Mzalendo Uchwara
JF-Expert Member
- Jan 26, 2020
- 4,437
- 13,836
Hapana sijasema hivyo, ofisi ya CAG ni muhimu mno, yeye ndio jicho la bunge. Ninachokisema ni watu waelewe kazi ya CAG, ni jicho la bunge na sio kwamba yeye ndio Bunge.Kwa maelezo yako ni kwamba Hakuna haja ya kuwa na CAG. Mbona tutaibiwa mpaka tukome.
Huwezi kutumia ripoti ya CAG kuhukumu watu hapohapo, watu hawatatotendewa haki. Na uzoefu wa miaka ya nyuma unaonesha kuna baadhi ya hoja huwa zinakuwa hazina uzito wa kuitwa 'upigaji', zinafutwa na CAG anaridhia zifutwe kule bungeni.
Pia kuna hoja ambazo zinaibua wizi wa kweli, na huwa zinafuatiliwa vuzuri sana, tena mwaka unaofuata CAG huwa anaanza na hizo kuhakikisha kuwa tatizo halijajirudia.
Kinachotakiwa ni utaratibu kamili ufuatwe, Spika alijaribu kueleza hilo lakini watu wakawa moto kwelikweli, akatumia busara kukaa kimya, japo alikuwa sahihi.
Imagine kama ungekuwa ukikamatwa na polisi unaambiwa toa maelezo, maelezo yako yasipo waridhisha basi unahukimiwa hapohapo na polisi haohao! Unadhani haki inatendeka kwa utaratibu huo?
Likewise CAG anaona mapungufu, anaomba ufafanuzi kutoka kwa wahusika, asiporidhishwa na ufafanuzi anaandika kuwa ameona kasoro moja mbili tatu. Sasa kitendo cha CAG kuandika sio hukumu, ni tuhuma.