This is gaslighting!! Kama hivi ndio mnachukulia ujumla wa Tanzania, mnakosea sana. Nadhani wewe ndio hauko objective (ni rahisi sana kuona kibanzi kwa mwenzio). Ripoti ya CAG inaonesha mradi umegharimu bilioni 3 japo viambatanishi viko vya milioni 500. Swala hili linatatuliwaje na Kamati ya Bunge?? Viambatanishi vinapatikanaje baadae wakati viliombwa na havikuwepo ndipo ikaje ripoti?Watanzania wengi wana mihemko na hawako objective, ndio maana serikali huwa inapuuza na kungojea mijadala ife yenyewe, kubishana nao ni kupoteza muda.
Msigwa ameongea ukweli mtupu, wenye uzoefu na ripoti za CAG wanayajua hayo, huwa zina makosa mengi tu, na ndio maana baadhi ya hoja zake huwa zinafutwa na kufungwa kabisa.
Wanaofanya ukaguzi ni watumishi wa umma wa kawaida tu, tena wengine wameajiriwa juzi juzi hapa hata uzoefu hawana. Watu huwa wanadhani Kichere mwenyewe ndio anakwenda 'site'.
Hatusemi kuwa ripoti yote imejaa makosa, tunachosema ni kuwa watu wawe watulivu utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria ufuatwe, wenye makosa watachukuliwa hatua na wale wasio na makosa hoja zao zitafutwa.
Kwa hisia kali za watanzania ni bora Msigwa angekaa kimya, sometimes it doesn't matter if you are correct.
Nadhani kilicho sahihi kusema kuhusu waTanzania ni ulichoandika ............." wawe watulivu, utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria ufuatwe ..........." Ni utulivu wa waTanzania ndio umechukuliwa kwa mzaa na watawala!! Subra ya kiwango cha juu sana ndio udhaifu wa waTanzania. Sheria unazozisema ni zile zinazoficha aibu, udhalimu, dhuluma, wizi na mambo mengine!! CPA holder aliyechunguza bajeti na matumizi kama taaluma zinavotaka, anakuja kuhojiwa na mbunge asiye na taaluma na mwenye nia ya kukifutia "chama na serikali aibu" ndio anakuja kuamua hoja zifungwe. Kama tungekuwa ni watu huru, ubadhirifu wote ungepelekwa mahakamani na huko mbivu na mbichi zingejulikana.
Hawa waTanzania unaowananga leo, wametengenezwa na mifumo na sheria zilizotungwa na wabadhirifu!! Ingefaa utoe takwimu za kesi ambazo zimethibitishwa kuwa si za kweli. La sivyo tukubali kuwa utaratibu wa wadhalimu ni kufanya ukaguzi kila mwaka na kutoa taarifa ambayo haitafayiwa kazi. Kila mwaka tunasikia hasara na ubadhirifu wa matrilioni ya pesa sasa!! Hatusikii kesi isipokuwa ya Mramba na Yona miaka zaidi ya 15 iliyopita!!!