa ishara kijana huyo alipewa ishara ya kutoka humo ndani kazi yake alikuwa tayari ameikamilisha hakukuwa na cha ziada kwake.

“Inabidi uwatume vijana haraka sana ndani ya nchi ya Tanzania leo leo kwa gharama yoyote ile huyu mtu anatakiwa kupatikana haraka sana kama sio kuuawa kama akikutana na raisi wa nchi yake litakuwa ni jambo la hatari sana kwa upande wangu, THE FIRST I trust you nina imani vijana wako nane walio baki unawaamini kwenye kazi wachukue watano waende kule this time sitaki the same mistake kama mliyo ifanya usije ukanifanya nikawaua kwa mikono yangu mimi mwenyewe”

“Nimekuelewa mkuu ndani ya nusu saa ijayo ndege ya jeshi inawapeleka mpaka Kenya baada ya hapo kule wataingia kama raia wa kawaida tu kwa sababu Kenya sheria zao hazibani sana tutawaekekeza kwamba tumetoa escot kuwapeleka watu wetu kwenye ubalozi kule na ndiyo nafasi tunayo itumia kuwaingiza kule Kenya ila baada ya hapo wataingia Tanzania kama watalii tu wa kawaida rubani atarudi na ndege huku then wakimkamata kuna watu tutawatuma kuwachukua kama ikishindikana basi nitawapa maagizo kwamba wamuulie huko huko kabla hakujawa na matatizo”

“Ndiyo maana nilikuamini na kukupa hiyo nafasi najua huwezi kuniangusha ukitoka hapa wapigie simu na uwasisitize sana wasije wakajulikana ni bora anaye julikana afe lakini hili jambo libaki kuwa siri kubwa sana ambayo hakuna mtu ataipata kiwepesi, mimi kwa sasa naenda huko gerezani nikaonane na huyo mpuuzi ambaye alikuwa lindo mpaka mtu huyo akatoweka”

“Sawa mkuu” 01 alitoa heshima na kutoka humo ndani,mheshimiwa alijifuta jasho mambo yalikuwa ni magumu sana upande wake ila hata hivyo alifurahi sana baada ya kujua eneo ambalo mtu huyo alikuwepo kwa huo muda kidogo ilikuwa ni nafuu kwa upande wake kama angepatikana na hakuwa na wasiwasi sana na vijana wake hao ambao alikuwa anawaaamini sana. leo kwa mara ya kwanza alitoka na kimada wake hadharani na kupanda naye kwenye helikopita kuelekea ndani ya Gereza la Hazwa, saa moja lilimtosha yeye kufika ndani ya gereza hilo aliingia ndani akiwa na hasira sana, alipokelewa na mkuu wa gereza huko walikuwa wanamuita bwana jela.

“Nipe majina ya watu ambao walikuwa wanasimamia humu ndani siku hiyo mpaka mtu huyo akafanikiwa kutoroka humu ndani kiwepesi sana namna hiyo” aliongea akiwa amemkazia macho mkuu wa gereza hilo, alibabaika sana mzee huyo ambaye alikuwa na kitambi cha wadhifa leo alikuwa anatetemeka mbele ya mkubwa wake wa nchi. Hakuchukua muda waliletwa wanaume kama sita mbele yake alimwangalia kila mmoja kwa wakati wake akiwa ana hasira nao sana mkononi mwake alikuwa na bastola mbili ambazo zilijaa risasi.

“Hivi nyie wapuuzi mnajua ni kiasi gani niliwekeza ili kumpata huyu mtu mpaka akafika kwenye hili gereza? Mnajua ni pesa kiasi gani nimepoteza baada ya yeye kuacha kupigana hapa ulingoni? Na mnajua ni hasara kiasi gani na madhara yatakayo tokea baada ya kuruhusu jambo la kijinga kama hili?” aliuliza akiwa anamzunguka mmoja mmoja, hakuna aliyekuwa na jibu la kutoa alipita mbele yao na kuwamiminia risasi za vichwa kwa hasira sana walikufa vibaya mno, wengine waliokuwa pembeni pamoja na mkuu wa gereza hilo waliogopa sana hawakuwahi kumuona mheshimiwa huyo akiwa kwenye hali kama hiyo.

Baada ya kutekeleza hilo tukio alitoka humo ndani mkuu wa gereza akiwa na mrembo wake, alienda mpaka kwenye chumba kimoja ambacho kilifungwa kisasa sana, miale ya umeme ilikuwa inaonekana kila sehemu hakuna sehemu mtu angegusa akachukua hata sekunde tatu akiwa hajafa, hicho kilikuwa chumba cha mkuu wa majeshi huyo, humo ndimo mlikuwa na siri zake nyingi sana na kila kitu chake kilikuwa hapo, aligeuka na kumuangalia mkuu wa gereza hilo kwa macho makali sana akiwa na mwanamke wake pembeni, mkuu huyo wa gereza alijua wazi kwamba huyo mtu alimhitaji yeye na vijana wake watoke hilo eneo hawakuwa wakiruhusiwa kabisa kuingia, aliwapa ishara vijana wake wakatoka na kumuacha mheshimiwa huyo na mwanamke wake, aliweka jicho lake kwenye sehemu moja ya tobo ile miale ya umeme mkali ikapotea hapo alisogea mlangoni na kubonyeza namba kadhaa mlango ukafunguka, waliingia yeye na mwanamke wake huko ndani akawasha skrini zote kwenye hicho chumba ambacho kilikuwa cha thamani sana na mlikuwa na kila kitu.

Skrinin hizo zilikuwa zimeunganishwa na kamera za siri sana humo ndani ambazo hata mkuu wa gereza hakuwa akizijua kabisa kama zipo humo ndani,zilikuwa ni tofauti kabisa na zile za ulinzi za mle ndani, aliziwasha ili aweze kujua mwanaume huyo alitorokaje mle ndani mpaka akafanikiwa kutoka eneo la hatari kama hilo.

Unahisi Zakaria alifanikiwa vipi kutoka humo ndani? Wale wanaume walio tumwa ndani ya ardhi ya Tanzania watafanikiwa kumpata kweli?..........99 niseme inafika mwisho panapo majaaliwa tukutane tena wakati ujao.

Wasalaam

Bux the storyteller.
Tamu sana hii ngoma
 
Back
Top Bottom