Ukistaajabu ya Musa utayaona ya firauni!Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anahitaji klabu ya Yanga ijitahidi na kufika fainali ya kombe la mabingwa barani Afrika.
Ameyazungumza hayo akiwa anawakabidhi zawadi ya goli la mama fedha taslim Milion 10 baada ya ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Wiliete ya Angola.
Na huu ni wakati wa kampeni za uchaguzi. Hivi hii sio rushwa, kwa faida ya uchaguzi?Si kwa ubaya hivi hiki kifungu Cha kugawa Huwa kinatoka kwa mfuko wa nani?