Gerson Msigwa: Kabla ya 2030 tutanunua ndege nyingine 40

Gerson Msigwa: Kabla ya 2030 tutanunua ndege nyingine 40

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Akizungumza jijini Mwanza jana Jumanne, Juni 2, 2026, wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wanamawasiliano wa Serikali, Gerson Msigwa amefichua kuwa kuanzia Julai 1, 2026, Tanzania itaanza rasmi kutekeleza Dira Mpya ya Taifa ya Maendeleo ya 2050 inayolenga kukuza uchumi wa nchi kutoka dola bilioni 95 za sasa hadi kufikia dola trilioni moja ya Kimarekani.

Zaidi: Gerson Msigwa: Mwaka huu Serikali itanunua ndege 4 aina ya Bombadier Q400

Msigwa ameeleza kuwa uwekezaji mkubwa unafanywa na serikali ya awamu ya sita katika sekta ikiwamo sekta ya usafirishaji akibainisha kuwa serikali ina mpango kabla ya mwaka 2030 kuongeza ndege zingine 40 ili kuleta mageuzi makubwa ya kibiashara.

 
Hao abiria wa kupanda hizo ndege watatoka wapi?

Au zitageuzwa daladala zitembee kwenye lami!

Hawa jamaa vichwa vyao sijui vina wadudu gani kwakweli.
 
Wazilete Tu, zinapendeza sana zikiwa zimejipanga pale Airport, mana hata tukisema zinatia hasara Taifa hamtusikilizi, leteni ziwe mapambo, zingine mubebee chawa kwenda kushangilia Moira.
 
Hi nchi ina wajinga wengi sana.ndge kila mwaka ni hasara ya mabilion bdo unaendelea kununua.ilipaswa kuuza zilizokuwepo tuweke lami nchi nzma na tuboreshe sekta ya afya na elimu.
 
Shule hazina madawati, vitabu, maabara, library, na walimu wachache
Hospital hazina madawa ya kutosha na vifaa vyake
Tuna uhaba wa madaktari na manesi
Barabara nyingi hazina lami na zenye lami ni mashimo ya kutosha.
Nchi kama hii unawaza ndege ambazo CAG anasema zimeingiza hasara kubwa kila mwaka!?
Nchi yangu Tanzania🥲
 
Nadhani mambo ya ufanisi si kitu - ili mradi tuwashinde majirani zetu kwa idadi ya ndege.
 
Mwanza airport yenyewe imeshindikana hizo ndege bila viwanja vya kutosha ni kazi bure
 
Back
Top Bottom