Gerson Msigwa: Tozo kwenye Miamala ya kutoa pesa bado ipo

Gerson Msigwa: Tozo kwenye Miamala ya kutoa pesa bado ipo

ukituma wewe fedha kupitia kwenye simu yako kwenda kwenye simu nyingine, ile tozo tuliyokuwa tunaipigia kelele imefutwa

Msigwa naye ni Empty set ,kwani kelele zilikuwa kwenye kutuma tu? Kelele zilikuwa kote kutuma na kutoa ,hakuna anayetaka tozo ,kama vipi zirudisheni tu maana kwenye kutoa ndiyo kubwa sana na ukiona mtu anaenda kutoa maana yake ndiyo mwenye uhitaji ,anayetuma means ana mzigo kwahiyo hata ukimkata haina shida.
 
Bimkubwa huwa nahisi genge lake linalomzunguka kama halimshauri vizuri, wanamlamba lamba na kumpiga saundi bimkubwa.
 
Ni mwendo ule ule wa kuwahadaa wananchi kiaina, watu wasioaminika kwa kauli zao
 
Msigwa na serikali anayoisemea wote dhulumati tu. Walichopigia kelele Watanzania Hadi wakaambiwa na Mwigulu wahamie Burundi bado hakijaondolewa. Watu walilalamikia jinsi Baba na mama zetu wazee wanavyolazimika kukatwa hela wanazotumiwa na watoto wao kukidhi mahitaji muhimu kama chakula. Unapoacha Tozo kubwa upande wa kutoa ukijidanganya umemsaidia mtumaji huo ni unafiki maana akitaka mzazi wake apate kiwango sitahiki lazima aongeze hela. Akituma chini ya hapo anaumia mzazi Kwa makato yasiyo na huruma.
 
Tozo ya kutoa pesa imeongezeka kwa asilimia 50%
Huu ni ukweli usiosemwa na hawa wababaishaji. Unaondoa Tozo ya kutuma halafu unadabo Tozo ya kutoa unasema umepunguza makali? Hao waandishi wanaowahoji huwa hawana contents kiasi kwamba hawajui kinachoendelea?
 
Tozo zote zipo Msigwa ni muongo!
 
Huyu bwana ana kazi kubwa mno.Na kuna wakati hana budi kutete asichoamini maana 'mkate' nao muhimu kwa ajili ya watoto nyumbani.
 
Kutuma pesa si ilikuwa tunamtumia wakala kutuma inakuwa umekwema makato balaa analo mwenye kutoa huko.
 
Wakuu nadhani Mada hapo juu inajieleza naomba mnisaidie isije ikawa huyu wakala kanipiga!Leo nilienda kutoa hela kwa wakala wa halopesa lakini nikakuta ujumbe unasema tozo ya serikali kiasi cha shilingi 306.00 kimekatwa! Nawasilisha!
 
Kuanzia tarehe 1/7/2023,ilitangazwa kuwa serikali sikivu ya mama imesikia kilio Cha watanzania imeondoa tozo kwenye miamala ya simu,lakini jambo lililofanyika ni usanii tu,tozo zimetolewa kwenye miamala ya kutuma tu lakini kwenye miamala ya kutoa tozo Iko palepale.

Uhalisia uliopo ni watu wachaje sana huweka pesa kwenye simu zao na Kisha kutuma Kwa mtu mwingine,wanafanya hivyo kuepuka gharama za kutuma,wengi wao humpa wakala namba ya simu iliyokusudiwa kutumiwa Hela Kisha wakala anatuma mojakwamoja.

Hivyo serikali imeona miamala hiyo Haina faida kwao imeamua kuondoa tozo,tozo zinazosumbua watu wengi ni za kutoa pesa Kwa wakala ni Si kutuma Kwa mtu mwingine,serikali iache propaganda za kusema wameondoa tozo,tozo Bado ni changamoto.

Nisihamishe mada,suala la kuuza bandari za Tanganyika halikubaliki Kila mtanganyika Hana budi kulipinga Kwa ajiri ya vizazi vijavyo
 
Dah 😞 😞 😞 😞 😞 😞 😞 😞.
Wanajua ukisha weka pesa kutoa ni lazima.
 
Nani kakwambia kwamba bandari inauzwa tatizo lako unawasikiliza wapotoshaji ambao watakosa ulaji bandari ikiendeshwa na muwekezaji na wewe unafata mkumbo hupati manufaa yoyote nyinyi ndio mnaoingizwa kwenye matatizo hao kina slaa na lissu wakiona mambo mazito wanakuwa cheni na wanakumbilia ulaya walikoziweka familia zao.
 
Back
Top Bottom