Gerson Msigwa amelewa madaraka, anadhani kila mwananchi ana kipato kama chake

Amesema Ulaya. Tupatie nchi ya Ulaya ambayo raia wake wananunua internet kwa USD 10 kwa GB 1. Tuanzie hapo.
 
Ok, kwa sababu wananchi wa Uganda wanakandamizwa kupata mabando kwa bei kubwa na Tanzania ndio iwe hivyo?

Ndio justification ya kuwa na tozo za miamala?
 
Unazungumzia mataifa yaliyo na fursa kwananchi wake

Mataifa ambayo kila wananchi wake Ana allowance MWISHO wa mwezi awe kafanya kazi au hana nilazima kupata mataifa ambayo hata mtoto mdogo ana allowance yake vocha anajinunulia kutoka a na allowance yake kwamwezi


Kweli aliomotwa toka njombe
 
Amesema Ulaya. Tupatie nchi ya Ulaya ambayo raia wake wananunua internet kwa USD 10 kwa GB 1. Tuanzie hapo.
Kama ni Ulaya basi anapotosha maana kwao hyo Dollar 10 ni kma chenji tu ya juisi. Lakini pia kasi ya internet ya kule plus upatikanaji ni mara elfu ya huku so accessibility ni kubwa kuliko huku hasa wireless network imetapakaa sana na kuna baadhi ya maeneo ni bure kabisa.
 
Huyu ni mpuuzi mwingine Kati ya wapuuzi walioko serikalini,sasa hv anajiona na akili nyingi kwa kazi ya kuteuliwa,ajiulize hiyo nafasi ikitangazwa,watu waombe,hata nafasi ya 20 hatafika.
Ajiulize kabla hajafika hapo alikuwa wapi,mwandishi wa kawaida tu,mwenye salary isiyofika hata milion 2.
Alikuwa choka mbaya tu,
 
Ok, kwa sababu wananchi wa Uganda wanakandamizwa kupata mabando kwa bei kubwa na Tanzania ndio iwe hivyo?

Ndio justification ya kuwa na tozo za miamala?
Mimi siungi mkono tozo lakini nachosema ni kwamba watu wanakosea wanapomkejeli kuwa Tz haina Bundle nafuu kuliko nchi zingine hasa jirani!! Ndio nimegusia ripoti ya FinTech na pia experience yangu ya majirani zetu.

Kwahiyo ni kweli tuna unafuu ila sasa hiyo haitoshi kujustify tozo kubwa as you said....
 
Mkuu unazungumzia GB moja kumaliza wiki wakati hata siku 2 haziishi GB linakata.....
 
unataka kufananisha uchumi wa south africa na tz

Umemuuliza swali mujarab. Wakiwa wanalinganisha na nchi nyingine gharama, walinganishe pia na ukubwa wa uchumi, pato la nchi. Je hizo dola 10 kwa 1GB ni shehemu gani ya pato la mtu. Hawaki kulinganishwa hivo - wanataka selective comparisons!
 
Mpaka mwaka jana 1GB Afrika Kusini ilikua USD 10 Vodacom
Unataka kufananisha uchumi wa south africa na tz
The average price of 1GB of mobile data in SA is $2.67 (R39)
 
Anapoongelea Ulaya anazingatia Kipato cha mtu?
Je anajua kuwa wengi wa raia wa Tz hawana kipato zaidibya US 1 kwa siku?
Je anajua Per capita income ya Tz ni kiasi gani?
Je anajua kuwa wengi wa Tz wanaishi kwa mlo mmoja?

Kama ni hizi elimu za kuunga unga ana haki hiyo
 
Huyu kijana ni wa kusikitikia tu maana alikotolewa lakini leo anajiona yuko juu ya mnazi.

Wananchi wanamsubiri tu siku moja atadondoka chini na kupasuka na hakuna atakayeguswa na tukio hilo.
 
Viongozi hua hawataki kutatua tatizo badala yake hua wanafananisha tatizo tulilonalo na tatizo la sehemu nyingine kisha kujiona tuna unafuu hivyo tutulie.

Hii ni tabia mbaya iliyoota mizizi.
 
Hawajui kitu inaitwa compare and contrast.
 
Kama wangekuwa na huruma na wananchi hapo walitakiwa wawe mfano kwa kushusha bei zaidi ili na nchi zinazouza bei kubwa waige kwao,wasiwe nchi ya kuwaiga wenzao tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…