Gerson Msigwa: Huwezi kukurupuka kumfukuza mtu, pengine hata wakaguzi wa CAG nao ukaguzi wao una dosari

Gerson Msigwa: Huwezi kukurupuka kumfukuza mtu, pengine hata wakaguzi wa CAG nao ukaguzi wao una dosari

Some sheria ya ukaguzi wa umma kuanzia kifungu cha 37 mpaka 40, utaona kuwa ripoti hiyo ni kwa ajili ya Bunge kufanyia kazi, Bunge ndio linatoa mapendekezo serikalini ya hatua gani zichukuliwe.

Lakini pia, kama sehemu kuna wizi unaofanyika, haijalishi kama CAG amendika au la, vyombo husika kama PCCB wanapaswa kuchukua hatua. Kwani yote ambayo PCCB wanafanya CAG huwa anayaona?
- lete hivyo vifungu, screenshot tuvione tusome
-Pccb wanafanya Kazi nyingi sana, hadi hizo za Wezi wa Ripoti ya CAG pia ni Sehemu ya Kazi zake
 
Kwani wewe ni lini uliona watumishi wenzako wamechukuliwa hatua kutokana na ripoti ya CAG!
Acha usanii,hiyo ofisi ya CAG si ndiyo huwa inapewa kazi mpaka na taasisi za kimataifa kufanya ukaguzi?sasa leo unatuambiaje kuwa ripoti imekosewa?mbona kimataifa ofisi ya CAG inasifiwa kwa kazi nzuri!
Nimewahi kushuhudia watumishi (sio wenzangu BTW) wakichukuliwa hatua hata kabla ya CAG kukagua.

Lakini pia hata baada ya kufuatia ukaguzi wa CAG.

Kuwa mtulivu utaona Ma DED wangapi wanakwenda ma maji.
 
Msemaji wa Serikali ya Tanzania, Gerson Msigwa amesema kwamba ni vema Wadau wakavuta subira badala ya kutaka kila aliyetajwa kwenye ripoti ya CAG achukuliwe hatua, yapo maeneo ambayo ni lazima yapitiwe upya ili kujiridhisha na kila lililotajwa.

Amedai kwamba unaweza kumchukulia mtu hatua kumbe hana makosa na pengine ripoti ya CAG ndio iliyokosewa.

Toa Maoni yako.
Kwahiyo anabishana na Bosi wake Hangaya?
 
Mh Jakaya Kikwete wakati huo akiwa foreign minister aliwahi kuwaeleza BBC kuhusu ufisadi ulioibuliwa na CAG ktk ubalozi wa Italy kuwa "kazi ya auditor ni kuibua hoja na kazi ya serikali ni kuzijibu". Sasa kusema wanaotajwa na ripoti ya CAG tayari wanastahili adhabu ni ku-miss the point. Ndio maana kuna kamati za mahesabu za bunge. Na kama tayari kama waliotajwa tayari ni wahalifu kusingekuwa na haja ya kujadili ripoti hiyo bungeni. Umewahi kusikia bunge likijadili hukumu iliyotolewa na mahakams?
Upotevu wa fedha na Mali za watu binafsi huku mtaani tunauita wizi..na ujibiwa mahakamani,kumbe serikalini mnauita hoja na mnaujibu kwenye media... ahsante Kwa elimu hiyo.
 
Msemaji wa Serikali ya Tanzania, Gerson Msigwa amesema kwamba ni vema Wadau wakavuta subira badala ya kutaka kila aliyetajwa kwenye ripoti ya CAG achukuliwe hatua, yapo maeneo ambayo ni lazima yapitiwe upya ili kujiridhisha na kila lililotajwa.

Amedai kwamba unaweza kumchukulia mtu hatua kumbe hana makosa na pengine ripoti ya CAG ndio iliyokosewa.

Toa Maoni yako.

Msigwa anachanganyikiwa sasa.
 
- lete hivyo vifungu, screenshot tuvione tusome
-Pccb wanafanya Kazi nyingi sana, hadi hizo za Wezi wa Ripoti ya CAG pia ni Sehemu ya Kazi zake
Ni kweli, tena wala hawahitaji kungojea ripoti ya CAG. wako huru kunusa na kuchunguza ufisadi na rushwa sehemu yoyote.

Sasa jiulize swali rahisi, nini tofauti ya uchunguzi wa PCCB na ukaguzi wa CAG?
 
- lete hivyo vifungu, screenshot tuvione tusome
-Pccb wanafanya Kazi nyingi sana, hadi hizo za Wezi wa Ripoti ya CAG pia ni Sehemu ya Kazi zake
Labda wakwapuzi wa mboga hizi rushwa ndogo ndogo.
Ukikamatwa na rushwa unatoa rushwa mambo yanaisha
 
Unadhani wanakaa kwenye taasisi moja kwa muda gani? CAG hana workforce ya kukagua taasisi zote kwa pamoja, wanatumia muda mfupi sana kwenye kila eneo.

Mbali na hapo watumishi wa ofisi ya CAG wanaweza kuwa na changamoto za uelewa wa baadhi ya mambo, jambo ambalo ni kawaida kwa watumishi wote serikali, wao sio malaika. Kuna vitu wanaibua kama dosari ambavyo sio dosari.

Hata wakipewa maelezo na vielelezo haisaidii, ndio maana kwa mujibu wa sheria ripoti ya CAG ni 'input' kule bungeni, sio final.

Lazima kamati za bunge zipitie kwa umakini hoja zote, na wakihitaji maelezo zaidi pande zote mbili zinaitwa, upande CAG na taasisi husika.

Mara nyingi tu CAG mwenyewe anaridhia baadhi ya hoja zifutwe baada ya wote kukalishwa na kamati ya bunge.

CAG ni kama mwendesha mashtaka, kushtakiwa haimaanishi una hatia. Bunge ndio mahakama, na taasisi zenye kasoro ni watuhumiwa.

It's basic stuff, but somehow people don't get it. Ndio maana nasema watanzania wengi ni wajinga.
Mkuu acha kutupanga,huoni aibu? Kwaiyo umu jukwaani wewe peke yako ndiyo una uelewa mpana wa ripoti za CAG,na sisi wengine hatujui kitu.
CAG anafuata sheria na kanuni za kazi yake zinavyomuongoza;sasa anakoseaje?
Kwani mpaka anatoa ripoti si Kuna muda maalumu ambao taasisi tajwa zenye dosari zinapewa muda wa kujibu hoja za CAG!!
 
Sio mimi tu mkuu, wengi wanaelewa ila wanatumia busara kukaa kimya. Inawezekana mimi mzalendo uchwara nimepungukiwa hekima.

It's unwise kubishana na wengi, ndio maana hata Spika aliufyata baada ya kelele kuzidi. Alikuwa sahihi lakini ukiona wengi wanasema hivi basi ni bora ukae kimya ungojee lipite.

Ndio maana nikasema Msigwa angekaa kimya tu, being correct is not always enough. No wonder serikali huwa inazuga na kungojea watu wasahau..
 
Nilipokaa muda huu Niko na DED aliyetajwa na CAG kuwa ni mwizi ana warembo wanne wanakula bata haijawahi kutokea. Ikitoka 10,000 ya bia moja hataki chenchi. Ana wapambe kama wote japo yeye amelala tu kwenye kiti udenda unamtoka.
Duuuh hii hatarii kwa kweli.
 
Ni kweli, tena wala hawahitaji kungojea ripoti ya CAG. wako huru kunusa na kuchunguza ufisadi na rushwa sehemu yoyote.

Sasa jiulize swali rahisi, nini tofauti ya uchunguzi wa PCCB na ukaguzi wa CAG?
- Pccb kazi Yao ni kuangalia Kama kuna jinai inayohusisha Rushwa, matumizi mabaya ya Ofisi nk, na kuangalia Kama kuna kosa la jinai lililo chini ya sheria Yao ya pcca
 
Msemaji wa Serikali ya Tanzania, Gerson Msigwa amesema kwamba ni vema Wadau wakavuta subira badala ya kutaka kila aliyetajwa kwenye ripoti ya CAG achukuliwe hatua, yapo maeneo ambayo ni lazima yapitiwe upya ili kujiridhisha na kila lililotajwa.

Amedai kwamba unaweza kumchukulia mtu hatua kumbe hana makosa na pengine ripoti ya CAG ndio iliyokosewa.

Toa Maoni yako.
Msigwa ni watu wa wapi? Hili nalo boga lipo tu.
 
Back
Top Bottom