Gerson Msigwa aniombe radhi hadharani kupitia chombo cha habari alichonichafulia jina na Utu wangu

Gerson Msigwa aniombe radhi hadharani kupitia chombo cha habari alichonichafulia jina na Utu wangu

Nasoma nyundo za watanzania wakikupiga vitu vizito kichwani,ungekaa kimya walianza kusahau wabongo sio wa kuwaambia matatizo yako .
Any way kama ni ya kweli yachukulie sheria sio msamaha tena ,huo ni udhalilishaji mkubwa
 
Ili msamaha uombwe si lazima kuwe na uthibitisho wa kukanusha?

Haya mambo Sufiani ameyaleta humu kwanini?? Alitaka fedheha? Au alitaka promo?
Duuuh😳😳

Haya dada yangu mama D....

Ndg.Suphian analalamika kutuhumiwa hadharani na ametaka kuombwa msamaha hadharani.....

All and all ninaamini hili litakwisha KIUNGWANA NA KIHEKIMA ila lituachie FUNZO kuwa si VYEMA NA HAKUNA AFYA kutuhumiana hadharani mambo ya aibu na machafu....wakati mwingine hata ikiwa ni kweli....kwani YANAYOTUUNGANISHA NI MENGI...MENGI MNO...kuliko yanayotutenganisha......

Binafsi ninaendelea kuheshimu WAHENGA walioturai kuwa si vyema KUNENA KILA TUSIKIALO/TUJUALO NA TUONALO.....

1)Binadamu wote ni sawa

2)Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake
 
Hivi kweli wewe na shati lako zuri namna hiyo kutoka chama dume upakuliwe na viongozi wa chama jike!!!
Baadhi ya watanzania tunapenda sana kunyanyasana KIHISIA....

Hivi Kama hizo tuhuma si kweli basi ni kiasi gani unamtesa MTANZANIA mwenzako na kumuachia athari kubwa za PTSD(Post traumatic stress disorder)?!!!

Duuh kweli "MACHONI KAMA WATU....."

Khaaa 😳😳😳

It's terrible
 
RAIS WANGU SAMIA, MSEMAJI MKUU WA SERIKALI, GERSON MSIGWA ANIOMBE RADHI HADHARANI.

Mheshimiwa Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wangu wa Chama cha Mapinduzi,

Awali ya yote naomba nikupe Pole na hongera kwa majukumu mazito unayoendelea kutufanyia kwa weledi na mafanikio makubwa sisi wananchi wako wa Watanzania tangu uingie Ikulu miezi sita sasa. Kwa majina naitwa Suphian Juma Nkuwi, ni Mtanzania Mzaliwa wa Kijiji cha Minyughe, Wilaya ya Ikungi, mkoa wa Singida.

Rais wangu na Mwenyekiti wangu wa Chama cha Mapinduzi Taifa, kwa kuzingatia Ibara ya 12 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Katiba ya Chama cha Mapinduzi sehemu ya Kwanza, fungu la 4. Imani (1) Binadamu wote ni sawa (2) kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake;

Kwa masikitiko makubwa kupitia barua hii ya wazi napenda kuleta malalamiko yangu mbele ya ofisi yako takatifu kwamba Msaidizi wako, Gerson Msigwa ambaye kwa sasa ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Septemba 18, 2021 akihojiwa na Mtangazaji katika kituo cha habari cha Star TV () alitamka kwamba habari iliyochapishwa ukurasa wa mbele, Aprili 20, 2019 na gazeti la Tanzanite iliyosomeka kwamba "SHOGA AWACHANGANYA ZITTO, MAALIM SEIF" kwamba ILITHIBITISHWA ndio maana gazeti hilo la ndugu Cyprian Musiba halikuwahi kufungiwa na Serikali.

Rais wangu, ndani ya habari hiyo mwathirika aliyetambulishwa kama 'shoga' kwa majina na picha ni mimi. Na kwa hakika haikuwa habari ya kweli kwani natambua mapenzi ya jinsia moja si tu ni kinyume na sheria zetu za Tanzania bali pia maadili na tamaduni zetu haziruhusu. Na mbaya zaidi gazeti hilo linalofahamika nchini kama 'bingwa' wa kuchafua VIONGOZI wa Chama, Serikali, wanasiasa na Wanaharakati halikuwahi kunitafuta kabla ya kutoa habari hiyo ovu kama alivyodai ndugu Msigwa.

Hivyo, kauli hiyo potofu kutoka kwa Kiongozi Mkubwa kabisa wa Serikali yetu si tu imezua tafrani mtandaoni bali pia hadi naandika barua hii kwako imeendelea kunidhalilisha na kuusigina Utu wangu mbele ya familia yangu, ndugu, jamaa na marafiki zangu na kuniharibia taswira yangu na hata majukumu yangu ya kila siku kama Mtanzania na Mwanasiasa mchanga mwenye ndoto ya kuijenga nchi yake kwa wivu mkubwa.

Kwa kuzingatia ofisi yako ni tegemewa kwa kutoa haki, naomba ndugu Msigwa aniombe radhi hadharani kupitia chombo cha habari alichonichafulia jina na Utu wangu hadharani, ili tu si kufuta kashfa hiyo kwangu bali pia kuondoa tafsiri potovu kwamba Ofisi yako tukufu na hata Chama chetu cha Mapinduzi kimempa nafasi nyeti mtu asiye makini na asiyeona aibu kutamka kauli za uwongo mbele ya umma. Vinginevyo, nitaomba ruhusa ya ofisi yako niendelee kutafuta haki yangu kwa njia zingine ikiwemo njia za kisheria.

Aidha, Rais wangu kabla ya kukuandikia barua hii ya wazi, naomba pia kukujulisha kwamba Octoba 1, 2021 nilishawahi kutuma barua ya malalamiko haya kwako dhidi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia barua pepe ya Ofisi ya Rais Ikulu press@ikulu.go.tz ambapo kwa barua hiyo niliambatanisha kopi ya gazeti la Tanzanite lililonichafua na kipande cha video cha ndugu Gerson Msigwa akibariki kashfa hiyo dhalilishi kupitia Star TV. Ingawa sikupatiwa mrejesho wowote wa barua pepe hiyo hadi naandika barua hii ya wazi kwako.

Natanguliza Samahani kwa usumbufu. Na natumaini ombi langu litafanyiwa kazi mapema. Nakutakia kazi njema Rais wangu na Mwenyekiti wangu wa Chama cha Mapinduzi na Mwenyezi Mungu azidi kukutunza.

Raia wako mwema,
Suphian Juma,
Singida, Tanzania
Octoba 7, 2021.
Email: yessuphian@gmail.com
Phone: 0717027

Kama jama mmoja alivyosema hapo juu, ulikuwa wapi muda wote tokea Musiba achapishe hizo habari? Kimantiki, ukimya wako ni tafsiri tosha kuwa kuna ukweli kwenye hizo tuhuma. Hukuchukua hatua yoyote wakati ule unakuja kuibuka leo? Pumbaaf!
 
Ila ushoga Ni laana aisee wasenge sio!!!!

watu wanafumua tu marinda ukiwakenulia[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]

Jina lako linakuponza ila Kama ungekuwa serious ungeenda makamani kuliko kujikomba kwa watawala ambao ndio wateja wakuu [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787].

Ccm inaharibu vijana Sana!!
Mkuu si ulisema hutajihusisha na mambo ya siasa tena?
 
Ila kwa huyo aliye tuhumu haguswi maana ni sawa na kuichokoza ikulu
Kwa kuwa anayeshambuliwa ni UVCCM....naona leo umechagua upande.....🤣

Endelea kuiunga mkono serikali ya CCM katika kila jambo.....

Kidumu Chama Cha Mapinduzi💪
 
Duuuh😳😳

Haya dada yangu mama D....

Ndg.Suphian analalamika kutuhumiwa hadharani na ametaka kuombwa msamaha hadharani.....

All and all ninaamini hili litakwisha KIUNGWANA NA KIHEKIMA ila lituachie FUNZO kuwa si VYEMA NA HAKUNA AFYA kutuhumiana hadharani mambo ya aibu na machafu....wakati mwingine hata ikiwa ni kweli....kwani YANAYOTUUNGANISHA NI MENGI...MENGI MNO...kuliko yanayotutenganisha......

Binafsi ninaendelea kuheshimu WAHENGA walioturai kuwa si vyema KUNENA KILA TUSIKIALO/TUJUALO NA TUONALO.....

1)Binadamu wote ni sawa

2)Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake

Jumbe hili neno lilishakwisha na kupotea maskioni mwa watanzania walio wengi.

Angetumia utaratibu mwingine ila kwa hili ni kwamba amejivisha bango

Tena ukweli ni kwamba waliolisikiaga hili neno ni wachache sanaaaa ila kwa hii promo ya Sufiani yaani atakua anaongoza kwenye chat sasa. Yaani promo imefika kunakotakiwa...

Sasa mhenga mimi najiuliza nia yake haswa kuja kulifufua hili jambo kwa style alitumia ni ili aombwe msamaha? Au ni kutafuta attention ya wadau?
Kwanini hakulalamikaga palepale alipotuhumiwa

Tukiwa wadogo tulifundishwa kwamba mtu akikutukana unatakiwa kwenda kumshtaki kwamba amekutuka, ila kulirudia lile tusi alilokutukana hadharani ni kuwatukana wakubwa zako

Sufiani ameamua kutoa matusi hadharani
 
Duuh 😳😳🤣

Haya dadangu nisalimie wapwa zangu hapo Kigamboni 👍
 
Back
Top Bottom