Gerson Msigwa: Serikali haiwezi kuajiri kila mhitimu wa Chuo

Gerson Msigwa: Serikali haiwezi kuajiri kila mhitimu wa Chuo

Kuna Vitu Tanzania huwa tunajitakia Wenyewe..

Lets say Tukipunguza Mishahara Ya Wabunge Kutoka milion 18 na Tukaishusha mpaka Milion 8 Je kwa Pesa inayobaki Inaweza Kuajiri walimu wangapi na wanaweza Kutumika Wapi walimu hao...

Ngoja tufanye hesabu, tunaweza kuona ni walimu wangapi wangeajiriwa ikiwa mishahara ya wabunge ingepunguzwa kutoka milioni 18 hadi milioni 8 kwa mwezi.

1. Mshahara wa sasa wa wabunge:

Kila mbunge analipwa milioni 18 kwa mwezi.

Kwa wabunge 393, jumla ya mshahara kwa mwezi ni:

18,000,000 X 393 = 7,074,000,000 { (Tsh 7.074 bilioni)}


2. Lets say tumeshusha Mshahara wabunge (milioni 8):

Ikiwa kila mbunge atalipwa milioni 8, basi jumla ya mshahara kwa wabunge wote itakuwa:

8,000,000 X 393 = 3,144,000,000 { (Tsh 3.144 bilioni)}


3. Kiasi kinachookolewa kwa mwezi:

Pesa inayookolewa ni:

7,074,000,000 - 3,144,000,000 = 3,930,000,000 { (Tsh 3.93 bilioni)}


4. Idadi ya walimu wanaoweza kuajiriwa:

Ikiwa mshahara wa mwalimu mmoja ni Tsh 700,000 kwa mwezi, basi idadi ya walimu wanaoweza kulipwa kwa pesa iliyookolewa ni:

3,930,000,000 ÷ 700,000= 5,614

Kama Tutapunguza Mishahara ya Wabunge tunaweza kuajiri walimu 5,614 kwa mshahara wa Tsh 700,000 kila mmoja kwa mwezi
Umetumia nguvu kubwa sana kuua mende mkuu najua chawa wa mama wataku attack sn
 
Back
Top Bottom