Gerson Msigwa: Serikali inajua kila kitu kinachoendelea. Yoyote anayefanya makosa anaweza kufikiwa

Rekebisheni mambo yanayolalamikiwa muone kama.watu watatukana. Acha kukimbilia kusema sijui vyombo vya habari vinatumiwa na watu walioko nje. Hayo ni yako na wenzake. Tatueni kero za wananchi zinazosababisha watukanwe.

Kama mtu anadiriki kusema yeye ni chura kiziwi maana yake hata watu wakizungumzaje hawezi kusikiliza. Sasa kama hawasikilizi watu, hayo wanayosema yanawauma Nini?

Bora watu waseme ili kupunguza hasira zao. Ogopa watu wanaonyamazia kila jambo. Waacheni watu wateme nyongo japo mlishajiita chura kiziwi, na hayo matusi yao msiyasikilize.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…