Gerson Msigwa amelewa madaraka, anadhani kila mwananchi ana kipato kama chake

Gerson Msigwa amelewa madaraka, anadhani kila mwananchi ana kipato kama chake

Yes Msigwa kwa hili nitamtetea.... Ripoti ya worldbank juu ya FinTech inaonyesha kweli Tz ina unafuu wa bando kuliko mataifa mengi ya afrika mashariki na kati. Mfano tu pale UG nakumbuka MB 50 tuliuziwa kwa 500, GB moja iliuzwa elfu 5 na hii unatumia ndani ya saa moja tu!!

Na hili pia linapimwa kwa kutumia bando bila kujiunga pia.... Yaani ukiwasha daya bila kuwa na kifurushi utatumia MB nyingi kwa bei ndogo kuliko nchi nyingine zilizotuzunguka.
Amesema Ulaya. Tupatie nchi ya Ulaya ambayo raia wake wananunua internet kwa USD 10 kwa GB 1. Tuanzie hapo.
 
Ok, kwa sababu wananchi wa Uganda wanakandamizwa kupata mabando kwa bei kubwa na Tanzania ndio iwe hivyo?

Ndio justification ya kuwa na tozo za miamala?
 
Unazungumzia mataifa yaliyo na fursa kwananchi wake

Mataifa ambayo kila wananchi wake Ana allowance MWISHO wa mwezi awe kafanya kazi au hana nilazima kupata mataifa ambayo hata mtoto mdogo ana allowance yake vocha anajinunulia kutoka a na allowance yake kwamwezi

Kweli aliomotwa toka njombe
 
Amesema Ulaya. Tupatie nchi ya Ulaya ambayo raia wake wananunua internet kwa USD 10 kwa GB 1. Tuanzie hapo.
Kama ni Ulaya basi anapotosha maana kwao hyo Dollar 10 ni kma chenji tu ya juisi. Lakini pia kasi ya internet ya kule plus upatikanaji ni mara elfu ya huku so accessibility ni kubwa kuliko huku hasa wireless network imetapakaa sana na kuna baadhi ya maeneo ni bure kabisa.
 
"Kumekuwa na malalamiko ya vifurushi vimepanda, lakini niwaambie sisi ni kati ya nchi 5 Afrika zenye gharama za chini za bando, ziko baadhi ya nchi za Ulaya ambazo gharama zake ni kubwa, ninafahamu iko nchi ambayo unanunua GB 1 kwa Dola 15"- @MsigwaGerson

#MsemajiWaSerikaliPress https://t.co/v8HsgP6tlm
View attachment 1912341
Huyu ni mpuuzi mwingine Kati ya wapuuzi walioko serikalini,sasa hv anajiona na akili nyingi kwa kazi ya kuteuliwa,ajiulize hiyo nafasi ikitangazwa,watu waombe,hata nafasi ya 20 hatafika.
Ajiulize kabla hajafika hapo alikuwa wapi,mwandishi wa kawaida tu,mwenye salary isiyofika hata milion 2.
Alikuwa choka mbaya tu,
 
Ok, kwa sababu wananchi wa Uganda wanakandamizwa kupata mabando kwa bei kubwa na Tanzania ndio iwe hivyo?

Ndio justification ya kuwa na tozo za miamala?
Mimi siungi mkono tozo lakini nachosema ni kwamba watu wanakosea wanapomkejeli kuwa Tz haina Bundle nafuu kuliko nchi zingine hasa jirani!! Ndio nimegusia ripoti ya FinTech na pia experience yangu ya majirani zetu.

Kwahiyo ni kweli tuna unafuu ila sasa hiyo haitoshi kujustify tozo kubwa as you said....
 
Nina rafiki yangu alikuwa South Africa, ananunua GB 1 kwa mwezi, tunaongea kwa whatsup mwanzo mwisho na hata video call. Hapa Bongo ukinunua hiyo GB1 pamoja na mtandao kusua sua, kwa hayo matumizi haimalizi wiki sijui tofauti ya GB ya South Africa na GB ya Tanzania ni ipi? LAKINI muhimu zaidi ni kuwa, uchumu wa South Africa huwezi kabisa kulinganisha na Tanzania.
Nikisikia mtu analinganisha bei ya bidhaa kwa Nchi tofauti tofauti bila kuongelea Nguvu ya Uchumi (purchasing power) ya Nchi husika naona kama kuna kitu anahitaji kuelekezwa
Mkuu unazungumzia GB moja kumaliza wiki wakati hata siku 2 haziishi GB linakata.....
 
unataka kufananisha uchumi wa south africa na tz

Umemuuliza swali mujarab. Wakiwa wanalinganisha na nchi nyingine gharama, walinganishe pia na ukubwa wa uchumi, pato la nchi. Je hizo dola 10 kwa 1GB ni shehemu gani ya pato la mtu. Hawaki kulinganishwa hivo - wanataka selective comparisons!
 
Nina uhakika Ulaya hakuna nchi wanayouziwa GB 1 kwa USD 10. Huu ni uongo. Ulaya wanakaribia kuiingiza huduma ya internet kama mojawapo ya haki za binadamu, kama yalivyo maji na afya. Kuna nchi zimepitisha sheria kuwa serikali itoe angalau GB 1 FREE kwa siku, za ziada ndiyo unalipia.

Nchi nyingi za Ulaya anayoisema Msigwa zina internet ya bure kabisa - free Internet. Kwa cheo chake, Gerson Msigwa hakupaswa kuongea mambo ya jumla jumla bila mifano au utafiti unaoweza kurejewa na kila mtu.
Mpaka mwaka jana 1GB Afrika Kusini ilikua USD 10 Vodacom
Unataka kufananisha uchumi wa south africa na tz
Nina rafiki yangu alikuwa South Africa, ananunua GB 1 kwa mwezi, tunaongea kwa whatsup mwanzo mwisho na hata video call. Hapa Bongo ukinunua hiyo GB1 pamoja na mtandao kusua sua, kwa hayo matumizi haimalizi wiki sijui tofauti ya GB ya South Africa na GB ya Tanzania ni ipi? LAKINI muhimu zaidi ni kuwa, uchumu wa South Africa huwezi kabisa kulinganisha na Tanzania.
Nikisikia mtu analinganisha bei ya bidhaa kwa Nchi tofauti tofauti bila kuongelea Nguvu ya Uchumi (purchasing power) ya Nchi husika naona kama kuna kitu anahitaji kuelekezwa
The average price of 1GB of mobile data in SA is $2.67 (R39)
 
Anapoongelea Ulaya anazingatia Kipato cha mtu?
Je anajua kuwa wengi wa raia wa Tz hawana kipato zaidibya US 1 kwa siku?
Je anajua Per capita income ya Tz ni kiasi gani?
Je anajua kuwa wengi wa Tz wanaishi kwa mlo mmoja?

Kama ni hizi elimu za kuunga unga ana haki hiyo
 
"Kumekuwa na malalamiko ya vifurushi vimepanda, lakini niwaambie sisi ni kati ya nchi 5 Afrika zenye gharama za chini za bando, ziko baadhi ya nchi za Ulaya ambazo gharama zake ni kubwa, ninafahamu iko nchi ambayo unanunua GB 1 kwa Dola 15"- @MsigwaGerson

#MsemajiWaSerikaliPress https://t.co/v8HsgP6tlm
View attachment 1912341
Huyu kijana ni wa kusikitikia tu maana alikotolewa lakini leo anajiona yuko juu ya mnazi.

Wananchi wanamsubiri tu siku moja atadondoka chini na kupasuka na hakuna atakayeguswa na tukio hilo.
 
Viongozi hua hawataki kutatua tatizo badala yake hua wanafananisha tatizo tulilonalo na tatizo la sehemu nyingine kisha kujiona tuna unafuu hivyo tutulie.

Hii ni tabia mbaya iliyoota mizizi.
 
Anapoongelea Ulaya anazingatia Kipato cha mtu?
Je anajua kuwa wengi wa raia wa Tz hawana kipato zaidibya US 1 kwa siku?
Je anajua Per capita income ya Tz ni kiasi gani?
Je anajua kuwa wengi wa Tz wanaishi kwa mlo mmoja?

Kama ni hizi elimu za kuunga unga ana haki hiyo
Hawajui kitu inaitwa compare and contrast.
 
Kama wangekuwa na huruma na wananchi hapo walitakiwa wawe mfano kwa kushusha bei zaidi ili na nchi zinazouza bei kubwa waige kwao,wasiwe nchi ya kuwaiga wenzao tu.
 
Back
Top Bottom