FEBIANI BABUYA
JF-Expert Member
- Mar 5, 2022
- 1,916
- 3,850
- Thread starter
- #381
Kaka asante sana. Nimeyapokea ndugu yangu[emoji120]CHUKUA MAUA YAKO MAPEMA BROO THANKS
Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kaka asante sana. Nimeyapokea ndugu yangu[emoji120]CHUKUA MAUA YAKO MAPEMA BROO THANKS
Habari kakaUbarikiwe
Kesho panapo majaaliwa, tunaimaliza yote mpaka mwisho.
Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile aaaiseeee sina neno
Tamka Nash naashNaash naash
Nitamke au niandikeTamka Nash naash
NAASH nashNaash Nash
[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122] congratsqueen Virgo ADK Ihayabuyaga @Am-tunnechi winston20 clement edward @Kb ulayaulaya Analyse Half american Watu 8 Dr Restart Antonnia Kalpana Glenn Shunie Numbisa Clkey
Chizi Maarifa dr namugari wakuu njooni mnipopoe huku
Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
STORY: GEREZA LA HAZWA
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: Bux the storyteller
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
FINAL………………………….
UKURASA WA MIA MOJA KUMI NA TANO
Ilikuwa imepita miaka ishirini sasa tangu lile tukio la Zakaria kumuua mkuu wa majeshi wa nchi ya Libya, juu ya kilele cha mlima maarufu zaidi Afrika, mlima mkubwa na mrefu zaidi ndani ya bara la Afrika, na ndio mlima wa pili kwa ukubwa zaidi duniani kote, mlima huo umeweka historia kubwa ya kupandwa na watu maarufu sana duniani kama mcheza mpira kutoka ndani ya nchi ya Sweden ambaye ndiye mchezaji aliyewahi kufunga magoli ya kutisha zaidi duniani namzungumzia Zlatan Ibrahimovic, sio huyo tu hata kipenzi cha aliyekuwa Malkia na waingereza kwa ujumla David Beckam amewahi kufika hapo najua ushaujua kwamba ni mlima KILIMANJARO Fahari ya watanzania, ambapo pia Alexender aliupandisha mwenge wa uhuru ili uweze kumulika ndani na nje ya mipaka ya nchi ya Tanzania, mlima wa watanzania na Fahari yao KILIMANJARO MOUNTAIN.
Juu ya kilele cha mlima huo ilikuwa inaonekana helikopta moja ya kifahari sana sehemu hiyo iliyokuwa imeandikwa DECAN hizo huwa zinamalikiwa na watu matajiri mno, pembeni umbali mdogo kutoka ilipo helikopta hiyo alikuwa anaonekana kijana mmoja ambaye alikuwa anafanya mazoezi magumu sana mkononi mwake akiwa ana upanga mzito uliokuwa unang’aa sana, huo ndio upanga ambao ulikuwa unamilikiwa na mtaalamu Zakaria leo ulikuwa upo kwenye mikono ya kijana mdogo mwenye umri wa miaka ishirini tu, mwili wake ulikuwa umepasuka sana kwa mazoezi, umbali mdogo na alipokuwa alikuwa amesimama binti ambaye hakuwa chini ya umri wa miaka kumi na misaba alikuwa ni mzuri mno alikuwa anampigia makofi kijana huyo na kufurahia hicho alichokuwa anakifanya, mkono wake wa kulia walikuwa wamekaa watoto watatu mmoja alikuwa kama miaka kumi na mitatu hivi naye alikuwa wa kike na pembeni yake walikaa watoto wawili wa kike na wa kiume walifanana sana bila shaka walikuwa ni mapacha wote walikuwa wakifurahia kile alichokuwa anakifanya yule kijana aliyekuwa anaonekana kama chotara ngozi yake ilikuwa laini ya kuvutia mno kutokana na maisha safi waliyokuwa nayo.
Upande wa nyuma wa hiyo helikopita kulikuwa na sofa moja la gharama mno walikaa watu watatu hapo, alionekana mzee mmoja ambaye kwa makadirio alikuwa na miaka 56 hakuwa amezeeka sana kutokana na mwili wake kukomaa kwa mazoezi makali mno, pembeni yake mkono wa kulia na wa kushoto walikaa na wanawake wawili ambao walikuwa ni wamama lakini pesa ziliwafanya waonekane bado umri wao haukuwa mkubwa sana, mzee huyo alikuwa ameshika kalamu ya wino kwenye mkono wake note book ilikuwa imefunuliwa ukurasa wa mwanzo kabisa akihitaji kuiandika, wanawake hao walikuwa wamemkumbatia wakisubiri aandike hicho alicho hitaji kukiandika.
Anasema mimi naitwa Zakaria Mansour kama wachache walivyokuwa wanikijua mwanzo, wengine walinijua kama Alen huku wengine wachache zaidi wakinijua kwa jina la Aariz, leo nahitaji niiandike historia nzima ya maisha yangu sio kwa sababu ya kuujulisha ulimwengu hapana ila ni kwa ajili ya wake zangu ambao nawapenda sana, leo nina familia kubwa sana ya wake wawili na watoto watano, sisi tunaishi kwa furaha sana hapa duniani ndiyo maana nina kila sababu ya kuwa hai, hiki ninacho kiandika sitaki mwanangu yeyote akijue kabisa watabaki kusimuliwa tu kama watu wengine wanavyo simuliwa labda kama kuna ambaye atakuja kujua kwa bahati mbaya japo habari zangu kwa sasa zimesambaa duniani kote kwamba ni shujaa wa bara la Afrika huenda ni kweli ila sina uhakika sana juu ya hilo.
Wake zangu wamekaa namimi kwa miaka mingi sana ila hawajawahi kabisa kujua historia nzima ya maisha yangu na ndiyo maana nataka niiandike kwa ajili yao leo hii, aliinama na kuufunua ukurasa wa kwanza, kisha akatamka.
“Nitaandika kwa masaa matatu tu pekee kwa sababu ndio muda ambao kichaa wangu huwa anakamilisha mazoezi yake baada ya hapo huwa hahitaji kabisa kukaa mbali namimi kwa sababu anahofia usalama wangu sana na hamuamini mtu yeyote hapa duniani zaidi ya mimi na mama zake hawa wawili, hahahhhahh namuita kichaa wangu kwa sababu huyu namjua mwenyewe ndio maana ule upanga anao yeye kwa sasa ni bora kama ungekutana na mimi kwa wakati ule ungeweza kusalimika ila sio kukutana na huyo kichaa wangu ni mbaya na ni mbaya sana anapokuwa amelishika hilo panga anakasi ya kuua watu mia tano ndani ya dakika kumi na tano tu pekee na akaondoka sehemu bila wasi wasi hiyo ndiyo maana namalizia uzee wangu vizuri kwa sababu sina wasi wasi wa kuilinda familia huyo ndiye mlinzi wa hii familia na ana miaka ishirini tu pekee”
Anaendelea kwa kusema
“Anapendwa sana na dada zake pamoja na mdogo wake wa mwisho wa kuiume ambaye ni pacha kuliko kitu chochote huyo ndiye mtoto wangu wa kwanza nampenda mno naweza kusema nusu ya moyo wangu upo kwake, hilo ndilo jembe langu mimi hahhahaha jina lake anaitwa Kaylan Zakaria Mansour au unaweza kumuita Mansour JR jina la babu yake kabisa aliye nizaa mimi hapa. unaweza ukajiuliza sana kwamba huyu ni mtoto wa nani kwa sababu nina wake wawili kwa sasa ambao mpaka muda huu hata haujawajua kama ni nani na nani?”
“Wake zangu ni wazuri sana tena sana na ni wazuri mno mwanangu wa kwanza ni mtoto wa Josephene nadhani unamkumbuka huyu mrembo wa Tanga ambaye alikuwa anaishi Sinza nilikutanishwa naye na Stephano ambaye kwa sasa ni mkurugenzi wa kampuni kubwa sana Afrika ya usafirishaji, enhe sasa kama umemkumbuka basi ndiye huyu mke wangu wa kwanza yeye amebahatika kupata watoto wa wili wa kwanza kwenye uzao wangu ambaye ndiye huyo kichaa wangu ninaye mpenda sana lakini pia na mtoto wa tatu kwenye uzao wangu huyu anaitwa Caren kwa sasa ana miaka kumi na mitatu kachukua shepu na sura ya mama yake nadhani kaka yake atateseka sana kumlinda huko nje hahahahh, nilivyorudi kutoka Libya rasmi nilienda kwao kujitambulisha wakanikabidhi mke na kwa sasa familia yake nimeibadilisha imekuwa moja kati ya familia za kitajiri mno huko Tanga”
“Lakini mke wangu wa pili najua hata wewe utashtuka ndiyo lakini hakuna namna nampenda sana sana mpole wangu huyu hanaga makuu na mtu maskini, huyu ndiye mtoto au masalia ya Sudi Amadou Mbaye yule adui wangu wa zamani ndiyooooooooo, hii ndiyo familia ambayo mimi nilikuwa na uadui nayo wa kufa na kuuana lakini leo ndiye mke wangu kipenzi huyu ni Aasia ambaye alimuua baba yake mwenyewe kwa mapenzi yake kutokana na kile ambacho mzee huyo alikuwa amemfanyia sitaki kuandika mengi juu yake ya kumuudhi mama watoto wangu asije akajisikia vibaya nikashindwa kula raha mimi. Mrembo huyu amenipatia zawadi ya watoto watatu, nadhani umesikia kwamba kuna binti wa miaka 17 hapa ni mzuri sijawahi kuona mfano wake kwenye nchi hii sasa huyo ndo mwanangu wa kike kwa kwanza na mtoto wangu wa kwanza kutoka kwa Aasia mke wangu mdogo, lakini watoto wake wengine ni wale mapacha wawili wa mwisho wa kike na wa kiume tumekamilika familia ya watu saba japo baba yake mdogo Aami alifanikiwa kuondoka baada ya mimi kumuacha hai na Aasia aligoma kukutana naye hakutaka kukumbuka ya nyuma tena, nipewe nini mimi hapa duniani japo it suddens me when I remember RIP to my family, huwa sipendi sana kukumbuka kilicho nitokea kwa wake zangu wa mwanzo na wanangu kwa sababu kinaniumiza sana kila siku”
“Labda kwa kudokeza tu ngoja nielezee kidogo namna mama Sasha alivyoweza kuikataa familia yake kwa sababu yangu, kiuhalisia yule mwanamke familia yake ilipoteaga kwa kuzama na meli akiwa yeye bado binti mdogo sana ambapo alikuwa anasoma nursery school, baada ya hapo alichukuliwa na tajiri mmoja ambaye alikuwa rafiki wa baba yake na kumlea, huyo ndiyo ilikuwa familia yake kubwa, alimsomesha na kumpatia kila kitu mpaka alipokuja kukutana namimi, mzee huyo hakuwa na mtoto yeyote wa kike hivyo alihitaji kumrithisha nusu ya mali zake lakini alikataa kwa sababu yangu na alikuja kuolewa na mimi huwa namkumbuka sana ninapo yakumbuka haya kwa sababu sijawahi hata kuitafuta familia ile tena yatazuka mengine Rip to my wife, nilikupenda mno wewe na mwanangu Sasha” mzee huyo alipumzika baada ya kuumaliza utangulizi safi sana ambao ungemvutia msomaji, hapo sasa alianza kuiandika historia nzima ya maisha yake, mpaka anafika mwisho hao wanawake karibu yake walikuwa wamelia sana tena sana walimuonea sana huruma mwanaume huyo alikuwa amepitia mambo mengi ya kutisha sana kwnye maisha yake waliamua kumbembeleza sana na kuzitumia vyema siku walizo bakiza duniani kuweza kumpatia furaha yake.
Alitumia masaa mawili na nusu kuandika kila kilicho mtokea kwenye maisha yake ili wanawake hao waujue ukweli ambao kwa muda wote huo hawakuujua, baada ya kumaliza alitabasamu sana na kutamka.
“Kuna maswali ambayo najua wake zangu na hata atakaye kuja kuisoma hadithi hii atakuwa anayo kwenye kichwa chake hahahahah nitawasaidia kuwajibu baadhi ila kama yakinishinda basi huenda mtakuja kuyapata majibu kama mwanangu naye atakuja kuwa na historia yake ya kutisha huko baadae maana hayo ni maisha yake mwenyewe”
“kwanza kutakuwa na watu watakuwa wanajiuliza sana ilikuwaje baada ya mimi kutoka kule Libya na niliwaoaje hawa wanawake wote wawili?”
“Baada ya kutoka kule mwanamke ambaye nilikuwa na uhakika wa kumuoa alikuwa ni Josphene kwa sababu tulikuwa tumetengeneza mahusiano tayari lakini kutokana na upweke ambao alikuwa nao Aasia na mapenzi ya dhati ambayo alikuwa ananionyesha Josephene ndiye aliye nishauri nimuoe Aasia, mara ya kwanza niligoma sana lakini baadae nilikuja kukubali kufanya hivyo. Nashukuru sana MUNGU familia yangu iliwakubali wote nikawaoa wote wawili familia ilikuwa na furaha kubwa sana japo kwa baadae baada ya miaka kumi bibi yangu na babu yangu walikufa kwa maradhi ila namshukuru sana MUNGU ndugu zangu wengine wapo na wana maisha mazuri sana kwa sasa. Stephano nilimsaidia kukamilisha mipango yake na manzese kwa sasa imekuwa kama Mikocheni hahahha, oooh George na Rikardo hawa walikula vitengo vikubwa sana serikalini George kwa sasa ni mkuu wa majeshi wa Tanzania na Rikardo ni mkurugenzi wa usalama wa taifa”
“Raisi Alan Mwaiponela hakugombea tena uraisi baada ya kumpata mwanae wa pekee Mwaiponela Jr kwa sasa amemrudisha na mwanamke ambaye alimkimbia wakati hana maisha baada ya kugundua mwanamke huyo alikuwa amejutia na kujifunza vya kutosha, kwa sasa ni tajiri mkubwa sana wa madini”
“Kuna mtu atataka kujua siri ya ule uwezo wangu wa Kwenda kwa kasi sana kiasi kwamba mtu mwenye macho mazito sana hawezi kuniona? Mjhhhhhhhhh hizo ni siri nzito sana nenda China huko utajifunza au subiri mwanangu kipenzi atakuja kukupatia majibu pale utakapo kuja kumsoma japo kidogo kwa sababu yeye kafundishwa na mimi ila kwa mimi siwezi kufunguka hiyo siri kwa sababu nilikula kiapo mbele ya master wangu kutoka China”
“Muda wangu unanitupa sana mkono ila kuna maswali ya mhimu zaidi ambayo kuna watu watakao kuja kuisoma hadithi hii watakosa majibu nitawapa majibu mafupi sana huenda kwa wakati mwingine tukikutana nitakuja kuelezea zaidi ila kitu ambacho sitaweza kabisa kukisimulia kwenye maisha yangu ni namna nilivyoweza kufanya mauaji kwenye familia ya Amadou Mbaye, niliiua kikatili mno pamoja na wale wanajeshi miamoja, kuhusu hilo sitakuja kufunguka kamwe kwenye maisha yangu maana ule ukatili nadhani ukijulikana hata wanangu wanaweza wakaanza kunikimbia, naanza na kuyajibu maswali ambayo yalikuwa yanakutatiza sana kwenye kichwa chako kama ifuatavyo”
“Wale vijana wangu 12 kwamba niliwafundisha muda gani mpaka wakawa wananiheshimu sana mimi ni kwamba wakati nipo China wao walikuwa wanajeshi wa kawaida tu ulianzishwa mpango wa CONTINUE THE WAR PROCEDURE (CPW) huu mpango ulikuwa ni wa muda mrefu sana ambao uliandaliwa kama ikitokea mimi nikifa basi nafasi yangu itachukuliwa na mmoja wapo ambaye angeiva kuliko wote kwa hao vijana na namna ya kuwapata ilitumika njia kama ambayo waliitumia kunipata mimi hapa, hivyo wao waliletwa kule China kwa siri ili niwe nawafunza kila napo toka kwenye mazoezi yangu kwa sababu walijua mimi nina uwezo mkubwa sana na huo ulikuwa ni mpango wa siri kwa sababu wakuu wa nchi walikuwa wanadai kwamba wanataka kuimarisha usalama wa taifa hviyo vijana wale niliwafunza kwa moyo wote ndio maana walikuwa wakiniheshimu sana lakini bahati mbaya waliishia kuuawa wote”
“Wakati natoka Benghazi kama una kumbu kumbu sawa sawa nilikutana kwa siri sana na mkurugenzi wa usalama wa taifa wa Libya nadhani nilisema kuna siri aliniambia yes, aliniambia ukweli kwamba raisi alikuwa ameuawa na yule ambaye alikuwa madarakani hakuwa raisi alikuwa ni mkuu wa majeshi na alihitaji hiyo siri nibaki nayo mwenyewe ila kwa bahati mbaya sana aliuawa yule mzee nikiwa nimetoka kule”
“Hahahahah kuna swali ambalo najua kila anaye ijua historia yangu analitolea sana macho kwamba niliwezaje kupona ndani ya siku moja baada ya kuokotwa na mzee Razack Hakimu na kuisoma ile document ya majibu, wakati nikiwa kwenye hali mbaya sana niliwekewa kitu kinaitwa “ENERGETIC IMMORTAL VIRUSES” kwa sasa hauwezi kabisa kunielewa kwa sababu hii teknolojia inapatika kwa nchi chache kubwa sana duniani na ni siri kubwa mno, kwa mtu akiwekewa hivyo virusi havipatani kabisa na hewa maana yake hiyo sehemu ambapo vinahifadhiwa huwa inajifunga kwa kujivuta kwa nguvu, hiyo hali inatakiwa kukutokea ukiwa usingizini ukiwa upo macho unaweza kufa kwa maumivu na sikuwekewa hivyo tu ndani yake kuna vitu vingine niliweweka japo hivyo sio virusi hizo ni bakteria ambazo zinaitwa NEURO ZOOLOGY BRAIN CAPACITY RETAIN” hizi huwa zinanisaidia kurudisha kumbukumbu zangu kwa masaa matatu tu kama nilipoteza kumbu kumbu zangu halafu mtu anakipiga kwenye hiyo sehemu na ndicho kilicho tokea wakati nipo jela nikiwa kwenye mapambano kuna mfungwa alinipiga na ngumi nzito sana kwenye ubavu ambapo niliwekwa hivyo vitu na hiyo ilikuwa ni siri yangu mwenyewe hajawahi kuijua siri yoyote ile leo nimeiweka wazi. Lakini sio hivyo tu hivyo virusi kama mtu akipiga na kitu Kizito kwenye ubavu wangu huwa vinaongezeka nguvu ndio maana ilikuwa ukinipiga hilo eneo nabadilika kabisa kwanza nakuwa na hasira sana halafu nakuwa na nguvu za ajabu na ni bora unipige tu ngumi ila pakichomwa na kitu panakuwa wazi hivyo panakuwa panalazimisha kujiziba hapo nakuwa na hasira mara mbili na roho mbaya sana kwa sababu Napata maumivu makali isivyo kawaida nadhani unakumbuka nilicho kifanya kwa wale nakomando wa LIBYAN DEADLY SECRET 10 SPECIALISTS pale Magomeni Mwembe Chai baada ya kubadilika huyo ndo mimi na kupitia virusi hivyo ninakadiriwa kuishi miaka miamoja ndipo nitakufa labda nife kwa ajali au kuuawa ndipo nitakufa chini ya miaka hiyo na wanangu wote ni hivyo hivyo kwa sababu damu ni moja, hiyo ndiyo sababu siku ile baada ya kuisoma document ile nilichukia sana kwa sababu nilitaka kuwa na maisha ya kawaida tu kama wanadamu wengine”
“Kuna wengine wanahitaji kujua Kani alinidhoofisha na spray gani? Hili ni swali rahisi sana acheni uvivu wa kusoma mkaangalie hata movies za kijasusi mbona haya mambo madogo sana hahahahha, na mwingine atataka kujua nilitorokaje hospitali kule Arusha kweli kwa mtu kama mimi? mbona kazi ndogo sana sehemu kama ile ambayo haina hata ulinzi kabis,,,,aaaagr siwezi kujibu swali rahisi hilo labda ukiniuliza madini yako wapi mpaka sasa hapo nitakwambia madini mpaka sasa yapo ndani yana thamani ya trillioni ishirini za kitanzania nitawagawia wanangu kila mtu atafanyia anacho kitaka mwenyewe wamebahatika kuzaliwa kwenye familia ya kitajiri sana tena sana ila furaha yangu kubwa ni kuweza kusaidia wazee, watoto na mama wajane ndani ya Afrika hata kupunguza tatizo kubwa la ajira kwa vijana baada ya kuchukua mali zangu zote kule Libya na kwa sasa hapa ulimwenguni ni binadamu wachache sana ambao wanaweza kusimama mbele yangu na kupiga kelele kwamba wamenizidi pesa”
“Nina dakika saba tu zimebaki mpaka kichaa wangu amalize mazoezi yake ili tuondoke, dakika hizo nazitumia kujibu maswali mawili tu ya mwisho, la kwanza kuna wale watu watatu niliambiwa niwaue na mkuu wa majeshi bila kujua sababu niliwaua wawili uraiani yule mchora tatoo na kiongozi mmoja wa kijeshi ambaye nilisema nimemuua ila nilimuacha aendelee na maisha yake na kumsihi ahame nchi lakini mtu wa tatu nilimuulia gerezani na ndipo baadae nilikuja kugundua hao ndio waliokuwa wanajua siri yake mkuu wa majeshi ya kumuua mheshimiwa raisi, iliniuma sana baada hata ya kugundua kwamba kumbe yule mzee ambaye alinilea mimi ambaye kwangu alikuwa zaidi ya baba alimfunga ndani ya lile gereza na kumuulia mule mule wakati nimepoteza kumbu kumbu, baadae nilikuja kuijua historia nzima ilivyo kuwa”
“Ooooh dakika nne tu zimebaki mbona muda unakimbia sana ngoja nimalizie haraka haraka watu wanajiuliza sana kuhusu hilo swali la pili kwamba niliwezaje kutoroka ndani ya lile gereza na nilikuwa napigana wapi? sitaki hata kukumbuka sana hilo ila ilikuwa ni hivi?”
“Ile siku ambayo mkuu wa majeshi alinivamia ili nimshambulie awajue wale wanaume 20 alio ambiwa wanamlinda kwa siri ndiyo siku ambayo aliwajua na aliwaua wote, baada ya pale mimi nilirejeshwa kule gerezani sasa nilianza kuonyeshwa kila eneo ndipo nilijikuta mpaka mimi naogopa sana, lile gereza lilikuwa kubwa sana tofauti na nilivyokuwa nafikiria kuna sehemu walikuwa wanahifadhia watu wakiwa wanaonekana mifupa tu walikonda mno, watu walikuwa wanachinjwa mle ndani kama kuku mateso ilikuwa ni kila muda, kule hawakupelekwa wafungwa tu bali hata wale ambao walikuwa wapo kinyume na kiongozi yule”
“Pia kwa baadae nilikuja kugundua kwamba kulikuwa na sehemu ambayo kulikuwa na wanaume wa kazi ambao walikuwa wanafanyishwa mazoezi tu sikuelewa wanaandaliwa kwa sababu gani sikuwa na kumbukumbu kwa wakati ule walinitumia watakavyo wao, nilianza kuishi vizuri eneo lile kama nipo nyumbani kesho yake walinipeleka sehemu moja ambayo ilikuwa chini sana kulikuwa na ulingo wa mapambano kwa haraka haraka tu nilielewa kazi yake, ulikuwa umezungukwa na kamera kila sehemu, niliambiwa kesho yake naanza kupigana na moja kati ya wanaume ambao walikuwa wanaandaliwa kule”
“Kweli kesho yake nilianza mapambano sikujua kama walikuwa wanauza video hizo kwa pesa nyingi sana, wao walikuwa wanadai kwamba wanatengeneza movies wakati hayo matukio yalikuwa ya moja kwa moja ili kutoka kwenye ule ukumbi ilikuwa ni lazima uue watu, niliua wapiganaji wengi sana kule ndani mpaka siku moja ambapo kuna mpiganaji alinipiga vibaya sana eneo langu la ubavu nilibadilika ghafla nilimuua kikatili sana, baada ya kumaliza pamano nilipata maumivu makali mno nililala baada ya kuamka nilijikuta nina kumbu kumbu zangu zote ndipo nikakumbuka siri iliyokuwepo hapo, kwa vyovyote nisingeweza kutoka humo ndani hivyo ilinilazimu kuendelea kuigiza kama sina kumbu kumbu kabisa ili niweze kuchora ramani ya jengo hilo lote ili siku moja nije nitoke kwakuwa hicho ndicho nilicho kisomea kwa maisha yangu haikuwa kazi kubwa sana nakumbuka hata baadae walikuja chuo kikuu cha HAVARD na kuniomba nikafundishe nikagoma nilihitaji kuwa na familia yangu”
“Nilikuwa na sample kadhaa za madini nilijitahidi sana kumshawishi mpishi mpaka alikubali hakuna kitu kinashindikana inapokuwepo pesa labda kuununua uhai tu, mpishi alinieleza kwamba inatakiwa nipate kadi ya kutokea kwenye mageti yenye ulinzi,alinielekeza mpaka sehemu ambayo nilitakiwa kuipata na tulipanga kwamba siku natoka ndo nitaichukua kadi hiyo na ndivyo ilikuwa hivyo nilimuua mwanaume aliyekuwa na ile kadi kwa sababu pete zangu nilikuwa nazificha kwenye nguo za ndani hakuna aliyeweza kuziona hizo ndizo nilizitumia kuua watu kirahisi mle ndani siku natoka na hivyo ndivyo nilivyo fanikiwa kutoka siku ile pale shukrani zake yule mpishi wa mle ndani” Alimaliza kuitoa historia yake ndefu sana ambayo ilikuwa ya kusisimua mno na ya kuvutia sana, wake zake walihisi wanangalia ni moja ya movie la kutisha mno sio tu kwa historia hiyo ya kusisimua hata kwa namna alivyokuwa anajua kuisimulia kwa maandishi mkono wake ulikuwa ni hatari sana kalamu ya wino ikiwa katikati ya mkono huo, pia aliikata kiu ya watu watakao kuja kuisoma kwa kuyajibu maswali ambayo yangewatatiza sana kwenye vichwa vyao, aliifunika note book hiyo na kuiweka kalamu mahali pake kisha akaangalia saa yake masaa matatu yalikuwa yamekamilia wake zake walimkumbatia na kumpiga mabusu wakati huo alikuwa anaitwa aligeuka.
“Bosi?” alikuwa ni mwanae mkubwa wa kiume.
“Nimemaliza bosi we can go back home now, nataka baada ya hapa nikasomee masters yangu ya Uhandisi ndani ya nchi hii hii ya Tanzania sitasoma nje kama nilivyosema mwanzo nitailinda hii familia kwa mkono wangu” mwanae wa damu wa kwanza aliongea kwa furaha akikumbatiana na baba yake pamoja na mama zake hata wadogo zake walisogea hilo eneo wakakumbatiana kama familia.
“Hahahahh that’s my boy” alitamka kwa furaha sana mwanadamu wa kutisha sana huyu enzi zake, waliichukua bendera ya taifa la Tanzania wakaiweka juu ya kilele hicho kisha wakarusha mapambo ambayo yalisomeka I LOVE YOU TANZANIA, rubani alikuwa anawasubiri, familia nzima iliingia ndani ya helikopita hiyo ya gharama mno, waliingia wote wakiwa na furaha sana, mke mkubwa wa mzee huyo ndiye ambaye alikuwa na notebook hiyo kwenye mkono wake alikumbuka kwamba mwandishi hakuandika jina la kitabu hicho alifunua kwenye mkoba wake na kuchungulia cha ajabu alishangaa jina liliandikwa kwa herufi kubwa kabisa kwa nje GEREZA LA HAZWA.
Naaam ulikuwa nami kwa wakati wote tangu mwanzo mpaka nafika mwisho, niseme tu asante kwa uvumilivu wako, asante kwa usikivu wako kwa kuwa nami mwanzo mpaka mwisho, sina neno zuri la kukwambia zaidi ya kusema asante sana kwa muda wako ni matumaini yangu umepata burudani ya kutosha lakini pia umepata elimu ya kutosha panapo majaaliwa tutakutana wakati mwingine tena kwa sasa sina la ziada tena nanyanyua kila kilicho changu natoka ndani ya chumba ambacho nilijifungia kwa miezi kadhaa kuiandaa simulizi hii nzuri sana.
Kwa majina naitwa FEBIANI BABUYA lakini wengi wananijua kama Bux the storyteller, niseme tu bye-bye.
Wasalaam
Bux the storytellerView attachment 2645041
Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile a