Unadhani wanakaa kwenye taasisi moja kwa muda gani? CAG hana workforce ya kukagua taasisi zote kwa pamoja, wanatumia muda mfupi sana kwenye kila eneo.
Mbali na hapo watumishi wa ofisi ya CAG wanaweza kuwa na changamoto za uelewa wa baadhi ya mambo, jambo ambalo ni kawaida kwa watumishi wote serikali, wao sio malaika. Kuna vitu wanaibua kama dosari ambavyo sio dosari.
Hata wakipewa maelezo na vielelezo haisaidii, ndio maana kwa mujibu wa sheria ripoti ya CAG ni 'input' kule bungeni, sio final.
Lazima kamati za bunge zipitie kwa umakini hoja zote, na wakihitaji maelezo zaidi pande zote mbili zinaitwa, upande CAG na taasisi husika.
Mara nyingi tu CAG mwenyewe anaridhia baadhi ya hoja zifutwe baada ya wote kukalishwa na kamati ya bunge.
CAG ni kama mwendesha mashtaka, kushtakiwa haimaanishi una hatia. Bunge ndio mahakama, na taasisi zenye kasoro ni watuhumiwa.
It's basic stuff, but somehow people don't get it. Ndio maana nasema watanzania wengi ni wajinga.