Gerson Msigwa: Huwezi kukurupuka kumfukuza mtu, pengine hata wakaguzi wa CAG nao ukaguzi wao una dosari

This is gaslighting!! Kama hivi ndio mnachukulia ujumla wa Tanzania, mnakosea sana. Nadhani wewe ndio hauko objective (ni rahisi sana kuona kibanzi kwa mwenzio). Ripoti ya CAG inaonesha mradi umegharimu bilioni 3 japo viambatanishi viko vya milioni 500. Swala hili linatatuliwaje na Kamati ya Bunge?? Viambatanishi vinapatikanaje baadae wakati viliombwa na havikuwepo ndipo ikaje ripoti?

Nadhani kilicho sahihi kusema kuhusu waTanzania ni ulichoandika ............." wawe watulivu, utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria ufuatwe ..........." Ni utulivu wa waTanzania ndio umechukuliwa kwa mzaa na watawala!! Subra ya kiwango cha juu sana ndio udhaifu wa waTanzania. Sheria unazozisema ni zile zinazoficha aibu, udhalimu, dhuluma, wizi na mambo mengine!! CPA holder aliyechunguza bajeti na matumizi kama taaluma zinavotaka, anakuja kuhojiwa na mbunge asiye na taaluma na mwenye nia ya kukifutia "chama na serikali aibu" ndio anakuja kuamua hoja zifungwe. Kama tungekuwa ni watu huru, ubadhirifu wote ungepelekwa mahakamani na huko mbivu na mbichi zingejulikana.

Hawa waTanzania unaowananga leo, wametengenezwa na mifumo na sheria zilizotungwa na wabadhirifu!! Ingefaa utoe takwimu za kesi ambazo zimethibitishwa kuwa si za kweli. La sivyo tukubali kuwa utaratibu wa wadhalimu ni kufanya ukaguzi kila mwaka na kutoa taarifa ambayo haitafayiwa kazi. Kila mwaka tunasikia hasara na ubadhirifu wa matrilioni ya pesa sasa!! Hatusikii kesi isipokuwa ya Mramba na Yona miaka zaidi ya 15 iliyopita!!!
 
Sawa tufanye ina makosa. Wewe miradi ya serikali inavyopigwa hela unataka kutuambia hizo hela huwa zinakwenda wapi?!
 
Nawe ni mmojawapo watetea upigaji au mpigaji mwenyewe! Kwa hivyo mnataka mbadala wa CAG apite ten kote alikopita CAG kuhakikisha ukweli? Ujinga mtupi! Kama mtu katuhumiwa ni mtuhumiwa, apelekwe mahakamani uchunguzi wa mahakama utasema! Atoe vidhibitisho vya kupinga, hapo ndo tutajua CAG kakosea (which I doubt maana CAG hakurupuki)! Uchawa nao taabu sana!
 
Nani awapeleke mahakamani, CAG? au DPP au PCCB? kwa ushahidi wa ripoti ya CAG? katika historia ya Tanzania ilishawahi kusikia kesi imeenda mahakamani na ushahidi ni ripoti ya CAG??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…