carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, ameeleza wasiwasi wake kuhusu kupungua kwa ushawishi wa waandishi wa habari kwa wananchi, akitaka kufanyika kwa utafiti kubaini sababu za wananchi kupoteza imani na ufuatiliaji wa vyombo vya habari.
Msigwa amesema hali hiyo inachangia wananchi kuelekeza imani yao katika makundi mengine yasiyo na taaluma wala jukumu rasmi la kuhabarisha umma, akisisitiza kuwa ni muhimu tasnia ya habari kujitathmini na kurejesha heshima na uaminifu wake.
Ametoa kauli hiyo Oktoba 31, 2026, jijini Dodoma, wakati wa Kongamano na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini Tanzania (RUJAT), ambapo amewataka wanahabari kuzingatia weledi, maadili na kutopendelea upande wowote ili kurejesha nafasi yao kama sauti ya wananchi na watetezi wa maslahi ya jamii.
Soma pia : Watanzania wamepunguza imani na vyombo vya habari