Gerson Msigwa: Kinachoendelea mitandaoni kuhusu "No Reforms, No Election" ni UPUUZI

Gerson Msigwa: Kinachoendelea mitandaoni kuhusu "No Reforms, No Election" ni UPUUZI

FB_IMG_1749286477359.jpg
 
Wana jamii forums hash tag ya No reforms no election imetibua Hali ya hewa wanufaika wa keki ya Taifa wameanza kutoa milio eti ni upuuzi,kanyagieni hapo hapo,Kila comment ya machawa tia Neno no reforms no election,twende sasa.
Screenshot_2025-06-07-19-15-42-873_com.instagram.android.jpg
 
Wana jamii forums hash tag ya No reforms no election imetibua Hali ya hewa wanufaika wa keki ya Taifa wameanza kutoa milio eti ni upuuzi,kanyagieni hapo hapo,Kila comment ya machawa tia Neno no reforms no election,twende sasa.
Uchaguzi upo hata bila reforms
 
The message is loud and clear: NO REFORM, NO ELECTION...; whether it is "upuuzi" to some or not!

The good news, the message is delivered effectively everywhere!
 
Kura watapiga wao na familia zao..lakini huku mitaani raia washasanuka..na ongezeko la hizi simu za mkopo mpk vijijini wanajua kinachoendelea..hakuna haja ya uchaguzi,ikiwa wanajua kabisa Kuna mbinu chafu ..waapishane tu maisha yaendelee
 
Hata chadema ikiingia unategemea hakutakua na viongozi walafi! Kwanza wafuasi wenu wengi ni wakristo, na asilimia kubwa ya Tanzania ni waislamu, na wanaoipigia kura ccm wengi ni waislamu, na wengi pia ni wakristo, japo ccm wana madhaifu yao, but kikubwa amani.
Hizi dini huwa zinawafanya muwe wajinga wajinga.
 
Wenzenu wanatekwa nyinyi mnajisifu kupigana nyuma ya Keyboard !

Kama mmnajiamini tokeni front , hata mwanamama anaweza kutype Ni reforms ni Election akiwa anachambua mchele.
 
Damu ya mzee Kibao na wenzake haitaenda Bure ..hii nchi ni yetu sote..Mungu anasikia kilio cha wenye haki..endeleeni kupora uchaguzi!
 
Wana masikio wala hawasikii, wana macho lakini hawaoni. Ndo walipofikia viongozi wa TZ
CCM wanaongoza nchi kwa kutumia mfumo wa unyumbu wa kisiasa

Unyumbu wa kisiasa ni mfumo unao wezesha wanaopewa dhamana kuahirisha kufikiri kwa nafsi kwasababu ya kulitumia kundi fulani kwa masilahi binafsi na hufanya hivyo, kwa kujipendekeza ama kwa uoga wa kuigiza kwa viongozi wao, (unafiki), a.k.a kujizima data kwassa uchawa tuseme kuahirisha kufikiri kizalendo

Kunyamaza siyo amani bali ni kusalimu amri kwa majukumu ya kijamii ama kitaifa


Silence surrenders public responsibilities
 
View attachment 3359827
DAR. Kufuatia wimbi la wananchi kujibu posti za viongozi wa Serikali na watu maarufu kwa kampeni ya No Reforms No Election inayotumiwa na CHADEMA, Msemaji mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema ni upuuzi akiwataka wajiepushe na kampeni zisizo na tija.

No Reforms No Election ni kampeni iliyoanzishwa na inayotangazwa kwenye mikutano ya CHADEMA wakitaka kuwepo mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi kabla ya kufika siku ya kupiga kura Oktoba 2025.

Katika mitandao ya kijamii makundi mbalimbali yanahamasisha kupaza sauti za kampeni hiyo kwa kuchapisha ujumbe na kutoa maoni ya No Reforms, No Election pale ukurasa fulani unapokuwa umechapisha maudhui yake yoyote.

Haijalishi ni ukurasa wa nani, iwe wa vyombo vya habari, kampuni, matangazo sehemu kubwa ya maoni ni No Reforms, No Election na wengine wanafupisha kwa kuandika NRNE.

Hali hiyo imewalazimu baadhi ya viongozi kuzima sehemu ya maoni ili kujiepusha na kampeni

Kauli ya Serikali
Alipoulizwa na tovuti ya Mwananchi Communications Ltd kuhusu hatua hiyo, Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amejibu "Watu wameamua kufanya hivyo, tutafanyaje," amesema.

Ingawa katika maelezo yake aliwatahadharisha wanaofanya mchezo huo akidai hauna tija na 'upuuzi' zaidi ya kupoteza muda wao.

"Watu wajiepushe na kampeni zisizokuwa na tija, watumie mitandao kama fursa ya kujifunza teknolojia mpya, wanapaswa kutambua na kujua kutumia mitandao vibaya ni kupoteza rasilimali fedha kwa kuwa wanatumia bando," amesema.

Katika maelezo yake Msigwa amesema badala ya kupoteza muda kuendesha kampeni hizo watumie nafasi hiyo wajielekeze kujenga nchi yao.

"Kinachoendelea kwenye mitandao ni upuuzi. Huu ni upuuzi unaoendelea Watanzania wajielekeze kujenga nchi yao. Huwezi kuendesha kampeni ya kuzuia Uchaguzi wakati nchi imejiwekea kalenda yake," amesema Msigwa.

Kampeni hiyo imeenda mbali zaidi kwa kumgusa hadi msanii wa Nigeria Chellaboi ambaye amekuja nchini hivi karibuni na kushangazwa na ukurasa wake kumiminika maoni yanayohusu kampeni hiyo.

Chanzo: Mwananchi
Gaddafi alianza kutukana raia wake hivihivi akaja kuokotwa kwenye mtaro
 
Wana jamii forums hash tag ya No reforms no election imetibua Hali ya hewa wanufaika wa keki ya Taifa wameanza kutoa milio eti ni upuuzi,kanyagieni hapo hapo,Kila comment ya machawa tia Neno no reforms no election,twende sasa.
Neno no reforms no election
 
Back
Top Bottom