PostGE2025 Gerson Msigwa: Maridhiano ni jambo la hiari sio kulazimishwa

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
"Maridhiano ni jambo la hiari"

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa akizungumza Februari 10, 2026 katika mahojiano na BBC Swahili, amesema endapo kutakuwa na wadau watakaokataa kushiriki kwenye maridhiano mara mchakato huo utakapoanza, hawatalazimishwa kufanya hivyo kwani kushiriki kwenye maridhiano ni zoezi la hiyari.

"Maridhiano ni jambo la hiari"

Je, taifa la Tanzania limeanza kupona kutokana na ghasia za uchaguzi mkuu wa mwaka uliopita?

Hamida Abubakar alizungumza na msemaji wa serikali ya Tanzania Gerson Msigwa ambaye pia amepuuzia mbali hatua ya upinzani ya kususia maridhiano
View attachment 3542211
Kiburi cha madaraka? Msigwa kuna kesho!

Soma hii ujue kiwa kuna kesho

TEMBELEA HOSPITALI,

Tembelea hospitali,
- ukauone unyonge wa mwanadamu. Ukaone jinsi miili yetu iliyojaa nguvu leo inavyoweza kusalishwa na maumivu. Hata wale waliokuwa na sauti kuu, leo wanalala vitandani wakiomba msaada wa kugeuzwa upande wa pili.
Tembelea hospitali,
- ukaione thamani ya pumzi unayoivuta bure. Utawaona ndugu zetu wanaolipia mamilioni ya pesa ili tu mashine iwasaidie kupata hewa unayoipata wewe ukiwa umelala au unatembea. Utajifunza kuwa uhai si haki yako, bali ni neema tu.
Tembelea hospitali,
- ukauone ukomo wa elimu, vyeo, na madaraka. Katika korido za wodini, hakuna profesa wala fundi, hakuna bosi wala kibarua; wote wamevalishwa mavazi yanayofanana, wakisubiri kudra za Muumba na mikono ya matabibu. Hapo ndipo utajua kuwa cheo ni dhamana, lakini afya ni utajiri mkuu.
Tembelea hospitali,
- ukajifunze maana ya uvumilivu na tumaini. Ukawaone wale ambao wamekaa wodini kwa miezi, wakitabasamu kwa kila hatua ndogo ya nafuu wanayoipata. Utajifunza kuacha kulalamika kuhusu chakula usichokipenda au nguo usizozitaka, maana kuna mtu anaomba tu aweze kumeza tone la maji bila maumivu.
Tembelea hospitali,
- ukauone upendo wa kweli. Utawaona ndugu wanaokesha bila kulala, wakifuta jasho na kuliwaza wagonjwa wao. Utajifunza kuwa watu ni bora kuliko vitu, na kuwa na mtu wa kukushika mkono wakati wa dhiki ni baraka isiyo na mfano.
Tembelea hospitali,
- ukajikumbushe kumshukuru Mungu kwa kila kiungo chako kinachofanya kazi. Utawaona waliofungwa bandeji, waliopoteza viungo, na wale ambao akili zao zimechoka. Utatoka hapo ukiwa na moyo wa shukrani, ukijua kuwa "Mzima ana matumaini, lakini mgonjwa ana hitaji moja tu—kuwa mzima."
Tembelea hospitali,
- ukakumbushwe kutumia muda wako vizuri ukiwa na nguvu. Fanya kazi kwa bidii, saidia wenye uhitaji, na hubiri amani; maana siku za giza zikija, utatamani ungekuwa umefanya mengi zaidi wakati wa nuru.
TEMBELEA HOSPITALI,
- Ukajifunze unyenyekevu na kumpenda jirani yako. Maisha ni kama upepo, yanapita haraka sana. Jitahidi kuacha alama ya wema kila unapopita, ili hata ukidhoofika, kumbukumbu za wema wako ziwe dawa kwa waliovunjika moyo.
TUMWOMBE MUNGU –
atujalie afya ya mwili na roho, na atupe mioyo ya huruma kwa wanaoteseka, tukiwakumbuka daima katika maombi yetu.

Mwenyezi Mungu akutunze na kukulinda na maradhi.
 
Hawa wahuni hawana nia ya nchi hii kuwa na Amani, kwani unaposema maridhiano ni hiari maana yake huweki kipaumbele ya nchi kuwa na utulivu kwani uko tayari kuzungumza na wachache na sio makundi yote ya wananchi na hiyo sio ishara nzuri kwa serikali iliyoingia madarakani kwa nguvu!!
Mkiendelea kushupaza shingo mkidhani kuwa ndio mmetoboa mtakuwa mnajidanganya kwani mtakuwa mnaahirisha tu matatizo ya nchi na kudumaza maendeleo! Hiyo miradi haiwezi kutekelezwa kwa ufanisi iwapo nchi haijawa tulivu.
 
ni kweli ..mtu mwema hana budi kuridhiana
 
"Maridhiano ni jambo la hiari"

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa akizungumza Februari 10, 2026 katika mahojiano na BBC Swahili, amesema endapo kutakuwa na wadau watakaokataa kushiriki kwenye maridhiano mara mchakato huo utakapoanza, hawatalazimishwa kufanya hivyo kwani kushiriki kwenye maridhiano ni zoezi la hiyari.

mbona WASIRA THE GREAT alisema watakaa jela milele
 
Hata wakati wa uchaguzi walifiliri kuwa wataweza kufanya walitakalo,lakini matokeo yao waliweza kuyaona. Walishikilia misimamo ya kujiamulia watakavyo, lakini CDM ikiungwa mkono na wananchi waliokuwa wengi ikawaambia No Reforms, No Election.

Ni kweli, serikali ikaweka pamba masikioni, watawala waliokaza shingo zao pamoja tume isiyokuwa huru vikashindwa kuendesha chaguz,na hatimaye ukavurugika na kupelekea mauaji ya kimbari. Wahusika wa uovu huu bado kuna suala lao linafukuta huko ICC.

Viongozi hao hao haramu, waliotokana na uchaguzi batili, leo tena wanakuja na kiburi cha uzima, na kutaka kulazimisha maridhiano pasipo kuona haja ya kuwashirikisha wadau muhimu ikiwemo CDM kikiwa ni chama muhimu sana katika maridhiano.

Wanamchi wazalendo bado wanasisitiza kuwa hakuna maridhiano pasipo kujulikana kwa ukubwa wa tatizo pamoja na uwajibikaji wa wale wote waliohusika kwa yale yaliyotea kabla, wakati, na baada ya uchaguzi.

Watawala bado wamejaa kiburi cha uzima. Hawaoni haja ya kufanya forensic investigation ili chanzo halisi cha tatizo kijulikane na pia ukubwa wa tatizo ubainike. Watuhuniwa wakuu wamekimbilia kuunda tume yao wenyewe ya uchunguzi ili ipaye kujichunguza yenyewe huku wajumbe wa tume hoyo wakiwa hawaaminiki mbele ya wananchi.

Waswahili tuna misemo, asiyesikia la mkuu huvunjika mguu,, sikio la kufa halisikii dawa, sikio lisikilizalo haliwezi kukatwa kichwani, Kwa mara nyingine muda utakuwa ni shahidi mzuri wa yale yajao.
 
Ulevi na ulafi wa madaraka ndo maana hawajali, na wako tayari kufanya unyama wowote kusudi wabaki madarakani
 
Kiburi cha madaraka? Msigwa kuna kesho!

Soma hii ujue kiwa kuna kesho

TEMBELEA HOSPITALI,

Tembelea hospitali,

- ukauone unyonge wa mwanadamu. Ukaone jinsi miili yetu iliyojaa nguvu leo inavyoweza kusalishwa na maumivu. Hata wale waliokuwa na sauti kuu, leo wanalala vitandani wakiomba msaada wa kugeuzwa upande wa pili.
Tembelea hospitali,
- ukaione thamani ya pumzi unayoivuta bure. Utawaona ndugu zetu wanaolipia mamilioni ya pesa ili tu mashine iwasaidie kupata hewa unayoipata wewe ukiwa umelala au unatembea. Utajifunza kuwa uhai si haki yako, bali ni neema tu.
Tembelea hospitali,
- ukauone ukomo wa elimu, vyeo, na madaraka. Katika korido za wodini, hakuna profesa wala fundi, hakuna bosi wala kibarua; wote wamevalishwa mavazi yanayofanana, wakisubiri kudra za Muumba na mikono ya matabibu. Hapo ndipo utajua kuwa cheo ni dhamana, lakini afya ni utajiri mkuu.
Tembelea hospitali,
- ukajifunze maana ya uvumilivu na tumaini. Ukawaone wale ambao wamekaa wodini kwa miezi, wakitabasamu kwa kila hatua ndogo ya nafuu wanayoipata. Utajifunza kuacha kulalamika kuhusu chakula usichokipenda au nguo usizozitaka, maana kuna mtu anaomba tu aweze kumeza tone la maji bila maumivu.
Tembelea hospitali,
- ukauone upendo wa kweli. Utawaona ndugu wanaokesha bila kulala, wakifuta jasho na kuliwaza wagonjwa wao. Utajifunza kuwa watu ni bora kuliko vitu, na kuwa na mtu wa kukushika mkono wakati wa dhiki ni baraka isiyo na mfano.
Tembelea hospitali,
- ukajikumbushe kumshukuru Mungu kwa kila kiungo chako kinachofanya kazi. Utawaona waliofungwa bandeji, waliopoteza viungo, na wale ambao akili zao zimechoka. Utatoka hapo ukiwa na moyo wa shukrani, ukijua kuwa "Mzima ana matumaini, lakini mgonjwa ana hitaji moja tu—kuwa mzima."
Tembelea hospitali,
- ukakumbushwe kutumia muda wako vizuri ukiwa na nguvu. Fanya kazi kwa bidii, saidia wenye uhitaji, na hubiri amani; maana siku za giza zikija, utatamani ungekuwa umefanya mengi zaidi wakati wa nuru.
TEMBELEA HOSPITALI,
- Ukajifunze unyenyekevu na kumpenda jirani yako. Maisha ni kama upepo, yanapita haraka sana. Jitahidi kuacha alama ya wema kila unapopita, ili hata ukidhoofika, kumbukumbu za wema wako ziwe dawa kwa waliovunjika moyo.
TUMWOMBE MUNGU –
atujalie afya ya mwili na roho, na atupe mioyo ya huruma kwa wanaoteseka, tukiwakumbuka daima katika maombi yetu.

Mwenyezi Mungu akutunze na kukulinda na maradhi.
Unawapigia mbuzi gitari?
 
Kabla ya maridhiano toeni kwanza ripoti ya marehemu mzee kibao.
Kesi za waliopotea na kutekwa zianzishiwe uchunguzi.alafu ndo mtangaze maridhiano.
 
"Maridhiano ni jambo la hiari"

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa akizungumza Februari 10, 2026 katika mahojiano na BBC Swahili, amesema endapo kutakuwa na wadau watakaokataa kushiriki kwenye maridhiano mara mchakato huo utakapoanza, hawatalazimishwa kufanya hivyo kwani kushiriki kwenye maridhiano ni zoezi la hiyari.

Wao wanaamini hizo vurugu zilisababishwa na kutoelewa ndani ya ccm kwa hiyo hayo makundi yakiridhiana mchezo utakuwa umeisha.
 
Kila siku wanakuja na hoja ya maridhiano, tukiwauliza yanayohusu maridhiano wanakimbia

1. Kwani wanaoridhiana ni akina nani, wanaridhiana kwa sababu gani?
2. Uchaguzi umekkwisha washindi wamepatikana, maridhiano ya kitu gani?
3. CCM imeshinda viti Bungeni na Urais kwa wastani wa 97%. Walioshindwa wamekubali matokeo. Maridhiano ya nini?
 
Back
Top Bottom