Gerson Msigwa: Serikali inawasiliana na watoa huduma wa mitandao ya WhatsApp, Facebook na Instagram kuhusu kukosekana kwa huduma

Gerson Msigwa: Serikali inawasiliana na watoa huduma wa mitandao ya WhatsApp, Facebook na Instagram kuhusu kukosekana kwa huduma

Ngariba1

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2017
Posts
1,829
Reaction score
3,807
Msemaji mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa ametoa wito kwa wananchi wote kuwa watulivu wakati serikali inawasiliana na makampuni ya WhatsApp, Facebook na Instagram kuhusu changamoto ya kukosekana kwa huduma ya mawasiliano ya mitandao hiyo.

Huduma za mitandao hiyo zilikwama kwa saa kadhaa tarehe 04 Oktoba 2021.

Taarifa hiyo ya wito wa serikali iliyotolewa usiku wa tarehe 4 Oktoba 2021 haikuwezekana kusambaa haraka kama ilivyo kawaida kwa kuwa mitandao hiyo ya kijamii haikuwa hewani.

Hata hivyo, baada ya juhudi mbalimbali za wataalamu huduma hizo zilirejea baadae usiku wa kuamkia tarehe 05 Oktoba 2021.

Kwa hatua hiyo serikali imeonesha kujali wananchi wake na kuthamini umuhimu wa mawasiliano. Pongezi kwa serikali.



Huduma ilivyorejeshwa, msemaji mkuu wa serikali alitumia kurasa zake za mitandao ya kijamii kutaarifu kuhusu kurudi kwa huduma hiyo.
 
Hivi hizi FB, twitter and Insta, si private entities au ni public bodies? Siku mmiliki wao akisema anaifunga kwa sababu tu ya kuchoka kupokea fedha, tutakimbilia wapi kama serikali? Kwanini serikali yetu nayo isianzishe kitu kama huko Egypt ambayo FB imepigwa marufuku au kama huko China wenye wechat au Russia wenye telegram?
 
Huyu naye aache sifa za kijinga sasa..kama wanajali kweli wapambanie kilio cha wananchi juu ya bei kubwa za vifurushi vya mitandao ya simu.

Serikali ina mengi ya kufanya aisee na sio kutia aibu kwa kuwasilian na Facebook Inc na wakati wameshatoa taarifa kuwa ni tatizo la dunia nzima kuwauliza nini tatizo kwa sasa ni kuonyesha jinsi ulivyo outdated
 
"hii ni serikali sikivu na inayojali wananchi wake" mwehu mmoja alisikika tokea mitaa ya Lumumba.
 
Back
Top Bottom