Gerson Msigwa aniombe radhi hadharani kupitia chombo cha habari alichonichafulia jina na Utu wangu

Duh! Inasikitisha sana kwa kiongozi Kama Msigwa ambaye ni msemaji mkuu wa serikali anaweza nena maneno hayo magumu.

Hata Kama unajua mtu huyo anatenda hivyo ,angepaswa kutumia lugha na njia zingine rafiki kushauri na si kumdhalilisha kiasi hicho!!
Kwahiyo na ww unasapoti ushoger?,nonsense
 
RAIS WANGU SAMIA, MSEMAJI MKUU WA SERIKALI, GERSON MSIGWA ANIOMBE RADHI HADHARANI.

Mheshimiwa Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wangu wa Chama cha Mapinduzi,

Awali ya yote naomba nikupe Pole na hongera kwa majukumu mazito unayoendelea kutufanyia kwa weledi na mafanikio makubwa sisi wananchi wako wa Watanzania tangu uingie Ikulu miezi sita sasa. Kwa majina naitwa Suphian Juma Nkuwi, ni Mtanzania Mzaliwa wa Kijiji cha Minyughe, Wilaya ya Ikungi, mkoa wa Singida.

Rais wangu na Mwenyekiti wangu wa Chama cha Mapinduzi Taifa, kwa kuzingatia Ibara ya 12 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Katiba ya Chama cha Mapinduzi sehemu ya Kwanza, fungu la 4. Imani (1) Binadamu wote ni sawa (2) kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake;

Kwa masikitiko makubwa kupitia barua hii ya wazi napenda kuleta malalamiko yangu mbele ya ofisi yako takatifu kwamba Msaidizi wako, Gerson Msigwa ambaye kwa sasa ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Septemba 18, 2021 akihojiwa na Mtangazaji katika kituo cha habari cha Star TV () alitamka kwamba habari iliyochapishwa ukurasa wa mbele, Aprili 20, 2019 na gazeti la Tanzanite iliyosomeka kwamba "SHOGA AWACHANGANYA ZITTO, MAALIM SEIF" kwamba ILITHIBITISHWA ndio maana gazeti hilo la ndugu Cyprian Musiba halikuwahi kufungiwa na Serikali.

Rais wangu, ndani ya habari hiyo mwathirika aliyetambulishwa kama 'shoga' kwa majina na picha ni mimi. Na kwa hakika haikuwa habari ya kweli kwani natambua mapenzi ya jinsia moja si tu ni kinyume na sheria zetu za Tanzania bali pia maadili na tamaduni zetu haziruhusu. Na mbaya zaidi gazeti hilo linalofahamika nchini kama 'bingwa' wa kuchafua VIONGOZI wa Chama, Serikali, wanasiasa na Wanaharakati halikuwahi kunitafuta kabla ya kutoa habari hiyo ovu kama alivyodai ndugu Msigwa.

Hivyo, kauli hiyo potofu kutoka kwa Kiongozi Mkubwa kabisa wa Serikali yetu si tu imezua tafrani mtandaoni bali pia hadi naandika barua hii kwako imeendelea kunidhalilisha na kuusigina Utu wangu mbele ya familia yangu, ndugu, jamaa na marafiki zangu na kuniharibia taswira yangu na hata majukumu yangu ya kila siku kama Mtanzania na Mwanasiasa mchanga mwenye ndoto ya kuijenga nchi yake kwa wivu mkubwa.

Kwa kuzingatia ofisi yako ni tegemewa kwa kutoa haki, naomba ndugu Msigwa aniombe radhi hadharani kupitia chombo cha habari alichonichafulia jina na Utu wangu hadharani, ili tu si kufuta kashfa hiyo kwangu bali pia kuondoa tafsiri potovu kwamba Ofisi yako tukufu na hata Chama chetu cha Mapinduzi kimempa nafasi nyeti mtu asiye makini na asiyeona aibu kutamka kauli za uwongo mbele ya umma. Vinginevyo, nitaomba ruhusa ya ofisi yako niendelee kutafuta haki yangu kwa njia zingine ikiwemo njia za kisheria.

Aidha, Rais wangu kabla ya kukuandikia barua hii ya wazi, naomba pia kukujulisha kwamba Octoba 1, 2021 nilishawahi kutuma barua ya malalamiko haya kwako dhidi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia barua pepe ya Ofisi ya Rais Ikulu press@ikulu.go.tz ambapo kwa barua hiyo niliambatanisha kopi ya gazeti la Tanzanite lililonichafua na kipande cha video cha ndugu Gerson Msigwa akibariki kashfa hiyo dhalilishi kupitia Star TV. Ingawa sikupatiwa mrejesho wowote wa barua pepe hiyo hadi naandika barua hii ya wazi kwako.

Natanguliza Samahani kwa usumbufu. Na natumaini ombi langu litafanyiwa kazi mapema. Nakutakia kazi njema Rais wangu na Mwenyekiti wangu wa Chama cha Mapinduzi na Mwenyezi Mungu azidi kukutunza.

Raia wako mwema,
Suphian Juma,
Singida, Tanzania
Octoba 7, 2021.
Email: yessuphian@gmail.com
Phone: 0717027973

View attachment 1966980

Hili tangazo ulipie sasa
 
Kumbe sayansi inasema wanaopinga ushoga nao ni mashoga?

"Sometimes people are threatened by gays and lesbians because they are fearing their own impulses, in a sense they 'doth protest too much,'" Ryan told LiveScience. "In addition, it appears that sometimes those who would oppress others have been oppressed themselves, and we can have some compassion for them too, they may be unaccepting of others because they cannot be accepting of themselves."

Umechelewa sana kuchukua hatua,ata hivyo njia uliyoitumia sio njia sahihi vinginevyo uwe na sababu maalamu ingawa itakua ngumu kueleweka maana njia stahiki iko wazi ambayo ni vyombo vyakisheria.Pole sana.
 
Utakuwa na chembechembe za ushoger mbona unamtetea sana na msemaji wa serikali amethibisha hilo
Duuuh😳😳😳

Sitetei tabia hizo mbaya...bali ninashutumu tabia ya hovyo ya kutoheshimiana kwa kuongea HADHARANI kashfa za AIBU NA FEDHEHA.......kwa yeyote afanyaye......

Haya umeshanidhalilisha basi furahisha nafsi yako mkuu....

Peace
 
Kwa kauli ile ya Msemaji wa Serikali ilitosha kuaminisha umma kwamba Zitto, wewe na Marehemu ni mashoga. Nasubiri kanusho kwa Zitto, pia kufungua kesi mahakamani ili kudai fidia kwa udhalilishaji, ikiwa Msemaji atashindwa kuithibitishia mahakama juu ya madai ya ushoga.
Kumtuhumu au kumsingizia mtu ushoga ni jambo kubwa sana. Laweza kumuathiri mtu na utenda kazi wa majukumu yake.
Muda muafaka wa kuwatapisha watu tozo.
 
RAIS WANGU SAMIA, MSEMAJI MKUU WA SERIKALI, GERSON MSIGWA ANIOMBE RADHI HADHARANI.

Mheshimiwa Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wangu wa Chama cha Mapinduzi,

Awali ya yote naomba nikupe Pole na hongera kwa majukumu mazito unayoendelea kutufanyia kwa weledi na mafanikio makubwa sisi wananchi wako wa Watanzania tangu uingie Ikulu miezi sita sasa. Kwa majina naitwa Suphian Juma Nkuwi, ni Mtanzania Mzaliwa wa Kijiji cha Minyughe, Wilaya ya Ikungi, mkoa wa Singida.

Rais wangu na Mwenyekiti wangu wa Chama cha Mapinduzi Taifa, kwa kuzingatia Ibara ya 12 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Katiba ya Chama cha Mapinduzi sehemu ya Kwanza, fungu la 4. Imani (1) Binadamu wote ni sawa (2) kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake;

Kwa masikitiko makubwa kupitia barua hii ya wazi napenda kuleta malalamiko yangu mbele ya ofisi yako takatifu kwamba Msaidizi wako, Gerson Msigwa ambaye kwa sasa ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Septemba 18, 2021 akihojiwa na Mtangazaji katika kituo cha habari cha Star TV () alitamka kwamba habari iliyochapishwa ukurasa wa mbele, Aprili 20, 2019 na gazeti la Tanzanite iliyosomeka kwamba "SHOGA AWACHANGANYA ZITTO, MAALIM SEIF" kwamba ILITHIBITISHWA ndio maana gazeti hilo la ndugu Cyprian Musiba halikuwahi kufungiwa na Serikali.

Rais wangu, ndani ya habari hiyo mwathirika aliyetambulishwa kama 'shoga' kwa majina na picha ni mimi. Na kwa hakika haikuwa habari ya kweli kwani natambua mapenzi ya jinsia moja si tu ni kinyume na sheria zetu za Tanzania bali pia maadili na tamaduni zetu haziruhusu. Na mbaya zaidi gazeti hilo linalofahamika nchini kama 'bingwa' wa kuchafua VIONGOZI wa Chama, Serikali, wanasiasa na Wanaharakati halikuwahi kunitafuta kabla ya kutoa habari hiyo ovu kama alivyodai ndugu Msigwa.

Hivyo, kauli hiyo potofu kutoka kwa Kiongozi Mkubwa kabisa wa Serikali yetu si tu imezua tafrani mtandaoni bali pia hadi naandika barua hii kwako imeendelea kunidhalilisha na kuusigina Utu wangu mbele ya familia yangu, ndugu, jamaa na marafiki zangu na kuniharibia taswira yangu na hata majukumu yangu ya kila siku kama Mtanzania na Mwanasiasa mchanga mwenye ndoto ya kuijenga nchi yake kwa wivu mkubwa.

Kwa kuzingatia ofisi yako ni tegemewa kwa kutoa haki, naomba ndugu Msigwa aniombe radhi hadharani kupitia chombo cha habari alichonichafulia jina na Utu wangu hadharani, ili tu si kufuta kashfa hiyo kwangu bali pia kuondoa tafsiri potovu kwamba Ofisi yako tukufu na hata Chama chetu cha Mapinduzi kimempa nafasi nyeti mtu asiye makini na asiyeona aibu kutamka kauli za uwongo mbele ya umma. Vinginevyo, nitaomba ruhusa ya ofisi yako niendelee kutafuta haki yangu kwa njia zingine ikiwemo njia za kisheria.

Aidha, Rais wangu kabla ya kukuandikia barua hii ya wazi, naomba pia kukujulisha kwamba Octoba 1, 2021 nilishawahi kutuma barua ya malalamiko haya kwako dhidi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia barua pepe ya Ofisi ya Rais Ikulu press@ikulu.go.tz ambapo kwa barua hiyo niliambatanisha kopi ya gazeti la Tanzanite lililonichafua na kipande cha video cha ndugu Gerson Msigwa akibariki kashfa hiyo dhalilishi kupitia Star TV. Ingawa sikupatiwa mrejesho wowote wa barua pepe hiyo hadi naandika barua hii ya wazi kwako.

Natanguliza Samahani kwa usumbufu. Na natumaini ombi langu litafanyiwa kazi mapema. Nakutakia kazi njema Rais wangu na Mwenyekiti wangu wa Chama cha Mapinduzi na Mwenyezi Mungu azidi kukutunza.

Raia wako mwema,
Suphian Juma,
Singida, Tanzania
Octoba 7, 2021.
Email: yessuphian@gmail.com
Phone: 0717027973

View attachment 1966980

I thought you were going straight to Court and press legal charges (Defamation)in-case you're 100% sure that what was said is contrary to...... !!!
 
Kumbe sayansi inasema wanaopinga ushoga nao ni mashoga?

Wanaopinga ushoga wengi ni mashoga wasiokubali uhalisia wa ushoga wao,
Na wale watu wenye akili na uwezo mdogo wa ufahamu.
 
Back
Top Bottom