Gerson Msigwa: Kilichotokea jana kwenye umeme ni changamoto za kawaida na zinatokea kokote duniani

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
1,170
Reaction score
3,743
Serikali, kupitia Msemaji wake Gerson Msigwa, imetoa ufafanuzi wa kiufundi kuhusu changamoto ya kukatika kwa umeme nchi nzima iliyotokea jana na jinsi ilivyoathiri huduma za treni ya kisasa (SGR)

"Najua wengi mmetikiswa na tatizo lililojitokeza jana. Tulipata hitilafu kwenye gridi ya taifa. Mitambo yetu kule kwa sababu imefungwa mifumo ya kidijitali, iliona kuna matatizo kwenye matumizi.

Ni kama wewe kule nyumbani kwako, ukiwasha umeme ukazimika kwa sababu circuit breaker imekatika. Imekata kwa sababu kuna hatari ilikuwa inakuja kuathiri nyumba yako. Kwa hiyo na mitambo yetu kule imewekewa mifumo ya kujilinda.

Kwa hiyo kilichotokea jana, kulitokea changamoto kwenye matumizi ya umeme. Mitambo kule ikajizima. Ilipojizima, ikabidi TANESCO, mafundi watafute tatizo liko wapi; wamelipata, wamelitatua, na majira kama ya saa sita za usiku nchi nzima ilirudi katika upatikanaji wa umeme"

Kuhusu huduma za SGR kusimama kutokana na umeme kukatika amesema:

"Halikadhalika, baadhi ya huduma muhimu ambazo zilipata shida, mojawapo ni usafiri wa SGR. Baada ya umeme kurudi, treni zimefanya kazi, abiria wamesafirishwa, na tunarudi kwenye ratiba yetu ya kama kawaida.

Hizi ni changamoto za kawaida, zinatokea mahali popote duniani. Maana kuna mtu anaweza akasimama hapa akasema kama vile Tanzania peke yake ndio kuna changamoto za namna hii. Zinatokea kokote duniani. Nashindwa tu kutaja nchi.

Lakini mimi nina ushahidi, sio wa kuambiwa wala wa kusoma, wa mimi mwenyewe. Nchi imeendelea, iko juu kiuchumi, kunatokea changamoto, vitu vinabadilika. Ratiba za treni zitabadilishwa, ratiba za ndege zitabadilishwa, umeme unakatika na kurudi"
 
Hii tabia ya kupenda kufananisha matatizo yetu na ya watu wengine haijakaa sawa.

Tuweke bidii kujifananisha kwenye mambo yenye tija.
 
well done,

unafanya kazi nzuri sana G.Msigwa 👊
 
Masikini

Masikini nchi yangu Tanganyika
 
Atutajie nchi ambayo tatizo kama ilo lilitokea na viongoz wao wakasema nikawaida tu
 
Hata maandamano ni changamoto ya kawaida hutokea nchi yoyote ni jambo la kawaida acheni kupanic😆
 
Kwanini afananishe matatizo na nchi zingine?

Ila linapofika suala la haki za binadamu, maandamano , uchsguzi huru na wa haki wanasema wao ni nchi huru isingalinshwe na wengine inajipangia mambo yake.
Na huu ndio ukweli wenyewe kabisa.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Hitilafu tu, press...
Je tukipigwa bom moja kama Iran, sindio tutakaa gizani hadi milele...🤔
20260604_185414.jpg
 
Ccm wanaiga kila kitu kibaya toka nchi nyingine na wanajitetea kwa sababu kwa wengine vinatokea basi na kwetu vinapaswa kutokea. So sad
 
Hichi ndiyo kichaka wakipendacho ccm cha kukwepa uwajibikaji kwa kujilinganisha na wengine hata kama wanadanganya

Uwajibikaji kwao ni msamiati ambao haupo

Poor ccm
 
Back
Top Bottom