Watanzania wengi wana mihemko na ni wajinga, ndio maana serikali huwa inapuuza na kungojea mijadala ife yenyewe, kubishana nao ni kupoteza muda.
Msigwa ameongea ukweli mtupu, wenye uzoefu na ripoti za CAG wanayajua hayo, huwa zina makosa mengi tu, na ndio maana baadhi ya hoja zake huwa zinafutwa na kufungwa kabisa.
Wanaofanya ukaguzi ni watumishi wa umma wa kawaida tu, tena wengine wameajiriwa juzi juzi hapa hata uzoefu hawana. Watu huwa wanadhani Kichere mwenyewe ndio anakwenda 'site'.
Hatusemi kuwa ripoti yote imejaa makosa, tunachosema ni kuwa watu wawe watulivu utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria ufuatwe, wenye makosa watachukuliwa hatua na wale wasio na makosa hoja zao zitafutwa.
Kwa umbumbumbu wa watanzania ni bora Msigwa angekaa kimya, sometimes it doesn't matter if you are correct.