Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa, leo Julai 8, 2023 amesema kuwa tozo kwenye miamala ya kutoa pesa haijafutwa.
"Tozo imefutwa kwenye utumaji ama usafirishaji wa fedha kupitia kwenye mifumo, ukituma wewe fedha kupitia kwenye simu yako kwenda kwenye simu nyingine, ile tozo tuliyokuwa tunaipigia kelele imefutwa, lakini ukienda kutoa fedha kwenye ATM ama kwa wakala ipo" amesema Msigwa.
Pia, amebainisha kuwa lengo la Serikali ni kuhamasisha uchumi usiotumia fedha taslimu ambao dunia ya sasa inahama huko pamoja na kupunguza gharama za uchapishaji wa noti ambapo serikali hutumia fedha nyingi.
Awali, JamiiForums kupitia jukwaa lake la Jamii Check, Julai 6, 2023, ilitoa pia ufafanuzi huu ulioungwa mkono na msemaji wa Serikali hii leo.
Tozo za miamala ya kieletroniki zilizofutwa ni;
- Unapomtumia mtu muamala kutoka simu yako kwenda simu ya mtu mwingine.
- Unapohamisha fedha kutoka akaunti yako ya Benki kwenda akaunti nyingine.
- Unapohamisha fedha kutoka akaunti yako ya Benki kwenda kwenye simu yako.
MATAMKO, MIJADALA NA MATUKIO MENGINE YALIYOTOKEA KWENYE DIGITALI
- Tozo za kutoa pesa kwa wakala na ATM bado hazijafutwa
- Mbunge wa Gairo, Shabiby ataka fedha za bima kwa wote zikatwe kwenye laini za simu
- Nape: Rais Samia alinikataza kujibizana na Watu Mitandaoni
- Rais Samia: Hadi Desemba 2024, Taasisi za Umma na Binafsi ziwe zimetekeleza Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi
- TCRA yawataka Watanzania kutotumia huduma za mawasiliano ambazo hazijaidhinishwa na mamlaka hiyo
- Benki ya I & M yawapiga mkwara mzito wadeni wake, kusambaza picha na madeni yao kama wakopeshaji mtandaoni
- DOKEZO - Taarifa Binafsi zinakusanywa na "Kampuni za Mikopo Mtandaoni" ni Hatarishi kwa Faragha ya Mtu
- App zinazotoa mikopo mitandaoni zina riba kubwa sana, ukichelewa rejesho wanatuma SMS kwa namba zote ulizowasiliana nazo
- Ubalozi wa Marekani - Tanzania wasitisha Miadi ya Wageni kutokana na tatizo la Intaneti
- Mbunge Santiel Kirumba: Kila laini ikatwe Tsh. 50 tujenge barabara
- Nape Nnauye aliyekuambia kuwa wanaoshinda Mitandaoni 24/7 hawachangii katika kuiletea nchi Maendeleo kama uliyoyaona huko Korea ni nani?
- Serikali yaridhia kufuta tozo kwenye miamala ya simu
- Kuelekea 2025 - Kumbusho Dawson aishtaki Serikali kwa kuzima Intaneti wakati wa uchaguzi mkuu 2020
- Kuelekea 2025 - UVCCM waitaka Serikali kuifungia X (zamani Tittwer)